Changamoto kwa Waandishi wa Habari: (Mwandosya & Mwakyembe Kuundiwa Mzengwe) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Changamoto kwa Waandishi wa Habari: (Mwandosya & Mwakyembe Kuundiwa Mzengwe)

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mtanzania, Apr 23, 2008.

 1. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #1
  Apr 23, 2008
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Hii habari hapa chini toka Raiamwema ni uwongo mtupu. Mwandishi ameshindwa hata kutambua jambo rahisi la kujua kwamba Dr. Mwakyembe sio mjumbe wa NEC ya CCM.

  Acheni kuutumia mkoa wa Mbeya kuendeleza vita ambavyo havipo.

  Sources zangu zote za huko Mbeya zinaonyesha hakuna kitu kama hicho. Baadhi ya waandishi wa habari wana sababu zao za kutaka kuona ugomvi huu unaendelea kwa cost ya wananchi wa Mbeya.

  Hakuna kikao cha kuwajadili Mwandosya na Mwakyembe na wala Prof. hana mpango wa kugombea urais mwaka 2010.

  Inaelekea kuna watu wanakuza hayo maneno kwa faida zao binafsi.


  Mwandosya, Mwakyembe waundiwa mzengwe

  Mwandishi Wetu Aprili 23, 2008


  HASIRA za wanamtandao waliojeruhiwa na sakata la Richmond sasa zimeelekezwa mkoani Mbeya kuhakikisha viongozi wawili maarufu mkoani humo, Profesa Mark Mwandosya na Dk. Harrison Mwakyembe wanamalizwa kisiasa, Raia Mwema imeambiwa.

  Kwa mujibu wa habari ambazo gazeti hili lilizipata mjini Mbeya, hivi karibuni, hasira dhidi ya Mwandosya na Mwakyembe ambao wote ni wajumbe wa NEC ya CCM, zimejengeka baada ya Edward Lowassa kulazimika kujiuzulu uwaziri mkuu kutokana na taarifa ya Kamati Teule ya Bunge kumhusisha na kashfa ya Richmond. Kamati hiyo iliongozwa na Dk. Mwakyembe.

  Aidha, ushindi wa Profesa Mwandosya katika kinyang’anyiro cha kuwania ujumbe wa NEC (Mbeya) dhidi ya Tom Mwang’onda, mtoto wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa, Cornel Apson, umeacha majeraha mabichi CCM mkoani Mbeya.

  Taarifa za uhakika ndani ya chama hicho mkoani Mbeya zinasema kwamba maandalizi ya tuhuma nzito dhidi ya wanasiasa hao wawili ambao pia wana mahusiano ya karibu, yamekwisha kukamilika na kwamba kilichobakia ni kuwaandikia barua za kuwaita kujitetea katika kikao cha Chama kinachotarajiwa kuitishwa hivi karibuni.

  “Maandalizi ya mkakati huu yalianza siku nyingi wakati wa uhai wa Katibu wa CCM mkoani Mbeya, Silvester Kikungwe (marehemu) na sasa inadaiwa kuwa yamekamilishwa na Mwenyekiti mpya wa CCM wa mkoa, Nawab Mulla,” alisema ofisa mmoja wa CCM mkoani humo ambaye kwa sababu za wazi hakutaka jina lake litajwe.

  Ofisa huyo alitoa mfano wa kikao cha Wazee wa Mkoa kilichoitishwa na Mulla kwa lengo la kutoa tamko la kuwatuhumu Mwandosya na Mwakyembe kuwa wanadhoofisha chama, lakini ikashindikana baada ya viongozi wa dini waliohudhuria kikao hicho kupinga utoaji wa tamko hilo bila kwanza wahusika kuitwa kujitetea. Profesa Mwandosya na Dk. Mwakyembe hawakuitwa katika kikao hicho kilichofanyika Februari mwaka huu mjini Mbeya.

  Raia Mwema ilipomtafuta Mulla kueleza kwa undani suala hilo, iliambiwa kuwa alikuwa Dubai, lakini Katibu wake msaidizi, Zongo Lobe Zongo, alithibitisha kwamba kutakuwa na kikao cha CCM Mkoa wa Mbeya hivi karibuni, ingawa alisema hajui ajenda zake.

  “Kwa sasa Mwenyekiti yuko Dubai, lakini ninajua kuwa kutakuwa na kikao siku za karibuni. Ajenda sizijui, kwa sababu sekretarieti ndiyo inayopanga…Wao ndio wanaweza kujua na inawezekana wao wamejadili wakati Mwenyekiti hayupo,” alisema Zongo.

  Hata hivyo, alipodokezwa kuhusu kuwajadili wanachama, ambao CCM Mkoa wa Mbeya inadai wanakigawa chama, Zongo alidai kwamba Mwenyekiti wake hawezi kuruhusu ajenda kama hiyo kujadiliwa kwenye kikao.

  Lakini Raia Mwema imethibitishiwa na vyanzo vingine vya habari kwamba kesi inayotungwa dhidi ya Profesa Mwandosya, Mbunge wa Rungwe Mashariki na Waziri wa Maji na Umwagiliaji, ni ya tuhuma kwamba ameanza mapema maandalizi ya kugombea urais mwaka 2010 kinyume cha taratibu za Chama, na kwamba akipita mitaani mkoani Mbeya baadhi ya watu humwita “Rais” , “Rais”. Tuhuma hizo pia zilipata kuandikwa na gazeti moja la wiki lililo karibu na wanamtandao hao.

  Kuhusu Dk. Mwakyembe, taarifa zinasema kwamba tuhuma zake zimebadilishwa. Awali alikuwa anatuhumiwa kwa kumuunga mkono Profesa Mwandosya katika hicho kinachodaiwa kuwa ni maandalizi ya mapema ya kuwania urais mwaka 2010, lakini sasa anatuhumiwa kwa ukosefu wa utiifu kwa Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa (Mulla).

  Kinachodaiwa kuwa ni ukosefu wa utiifu kwa Mwenyekiti wa Chama wa Mkoa ni hatua ya Dk. Mwakyembe kukubali kupokewa na umati mkubwa wa watu siku aliporejea Kyela baada ya kuwasilisha ripoti ya Kamati Teule ya Bunge kuhusu Richmond ambayo hatimaye ilisababisha kujiuzulu kwa Lowassa, mawaziri Nazir Karamagi na Ibrahim Msabaha.

  Inadaiwa kwamba Mulla alimkataza asishiriki katika mapokezi hayo kwa kuwa hayakubarikiwa na Chama, na kwamba alikasirika zaidi baada ya Dk. Mwakyembe kueleza wakati akihutubia umati huo kwamba alikuwa amezuiwa na yeye (Mulla) kushiriki katika mapokezi hayo.

  Kwa mujibu wa Ofisa huyo wa CCM Mkoa, barua zenye tuhuma dhidi ya wanasiasa hao wawili tayari zimekwisha kutawanywa kwa baadhi ya wabunge wa CCM wa mkoa huo na kwamba njama hizo za kuwamaliza kisiasa Profesa Mwandosya na Dk. Mwakyembe zinaeleweka kwa baadhi ya viongozi waandamizi wa kitaifa wa CCM walio kwenye mtandao na inadaiwa wameubariki mpango huo.

  Baadhi ya wachambuzi wa masuala ya siasa nchini wanaamini kwamba kama kutokuelewana huko kwa CCM mkoa wa Mbeya hakutashughulikiwa, chama hicho kitaupoteza kabisa mkoa huo kwa wapinzani katika uchaguzi wa mwaka 2010.

  “Kampeni hii ya kuwamaliza kisiasa kama itafanikiwa itaiumiza sana CCM mwaka 2010. Kwanza Profesa Mwandosya na Dk. Mwakyembe wana ushawishi mkubwa si tu kwenye majimbo yao bali vilevile mkoa mzima na pia miongoni mwa wabunge wenzao,” alisema.

  Profesa Mwandosya hakupatikana jana kwa simu kuzungumzia suala hilo, lakini Dk. Mwakyembe yeye alipopatikana hakupenda kulizungumzia suala hilo mbali ya kukiri kusikia kuwepo kwa tuhuma hizo dhidi yake.
   
 2. M

  Mwafrika wa Kike JF-Expert Member

  #2
  Apr 23, 2008
  Joined: Jul 5, 2007
  Messages: 5,194
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Kweli kabisa Mtanzania hata mimi hii habari nimeitilia sana shaka na nimejaribu kuwasiliana na mhariri wa raia mwema.
   
 3. Kitila Mkumbo

  Kitila Mkumbo Verified User

  #3
  Apr 23, 2008
  Joined: Feb 25, 2006
  Messages: 3,347
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  Tatizo waandishi wetu hawataki kabisa kufanya research. Uandishi wao unategemea sana mazungumzo ya kwenye vilabu; unaambiwa siku hizi wanatembea na tape recorder kwenye bar, wana record udaku halafu wanaandika kwenye gazeti. It is pathetic. Nafikiri kuna haja ya kuanzisha Jambo Times. Tuna waandishi kibao hapa ambao hawatahitaji hata kulipwa. Tumechoka kulishwa sumu bwana ahaa!
   
 4. Mtu wa Pwani

  Mtu wa Pwani JF-Expert Member

  #4
  Apr 23, 2008
  Joined: Dec 26, 2006
  Messages: 4,095
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  wakiitwa makanja nja wananuna
   
 5. MwanaHabari

  MwanaHabari JF-Expert Member

  #5
  Apr 23, 2008
  Joined: Nov 9, 2006
  Messages: 444
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ...interesting
   
 6. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #6
  Apr 23, 2008
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Mkuu Kitila,

  Wazo zuri sana hilo kuhusu gazeti.
   
 7. J

  Jamco_Za JF-Expert Member

  #7
  Apr 23, 2008
  Joined: Jul 14, 2007
  Messages: 1,315
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Itakuwa vizuri sana maana mtatusaidi kuondokana na makanjanja, wanaopenda posho na kuandika habari zisizofanyiwa utafiti.
   
 8. MwanaHabari

  MwanaHabari JF-Expert Member

  #8
  Apr 23, 2008
  Joined: Nov 9, 2006
  Messages: 444
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  huu ni uandishi duni na wakichochezi tu, kama hiyo mikakati ipo, watu wa mbeya wataidhibiti wenyewe maana wametuonyesha kwamba wana uhuru wa kuchagua wanayotaka. waandishi hatuna sikuhizi
   
 9. Single D

  Single D JF-Expert Member

  #9
  Apr 23, 2008
  Joined: Feb 27, 2007
  Messages: 459
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Asilimia kubwa ya Watanzania wanajua wabunge wanaotetea wanyonge na walioingia bungeni kujishibisha matumbo na kufanya biashara.

  Tunajua yai bovu na zima kwa hiyo hayo mazengwe ya timu ya EL yatakwama yote.Walitaka waendelee kutuibia?

  Buriani hiyo timu inayounda mizengwe kwa watu walio na uchungu na raslimali za Taifa hili.
   
 10. mwanatanu

  mwanatanu JF-Expert Member

  #10
  Apr 23, 2008
  Joined: Jan 22, 2008
  Messages: 850
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 45
  Hapa kuna jambo Nawab Mulla na Rostam ni wote waburushi na wana kaundugu fulani.

  Je ni wale wa mtandao walioumia wana taka kisasi? jamani bongo kuna mlipuko soon
   
 11. Masanja

  Masanja JF-Expert Member

  #11
  Apr 23, 2008
  Joined: Aug 1, 2007
  Messages: 3,595
  Likes Received: 3,762
  Trophy Points: 280
  Over reaction? I dont know..lakini Mtanzania, how do you know kwamba Mwandosya hana NIA ya kugombea Uraisi? are you his secretary kwamba unajua mambo yake yote? Nadhani hii habari inaweza kuwa haina ukweli, lakini vema kuuangalia upande wa pili wa shillingi. In Tanzania hakuna kisichowezekana. Personally najua swala la support ya Mwakyembe kwa Mwandosya lilimcost politically. Anyway sijui hii habari imeanzia wapi au ina umuhimu gani, ila kwa nchi yetu ilivyo anything is possible...
   
 12. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #12
  Apr 23, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,691
  Likes Received: 82,581
  Trophy Points: 280
  Waungwana hata waandishi waliobobea katika nchi za magharibi wanafanya makosa mengi tu. Mara nyingi huomba samahani kwa makosa waliyoyaandika au kuyatangaza na kurekebisha kila kilichoandikwa au kutangazwa.

  Hivyo kwa maoni yangu kama watakuwa tayari kuomba samahani na kusahihisha kile walichokipotosha basi halijaharibika neno.

  Wazo la kuwa na Jambo times ni zuri, lakini kuwa na magazeti mengine kunaongeza ile media freedom ambayo kwa wakati huu ambapo Watanzania tunapambana na mafisadi tunaihitaji sana.
   
 13. U

  Ufunuo wa Yohana JF-Expert Member

  #13
  Apr 23, 2008
  Joined: Oct 9, 2007
  Messages: 317
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 35
  Waandishi wetu mara nyingi huwa hawako makini na wanayoandika. Hali hii ikiachwa iendelee itatufanya tutende dhambi ya uongo bure. Maana unaweza kusoma habari ukaenda kumwambia jirani yako na baadaye wewe ukaonekana muongo.

  Jambo News/Times ni bomba


  Jamani zile T-shirt za JamboForums zimeingia sokoni au nalo lilikuwa ni udaku? I like to have one to beauty my body
   
 14. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #14
  Apr 23, 2008
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  waandishi wa tanzania sometimes wakipata pa kuegemea, huwa hawapaganduki.
  wengi hawafanyi research na wanaandika kile wanachojua watu wanataka kukisikia tu, na sio ukweli weyewe.
   
 15. mwanatanu

  mwanatanu JF-Expert Member

  #15
  Apr 23, 2008
  Joined: Jan 22, 2008
  Messages: 850
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 45
  What we have in TZ ni reporters....we need journalists
   
 16. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #16
  Apr 23, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Mtanzania umesema kweli na ninaamini kuna mambo machache ambayo mwandishi asiyachukulie at face value au kuyakubali tu. Kwa mfano Rais aliposema "watu hawali mapanki" au pale aliposema "BAE ni kampuni ya Serikali ya Uingereza" waandishi hawana budi kuangalia kauli hizo na kuhakikisha ukweli wake. Mtu anaposema fulani ni mwanachama wa chama fulani ni bora uhakikishe anachosema ni sahihi. Nakubaliana na wewe 100% kwamba ni jukumu la wale wanaoandika habari au maoni to be as accurate as humanly possible especially ambapo ni rahisi kuverify certain information.

  Nina tatizo hata hivyo na mahitimisho yako kadhaa.

  Kudai kuwa habari nzima ni uongo mtupu nafikiri ni exaggeration of the first order. Nadhani umeweza kuonesha ni yapi ambayo factually are just simply wrong. Hayo yanayohusiana na facts ni rahisi kuyaweka sawa. Kama hili:

  Nadhani hapa itakuwa ni maneno yako against maneno yao; kwanini tuamini kuwa vita hivyo havipo? aidha kwa sababu havipo au kwa vile umesema havipo?

  Hapa inabidi watu waamini "sources" zako ambazo ni unnamed na hatujui zina maslahi gani katika pande zinazohusika. How balanced are you sources? Maana hilo gazeti na wenyewe wanasema wana "sources" zao hapo hapo Mbeya. Kwanini sources zako ziaminike zaidi ya sources zao?

  Hili nadhani ni kweli kabisa; lakini it is the nature of the beast. Siasa ni moves, counter moves na moves na anti-moves! Jinsi gani waandishi wanashikiri katika michezo hii ya kisiasa? Nadhani ni sehemu yenyewe ya siasa. Kuna uhusiano wa ajabu sana kati ya vyombo vya habari na wanasiasa siyo Tanzania tu bali dunia nzima.

  Wenzako wanasema kipo, wewe unasema hakipo. Mmoja wenu hayuko sahihi. Ni nani? time only will tell. Umesema Prof. hana mpango wa kugombea you might be very right, lakini ukweli wa kauli hiyo utaonekana 2010, kabla ya hapo ni jambo la probability tu. Sasa akigombea 2010 unaweza ukasema in 2008 hakuwa na mpango huo..

  Of course, siasa ndivyo ilivyo. Labda kuna mambo hayapaswi kuwa hivyo (in a perfect world where personal interests are not at play) lakini katika ulimwengu ambao maslahi, matamanio, chuki, hasira, kinyongo, ushabiki, mapenzi nk vipo, utakutana na watu wa namna hiyo.

  Don't be too harsh.
   
 17. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #17
  Apr 23, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,691
  Likes Received: 82,581
  Trophy Points: 280
  Thank you Mkjj! Watu wanataka kuwalaumu waandishi pale wanapofanya makosa ambayo ukiyatathmini athari yake si kubwa kiasi hicho, lakini wakati huo huo wanapoandika mambo mazito kuhusiana na mafisadi hakuna anayewapongeza kwa jitihada zao katika vita dhidi ya mafisadi.
   
 18. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #18
  Apr 23, 2008
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Pia Ujue Maswali Ambayo Mwandishi Anayouliza Ni Yale Anayopewa Na Mhariri Wake Ndio Vyombo Vingi Hapa Tanzania Vinavyofanya Kazi Kwahiyo Anafanya Kazi Kutokana Na Mhariri Wake .

  Yeye Anapopeleka Habari Na Mhariri Akaikubali Sio Kazi Yake Yeye Kuomba Radhi Au Kutoa Maelezo Zaidi Kinachotakiwa Ni Kwa Watuhumiwa Kujitokeza Na Kuongea Chochote Wanachojua Kama Kukanusha Na Mambo Kama Hayo

  Kila Chombo Cha Habari Kina Sheria Na Sera Zake Za Ufanyaji Kazi Pia Kuna Sheria Za Nchi Na Za Vyama Vya Hawa Wanahabari Wana Miiko Yao Pia
   
 19. M

  Mwafrika wa Kike JF-Expert Member

  #19
  Apr 23, 2008
  Joined: Jul 5, 2007
  Messages: 5,194
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Kweli kabisa bubu,

  ndio maana nimekumbusha kuhusu kujaribu kuwasiliana na mhariri wa raia mwema maana inaonekana kuna makosa ya kiufundi zaidi ya nia ya kupotosha habari.
   
 20. mwanatanu

  mwanatanu JF-Expert Member

  #20
  Apr 23, 2008
  Joined: Jan 22, 2008
  Messages: 850
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 45
  Lakini wanapoandika mambo mazito huwa wakiandika jina tunalo lakini tunahifadhi huwa ina niboa sana ni kama vile hawana ujasiri
   
Loading...