Changamoto kwa JF

Pope

Senior Member
Dec 3, 2007
117
0
Makala Hii toka Raia Mwema ni ndefu lakini ni changamoto kwa JF, naomba muisome wadau....Kila mtu akitimiza wajibu wake tutafika.

Muungano Mtakatifu: wabunge, wapiga-filimbi, waandishi Na Jenerali Ulimwengu March 2008.

WAKUU wa chama-tawala walitaka kuufanya mfumo wa "vyama vingi" uwe ni mfumo tasa, usiozaa matunda ya demokrasia na unaofinya hata ile nafasi ndogo ya demokrasia iliyojitokeza mara kwa mara chini ya mfumo wa chama-kimoja.

Kwa kutumia kisingizio cha wapinzani rasmi kuwamo ndani ya Bunge, wabunge kutoka chama-tawala wakazibwa midomo, wakakatazwa kujadili kwa uwazi hata mambo nyeti yanayoliumiza Taifa. Ikawa kila akiinuka mbunge toka chama-tawala atazungumzia mlolongo wa masuala ya ‘kiparokia' tu: barabara ya kutoka Mwisi kwenda Igunga; ile zahanati ya John's Corner; daraja kati ya Makongolosi na Mkwajuni; soko kuu la Kwa Sadala.

Sawa, haya yote ni masuala muhimu kwa watu wanaoishi katika maeneo husika. Lakini hayawezi kufunika kabisa masuala mapana ya kitaifa yanayowaumiza wananchi wote na hata kuinyang'anya Serikali uwezo wa kutekeleza miradi hiyo yote ya kiparokia inayopigiwa kelele na wabunge.

Hata hivyo, nitakuwa sitendi haki kwa baadhi ya wabunge waliodiriki kusimama na kusema kwamba hawaridhishwi na mwendendo wa Serikali katika kuendesha shughuli za Taifa. Baadhi yao walizungumza wazi katika vikao vya hadhara vya Bunge, na wengine walipeleka hoja zao katika vikao vya wabunge wa CCM. Hawakusikilizwa.

Si tu hawakusikilizwa bali baadhi yao walishikishwa adabu na wakuu wa chama chao. Tutakumbuka bila shaka kilichotokea pale baadhi ya wabunge wa chama-tawala katika awamu ya tatu (utawala wa Benjamin Mkapa) walipothubutu kueleza dukuduku lao kuhusu mkataba baina ya Serikali na kampuni ya Afrika Kusini kuhusu uendeshaji wa TANESCO.

Mwenyekiti wa chama-tawala alikwenda katika kikao cha wabunge wake na kuwaambia kwamba hawakuwa na ubavu wa kuupinga mkataba huo; utatekelezwa watake wasitake; na atakayepinga ole wake wakati wa uchaguzi ujao. Kisha akawaambia kwamba amesikia wanasemasema kwamba kuna mabomu yanayohusu ndugu zake kuwamo katika mkataba huo. Akawaonya kwa kusema kwamba hata yeye alikuwa na mabomu ya hao wabunge, na angeyalipua. Hivyo ndivyo viwango tulivyokuwa tumefikia katika kusaka busara ya uongozi.

Wabunge wa CCM walinywea kwa kiwango kikubwa, ingawa wachache miongoni mwao waliendelea kufurukuta mara kwa mara. Kunywea kwa wabunge hao kunaelezeka kutokana na ukweli kwamba, kwa wengi wao, ubunge ni ajira, na tajiri ni mwenyekiti wa chama, na tajiri akisema ruka unaruka. Hapa tukumbushane tena yale niliyosema huko nyuma kuhusu utawala wa Bwana Mkubwa Mbadala wa Mkoloni.

Ingawaje wabunge wa chama-tawala walionekana kukaa kimya kuhusu masuala mengi makubwa lakini hali haikuwa shwari kwa sababu walikuwa wakisononeka mioyoni mwao. Hawa ni wazalendo, watu wenye uchungu na nchi yao, na kwa kweli wangeshangaza kama wasingesononeka.

Wengi wa wabunge wajuzi wa mambo (wapo wengine wa kufuata upepo mithili ya bendera) walisikika wakisema kwamba mambo yanakwenda hovyo, kwamba wanaburuzwa na kunyimwa fursa ya kusema. Mara nyingi waliwasihi watu waliomo ndani ya vyombo vya habari wasiandike hayo waliyoyasema, na kama wakiandika wasiwanukuu kwa majina.

Hapa tunakutana na mantiki ya nguvu ya maji yaliyojengewa ukuta ili yasiingie au kutoka mahali yalipofungiwa. Taratibu, siku hadi siku, yatajikusanya na baada ya muda ama yatapata njia ya kuuzunguka ukuta huo au yatauangusha na kupita. Walichofanya wabunge wa CCM ni kufanya kazi na wabunge wa vyama vya upinzani kwa kuwapa taarifa walizokuwa nazo na kuwataka wazifanyie kazi.

Katika mjadala kuhusu kashfa ya Richmond bungeni hivi majuzi tu, mbunge mmoja wa CCM alisema kwamba alikanywa asiendelee kuisemasema Serikali ya chama chake baada ya kuwa ameiongelea Richmond hiyo hiyo. Akasema kwamba sasa alikuwa ameamua kusema yaliyo moyoni mwake na kwamba hakuna atakayeweza kumyamazisha tena.

Jambo jingine lililotokea ni kule kuzuka kwa watu wanaoitwa wapiga-filimbi (whistleblowers). Hawa ni watu wanaojikuta katika nafasi zinazowawezesha kuona mambo maovu yanayotendeka, na kisha wakatafuta namna ya kuyafanya yajulikane, ama kwa vyombo vya Serikali ama (hususan vyombo vyenyewe vinapokuwa vimeoza) kwa umma mzima kupitia vyombo vya habari.

Hawa pia ni wazalendo (ingawa wapo wanaosukumwa na sababu nyingine) wanaoumizwa na mambo yanayofanyika machoni mwao, na wangependa wananchi wayajue ili watafute njia za kukabiliana nayo. Hivi sasa kila idara ya Serikali kuna wapiga-filimbi ambao wamekuwa wakiifanya kazi hii.

Hivyo ndivyo taarifa nyeti na za siri kubwa kuhusu mikataba inayojadiliwa leo zimekuwa zikianikwa hadharani mara kwa mara. Mkuu wa idara yo yote ya serikali anayedhani kwamba kubandika muhuri ulioandikwa SIRI ni kinga dhidi ya kujulikana kwa maudhui ya jalada husika, anajidanganya, kwani, siri si ya watu wawili.

Wapiga-filimbi wamo pia katika makampuni binafsi na wamekuwa wakitoa habari kuhusu utapeli, ukwepaji kodi, bidhaa bandia nk. ndani ya makampuni hayo. Hali ni hiyo hiyo katika asasi zisizo za kiserikali zinazojihusisha na utapeli kinyume na katiba zake, na asasi nyingine za kiraia zinazokiuka misingi ya usajili wake. Tunaweza kusema kwamba kadri tutakavyokuwa na wapiga-filimbi wengi ndivyo tutakavyoweza kupambana na ufisadi na kuupunguza katika maeneo yote ya maisha yetu.

Kiunganishi kikuu katika mapambano haya bila shaka ni vyombo vya habari, ambavyo vimefanya kazi kubwa kufanikisha juhudi za wabunge wazalendo (toka chama-tawala na vyama vya upinzani), wapiga-filimbi na wanaharakati wa masuala mbali mbali katika kupambana na ufisadi katika nyanja mbali mbali na kupigania uwazi mkubwa zaidi na demokrasia pana zaidi.

Vyombo vya habari nchini vimedhihirisha yale madai kwamba ni Muhimili wa Nne wa dola kwa kutangaza wasemayo wabunge wazalendo, kusambaza yatokanayo na wapiga-filimbi kutoka idara mbalimbali za serikali na makampuni binafsi, na kwa kuandika au kusoma tahariri zinazoshinikiza uchukuaji wa hatua dhidi ya watuhumiwa.

Bila vyombo vya habari matamshi na makabrasha yanayotolewa na hawa wanaharakati wengine yangeishia katika kundi la watu wachache na yasingekuwa na ushawishi wo wote kwa umma usio na taarifa za msingi. Hivi sasa, sura mpya ya vyombo vya habari imeanza kuonyesha makucha yake: mtandao au Internet.

Kwa muda mrefu, sheria zetu zimepigiwa kelele kwamba zinabana uhuru wa raia kwa ujumla, na mahsusi uhuru wa vyombo vya habari kutokana na vipengele vinavyojinaisha (neno hili ninalibuni kumaanisha ‘criminalise') makosa ambayo kinadharia yangehusishwa na madai ya kiraia. Ni baadhi ya sheria zilizomulikwa na Jaji Mkuu Francis Nyalali na tume yake ikashauri zifutiliwe mbali, lakini Serikali yetu ikawa na mawazo tofauti.

Kuingia kwa internet katika mchakato wa kupashana habari na kupiga filimbi dhidi ya ufisadi kumepunguza sana makali ya sheria hizo zinazojinaisha makosa ya uandishi. Hii ni kwa sababu mtandao u wazi kwa kila mmoja wetu na ni njia mwafaka kwa mpiga-filimbi kupuliza kipenga chake bila kuogopa kushitakiwa kwa kosa la jinai.

Bila shaka waliozoea vya kunyonga watatafuta njia za kudhibiti hata hili, lakini kwa sasa mtandao umetufanyia kazi nzuri. Ni wazi kwamba si kila kinachoandikwa kwenye mtandao ni kweli. Hakika, hiyo kinga yenyewe aliyo nayo mwandishi kwa kutojitambulisha inakinzana na dhana ya uwajibikaji wa mtoa-habari, na kwa hilo tu, ‘habari' anazozitoa zinastahili kutiliwa shaka.

Naamini hili ndilo alilotaka kusema Spika Sam Sitta alipowaasa wabunge wasiwe wepesi kuchukua habari kutoka katika mtandao wa internet, na akasema hivyo kwa namna iliyoashiria kwamba hakuziona kama zenye uzito wa kuaminika. Hilo lilihusu hoja iliyoibuliwa na Mbunge wa Karatu, Wilbroad Slaa kuhuse kile alichokiona kama kashfa ndani ya Benki Kuu (BOT).

Lakini thamani ya ‘habari' za aina hii ni kwamba ni dokezo, ‘tip' kwa ye yote anayetaka kufanya utafiti zaidi, awe ni mwandishi wa habari, asasi ya Serikali, mwenye mali iliyoibwa au mtu mwingine ye yote aliyeelemewa na nguvu za udaku. Imehalisi kwamba habari zile zile alizozikejeli Spika Sitta zimedhihirka kwa kiasi kikubwa mara wakaguzi walipozichunguza.

Muungano mtakatifu umeanza kujengeka kati ya wabunge (wa vyama vyote, wapiga-filimbi, wanaharakati na vyombo vya habari) na makali yake tumeyaona hivi karibuni. Huu unaweza kuwa ni mwanzo tu.
 
Tunarudi Kule Kule

Jamani Wanachama

Munapoweka Makala Au Chochote Basi Muwekaji Aandike Kwa Ufupi Anachoona Yeye Au Kufikiria Kabla Ya Kuleta Kwa Wengine

Hii Italeta Changamoto Kwa Watazamaji Na Wachangiaji Wengine

Unataka Kila Mtu Asome Makala Hiyo ?
 
SHY toa hoja baada ya kusoma mwandishi hakusaidii unataka ukamchomee ? Soma hoja ndiyo hasa inatakiwa .Jibu hoja kujua nani naandika haina maana kwako .
 
Hapana

Kwanza Yeye Atupe Mawazo Yake Na Ndio Wengine Tufuatie

Tujue Kwanini Yeye Ameleta Makalahiyo Mahala Hapa Nayeye Anafikiria Nini

Sio Kuweka Na Kukimbia

Ahsante
 
Hapana

Kwanza Yeye Atupe Mawazo Yake Na Ndio Wengine Tufuatie

Tujue Kwanini Yeye Ameleta Makalahiyo Mahala Hapa Nayeye Anafikiria Nini

Sio Kuweka Na Kukimbia

Ahsante

Unataka mawazo gani na wakati kesha sema kupitia makala yake ama bado ni mie sielewi kitu hapa ? Ama kweli ukiwa CCM unakuwa kiziwi, fisadi, kipofu na mengine mengi na hata kulewa madaraka mtoto mdogo unasema nyie CCM hamtaki kuwapa CUF madaraka .Shame on you .
 
Wewe

Tazama Uzuri

Hiyo Makala Imeandikwa Na Jenerali

Sasa Unataka Kusema Pope Ndio Jenerali Ulimwengu ? Yule Mamluki Wakinyarwanda ?

Mbona Unakuwa Hiyo Wewe

Usikurupuke
 
Wewe

Tazama Uzuri

Hiyo Makala Imeandikwa Na Jenerali

Sasa Unataka Kusema Pope Ndio Jenerali Ulimwengu ? Yule Mamluki Wakinyarwanda ?

Mbona Unakuwa Hiyo Wewe

Usikurupuke

Bwana mdogo Maro tunajua unavyo hangaika na kuganga njaa yako .Umeleta balaa JF na badio hakuna aliyekuita Mamluki na uko hapa leo Ulimwengu mtu ambaye anaweza kukuzaa mara kibao unamwita majina haya ? Yona Maro unaweza kusimama mbele ya Ulimwengu na kusema haya ? Mnyarwanda tangia lini ? CCM mlipo mpta vyeo ndani ya Chama na hada Ubalozi hamkujua haya ama ndiyo sasa unaonyesha makucha kwamba umekuwa traitor sirini sasa unachomoa makucha ?
 
Sasa Itabidi Tuanzishe Mjadala Mpya Kuhusu Uraia Wa Jenerali Ulimwengu Manake Wamezidi Kuwaandama Wengine

Naamini Hii Itakuwa Ni Changamoto Nyingine Kwetu Kama Wanachama Huru Wa Jf
 
Sasa Itabidi Tuanzishe Mjadala Mpya Kuhusu Uraia Wa Jenerali Ulimwengu Manake Wamezidi Kuwaandama Wengine

Naamini Hii Itakuwa Ni Changamoto Nyingine Kwetu Kama Wanachama Huru Wa Jf

Kila mmoja sasa amesha kujua kwamba ni traitor na Mkapa alijaribu akashindwa na wewe kwa kuwa unajifanya mwandishi na mchambuzi omba Audience na Ulimwengu mwaga utumbo wake mbele yake na uende kwenye blogu zako andika na si hapa JF.Sasa tutakubana Mbavu kila kona hadi uache uchakubimbi.Ulimwengu is fighting for the poor ambao wewe umeamua kuwa Yuda unakula kwa kuwaumiza .Wakubwa zako CCM thye cannot touch him itakuwa wewe mtoto mdogo bado? Si unajifanya mchambuzi wa ICT na mambo ya siasa kamvae uso kwa uso muulize juu ya Urais wake uone uacha majungu mjinga wewe .

Mbona wewe watu wanajua kamba umezaliwa na Mkikuyu na watu badi hawasemi walete hapa kujua kama wewe ni mtanzania ama Mkenya ?
 
Ahahhaa

Kumbe Mimi Ni Mkikuyu Sikujua

Nitarudi Kwetu Kwenya Nikaone Simba Na Wenzake Katika Nairobi National Park

Ahshss
 
Kila mmoja sasa amesha kujua kwamba ni traitor na Mkapa alijaribu akashindwa na wewe kwa kuwa unajifanya mwandishi na mchambuzi omba Audience na Ulimwengu mwaga utumbo wake mbele yake na uende kwenye blogu zako andika na si hapa JF.Sasa tutakubana Mbavu kila kona hadi uache uchakubimbi.Ulimwengu is fighting for the poor ambao wewe umeamua kuwa Yuda unakula kwa kuwaumiza .Wakubwa zako CCM thye cannot touch him itakuwa wewe mtoto mdogo bado? Si unajifanya mchambuzi wa ICT na mambo ya siasa kamvae uso kwa uso muulize juu ya Urais wake uone uacha majungu mjinga wewe .

Mbona wewe watu wanajua kamba umezaliwa na Mkikuyu na watu badi hawasemi walete hapa kujua kama wewe ni mtanzania ama Mkenya ?

KUNA WATU WAKOTAYARI HATA KUJITOA MHANGA UKIBISHA KILE ANACHOSEMA

BWANA /BIBI LUNYUNGU

SIO LAZIMA KILA KILA UNACHOSEMA KIKUBALIWE -- NDIO MAANA WEWE UPO HUKU NA MIMI NIPO KULE

AHSANTE
 
Naomba kurudi kwenye Mada...
Kiufupi Makala inasema Wapiga filimbi (ambao ni pamoja na Jambo Forums) wanasaidia kutoa Source za informations za scandals ambazo zimo ndani ya Serikali ya CCM na wabunge wa CCM kutokana na mfumo Dume ulipo wanashindwa kuikosoa Serikali kwani akifanya hivo adhabu yake ni kubwa hivyo basi yanayotokea mengi yanatolew na watu ambao wamo ndani ya system lakini hawapendi kuona jinsi system inavyoharibu na kuamua kuvujisha siri kupitia kwenye vyanzo vingine vya habari.

Kimsingi hoja ina mantiki na kweli kama tukiwa serious ni rahisi kupata vyanzo vingi na mambo mengi kufumbuka katika huu mfumo dume uliopo!!

Shy umenipata?
 
Bwana

Pope

Ahsante Kwa Ufafanuzi Wako Na Hii Ndio Inatakiwa Sasa Na Wengine Waige Mfano Ili Kuweza Kwenda Vizuri Na Mambo

Hizi Data Zinazoletwa Humu Wakati Mwngine Tunaweza Kuwashutumu Watu Wanaoshugulika Na Usalama Wahizo Huko Maofisini Nasehemu Zingine

Mfano Unaweza Kukuta Mkataba Fulani Ulihifadhiwa Katika Server Fulani Server Hiyo Ina Access Levels Na Kadhalika Lakini Maajabu Wengine Wanaweza Kuingia , Kuangalia Na Kuweka Katika Flashdisk Zao Au Kuweza Kuupload Katika Forums Na Sehemu Zingine Huo Ni Udhaifu Wa Mfumo Wa Mitandao Katika Sehemu Husika .

Katika Kazi Zetu Moja Ya Sehemu Tunazofanya Kazi Ni Katika Office Za Umoja Wa Ulaya Pale Computer Zote Zimeunganishwa Katika Domain Ambapo Main Iko Brussels Na Zingine Mbili Ziko Palepale

Kila Unachofanya Na Kusave Katika Computer Yako Copy Inaenda Katika File Server Kisha Inahifadhiwa Katikatape Ambayoikokatikahiyo Server -- Ukitaka Kuona Report Ya Fulani Alifanya Nini Alisave Nini Aliweka Nini Katika Computer Yake Unacheck Katika Backuputaona Vingine

So As Hapa Ingefanyika Hivyo Kwa Njia Ya Backup Kwahiyo Scandal Iki Vuja Basi Tutaenda Katika Server Kwanza Access Levels Tutaangalia Katika Backup Nani Alifanyavipi Na Vipina Hiyo Kitu Ilikuwa Kwa Nani Alitembelea Site Gani

Kwa Hakika Watashikwa Nakufikishwa Katika Vyombo Vyasheriamara Mojakama Kamatukiwa Namfumoimara

Halafu Taasisi Hizi Ziwe Na Kitu Kinachoitwa Internet Usage Agreement Na Watie Sahihi
 
Bwana Shy!! (Natumai ni BWana)
Point haiko hapo.
Point ni kuwa hao wanaokereka ndio wanaotoa hizo Scandal kwa Whistle Blowers, then zinawafikia watu kama akina Zitto.

Kiufupi ni kwamba Mfumo wa CCM ndio unaowapa umaafufu akina Zitto.
Kama ningekuwa mimi mwandishi wa MNakala ndio ningeipa kichwa hicho. Kwani akina Zitto wanalishwa na vyanzo kutoka ndani ya CCM.
 
Bwana

Pope

Ahsante Kwa Ufafanuzi Wako Na Hii Ndio Inatakiwa Sasa Na Wengine Waige Mfano Ili Kuweza Kwenda Vizuri Na Mambo

Hizi Data Zinazoletwa Humu Wakati Mwngine Tunaweza Kuwashutumu Watu Wanaoshugulika Na Usalama Wahizo Huko Maofisini Nasehemu Zingine

Mfano Unaweza Kukuta Mkataba Fulani Ulihifadhiwa Katika Server Fulani Server Hiyo Ina Access Levels Na Kadhalika Lakini Maajabu Wengine Wanaweza Kuingia , Kuangalia Na Kuweka Katika Flashdisk Zao Au Kuweza Kuupload Katika Forums Na Sehemu Zingine Huo Ni Udhaifu Wa Mfumo Wa Mitandao Katika Sehemu Husika .

Katika Kazi Zetu Moja Ya Sehemu Tunazofanya Kazi Ni Katika Office Za Umoja Wa Ulaya Pale Computer Zote Zimeunganishwa Katika Domain Ambapo Main Iko Brussels Na Zingine Mbili Ziko Palepale

Kila Unachofanya Na Kusave Katika Computer Yako Copy Inaenda Katika File Server Kisha Inahifadhiwa Katikatape Ambayoikokatikahiyo Server -- Ukitaka Kuona Report Ya Fulani Alifanya Nini Alisave Nini Aliweka Nini Katika Computer Yake Unacheck Katika Backuputaona Vingine

So As Hapa Ingefanyika Hivyo Kwa Njia Ya Backup Kwahiyo Scandal Iki Vuja Basi Tutaenda Katika Server Kwanza Access Levels Tutaangalia Katika Backup Nani Alifanyavipi Na Vipina Hiyo Kitu Ilikuwa Kwa Nani Alitembelea Site Gani

Kwa Hakika Watashikwa Nakufikishwa Katika Vyombo Vyasheriamara Mojakama Kamatukiwa Namfumoimara

Halafu Taasisi Hizi Ziwe Na Kitu Kinachoitwa Internet Usage Agreement Na Watie Sahihi

Mkuu shy, mimi nakushangaa jambo moja, unaonekana upo pesmistic, unapinga jitihada za WAZALENDO wanazofanya ili kufichua UFISADI. Inavyoonesha, hupendezwi na wala hujapendezwa na sakata la RICHMOND. nahisi upo upande wa mafisadi (samahani kama ninakosea).

Wapiga filimbi endeleeni, mnafanya kazi njema katika vita ya kulikomboa taifa.
 
Je Kuna Sehemu Nimeshawahi Kuandika Kwamba Napingana Na Hilo Kundi La Watu Unalolisemea?

suala la kushawishi ofisi ziwe na technologia ya kukamata wanaojitolea kufichua ufisadi, limenishawishi kuamini niliyo yaandika.
 
Hiyo Ni Kitu Kinachotakiwa Kufanyiwa Kazi Popote Pale

Kama Wako Interested Wakitangaza Tenda Tunaweza Kwenda Kugombea Tena Na Kudeploy Hizi Programu Zakufanya Shuguli Hizi
 
Hiyo Ni Kitu Kinachotakiwa Kufanyiwa Kazi Popote Pale

Kama Wako Interested Wakitangaza Tenda Tunaweza Kwenda Kugombea Tena Na Kudeploy Hizi Programu Zakufanya Shuguli Hizi

sasa unakataa nini kwamba upo katika kundi la mafisadi? uumhh WAKUAJIRI UFANYE KAZI YA KUWAFICHA MAFISADI. pesa inatafutwa kwa namna nyingi.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom