Synthesizer
Platinum Member
- Feb 15, 2010
- 12,265
- 21,443
Ni changamoto ambayo Nyerere aliliweka mkakati wa kuimaliza kwa kila hali, na akafanikiwa kwa kiasi kikubwa. Tukajenga Tanzania isiyo na mabwana na watwana, kwa kuwa ilikuwa Tanzania yenye kutoa fursa sawa kwa watoto wote; shule tulisoma za aina moja, na hata JKT tukaenda pamoja, na vyuo kusoma vya aina moja bila kujali wewe ni mtoto wa kigogo au tajiri au masikini.
Alipoondoka Nyerere akaja Mwinyi, kisha Mkapa na hatimaye Kiwete, misingi ya Nyerere ya kuondoa Mabwana na Watwana ikaondolewa. Taratibu ikaanzishwa misingi iliyotofautisha watoto wa vigogo na matajiri toka wale wa masikini. Hata JKT kilichokuwa kiungo cha kuondoa tabaka nchini ikafutwa kwa visingizio mbalimbali. Zikaanzishwa shule ambazo ada zikawa hadi milioni 30 kwa mwaka, ili watoto masikini wasiguse huko, na wale wa wanaokwenda huko basi wakajenge urafiki na watoto wa raisi, mawaziri, magavana wa benki kuu, matajiri nchini, mabalozi wa nje nk. Na watoto wa matajiri na vigogo wakapelekwa huko hata kama walifaulu kwenda shule za serikali.
Ukawa umejengwa mfumo ambao watoto wa vigogo na matajiri wanapokua, wanazungukwa na watoto wa vigogo na matajiri wenzao - wanatengeneza na kuimarisha network ya Mabwana. Matokeo yake yakawa ukienda taasisi nyeti kama Benki Kuu, au Ofisi ya Raisi, Usalama waa Taifa nk, unakuta wanaoajiriwa wengi ndio hao waliosoma shule kama Feza nk, watoto wa vigogo na matajiri, na hata walifahamishwa kwa wazazi walipoalikwa kwenye birthday party nk, na ikawa rahisi wao kupewa kazi katika hizo taasisi na ofisi nyeti. Wapo wenye bahati kutoka kundi la Watwana, kama kina Tulia Ackson, na hata Raisi Magufuli mwenyewe. Lakini kwa ujumla watoto wa walalahoi wanaishia kupewa "makombo" ya ajira, au kukosa kabisa.
Na hata katika mfumo wa siasa imekuwa hivyo. Utakuta sasa tuna Waziri, Wakurugenzi, wakuu wa wilaya au mkoa aliteuliwa kwa sababu ni mtoto, ndugu au alisoma na kuwa rafiki na mtoto wa raisi, au Waziri Mkuu nk. Taratibu tunakuwa na wanasiasa ambao ni watoto wa vigogo na matajiri ambao walijenga network wakiwa chuo au shule pamoja, ndani na nje ya nchi.
Na sasa mfumo huu umeanza kukomaa na kuzidi kuzamisha mizizi, na ukweli ni kwamba uliletwa na awamu za uongozi za Mwinyi, Mkapa na Kikwete.
Kwa mara nyingine tena, Tanzania imeshakuwa nchi ya Mabwana na Watwana. Hivi unajijua uko wapi, na watoto wako watakuwa wapi? Swali ni kama Raisi Magufuli atauachia huu mfumo wa Mabwana na Watwana uendelee. Tunajua wazi yeye katoka kundi la Watwana, mtaji mzuri. Lakini ataweza, au it is too late!