Changamoto juu ya katiba mpya.

tufikiri

Senior Member
Nov 26, 2010
155
0
Kutokana na Wimbi kubwa lililopo kwa sasa la kudai Katiba mpya, ni rahisi kukutana na kijana anaunga mkono madai ya katiba mpya, lakini ukimuuliza kwani hii iliyopo ina Mapungufu gani? atakuambia hajui ila kasikia hata Viongozi wa Siasa,Asasi mbalimbali za Kijamii pamoja na Viongozi wa dini wakionge hususan baada ya Uchaguzi Mkuu wa 2010. Ukimpata kidogo anayefuatilia Siasa na Habari mbalimbali atakuambia tatizo liko kwenye Tume ya Taifa ya Uchaguzi.Na hata hiyo Tume si rahisi kwake kuilezea matatizo yake Kikatiba.Lakini ukweli ni kwamba yapo mapungufu mengi Katika Katiba iliyopo yakiwemo yale ya kumpa Rais Madaraka makubwa na kusapoti uongozi wa Kiimla, jambo ambalo Mihimili mingine kama Bunge imebakia kuishauri tu Serikari na sio kuiamrisha. Hata pale Bunge linapotoa Maazimio yake kwa Serikali na yakashindwa kutekeleza kwa kupuuzwa tu, bado Bunge halina Mamlaka ya kwenda zaidi ya hapo.Mfano mzuri ni Maazimio ya Bunge baada ya Richmond saga kutotekelezwa na Serikali. Hata, lile jukumu kubwa la Bunge baada ya kutunga Sheria, ambalo ni Oversight bado Bunge halipewi nafasi ya kulitekeleza kwa vitendo.Imekosekana ile dhana nzima ya check and Balance baina ya Mihili hii mitatu.
Wengi wa vijana, wengine wakiwemo humu kwenye JF wanaunga mkono Madai ya Katiba mpya lkn wengi wao hawajawahi hata kuisoma hiyo Katiba iliyopo na kujua mapungufu yaliyopo na hawa ni wale waliopata mwanga wa elimu, sasa sisemei wale walioko vijijini ambao hata hawawezi kujua hata cover la Katiba lina rangi gani?
Ushauri wangu ni kwamba, Kama kweli tunataka kuwa na Katiba Shirikishi na vyema kila mmoja kwa nafasi yake aweke jitihada katika kupata nakala ya Katiba kama hana ili ajiwekee utamaduni wa kuisoma mara kwa mara angalau aweze hata kubainisha kifungu kimoja ambacho anadhani kina mapungufu.
Wasiwasi wangu ni kwamba tunasubiri iundwe Tume ifanye kazi hiyo kwa niaba yetu na sio kuipa maoni yetu. Naamini wote tutatumia nafasi hii, badala ya kupoteza muda kwa kutukanana na kuitakana majina yasiofaa hapa jamvini.
Nawasilisha.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom