Changamoto juu ya chanjo iliyotokea miaka ya 1950s ndio inayojitokeza sasa, ila mwishoni utafika tu

SOPINTO

Senior Member
Oct 19, 2020
155
385
Nianze kwa kusema kuwa wenzetu ambao ni jirani zetu hapo kenya nao walianza kwa kusema kuwa chanjo ya Corona ni hiyari na sio lazima , lakini tamko lilitoka jana kutoka serikalini ni kwamba kila Mkenya ambaye ni mtumishi wa Umma lazima apate chanjo ndani ya wiki mbili zijazo na mwisho ni tarehe 24/8/2021 vinginevyo utajua kitakachokutokea. Hili tusema tu ni mwanzo kwa jirani zetu ila hapa nyumbani tutarajie makubwa zaidi , waswahili wanasema kuwa siku zote muda ndio mtoa majibu mzuri mwanafalsafa Bob Marley aliimba nyimbo moja inasema "Time will Tell".

Kuna kisa hiki cha miaka ya 1950 kulitokea ugonjwa mmoja unaoitwa Kimeta, ugonjwa huu uliua sana ng'ombe za wenyeji yaani watanganyika kutokana na sababu hiyo wakoloni wakaona kwa speed hii ya vifo vya ng'ombe basi itafika mahali tutakosa ha kitoweo , kutokana na hali hiyo wakoloni wakafanya study zao na kugundua kinga ya ugonjwa huo uliokuwa unaua sana ng'ombe hivyo wakafanya mikutano na Watanganyika kwa lengo kuwaelezea juu ya tatizo ikiwa pamoja na chanjo iliyopatikana ya kuzuia vifo vya ng'ombe.

Watanganyika baada ya mikutano kadhaa na wakoloni nao wakawa wanakusanyika kwa upande wao kupeana ujinga kuwa awa wazungu ndio chanzo cha vifo vya ng'ombe wetu hivyo basi hizi chanjo kamwe tusikubali, lakini kutokana na vifo kuendelea hali ikawa mbaya sana, katika juhudi wakoloni wakoloni walifanikiwa kuchanja baadhi ya ngo'mbe zilizokuwa karibu na makazi yao, matokeo ya chanjo yakawa mazuri sana na baada ya taarifa kuvuma juu ya chanjo hiyo na ng'ombe kupona basi wale watanganyika wakarudi kwa umoja wao na kukubaliana na maelekezo yalikuwa yanatolewa na wakoloni ikiwa na kuchimba mashimo kwa ajili ya kutengeneza majosho ya kuogeshea ng'ombe kila wilaya.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom