Changamoto jinsi ya kufika katika Hospitali ya Muhimbili~Mloganzila

zandrano

JF-Expert Member
Jan 24, 2017
7,120
7,703
Kwanza nianze kwa pongezi kwa Serikali kwa kujenga Hospitali ya Taifa kubwa na ya kisasa ya Muhimbili Mloganzila.
kwa wasiojua Hospitali hiyo ipo katika Wilaya ya Kisawe Mkoani Pwani lakini ili ufike katika Hospitali hiyo lazima upitie Barabara kuu ya Morogoro na kisha ufike Kibamba halafu utaingia Mloganzila.

Changamoto wanazozipata wananchi kutoka maeneo ya pembezoni kama vile Kisarawe, Chanika, Gongolamboto, Temeke n.k ni umbali, wagonjwa wengi kutoka maeneo mbalimbali ya Mkoa wa DSM wanapewa rufaa kwenda Hospitali ya Mloganzila lakini kutokana na miundombinu maalum kukosekana imekuwa changamoto kwa wanaofuata huduma.

Ushauri;
1. Serikali ijenge barabara shortcut inayotokea Kisarawe kupitia Makurunge na kutokea Kiluvya.

2. Serikali ijenge uwanja wa kutua ndege ndogo katika eneo hilo ili wagonjwa kutoa mataifa mengine waweze kufika kwa urahisi na kwa wakati, ikizingatiwa Hospitali hiyo inahudumia wagonjwa kutoka DRC, Burundi, Kenya, Uganda, Comoro n.k.

Hospitali ya Taifa Muhimbili Mloganzila ina eneo kubwa sana hivyo ina nafasi ya kutosha na kweli panafaa kwa wagonjwa.

Waziri wa Ujenzi angalia jinsi ya kutatua kero/changamoto hizo ili wananchi wapate urahisi kufika kwa wakati kupata huduma kwa wakati.
 
Correction Zanda

Kaka Muhimbili Mlogazila zamani MAMC ilishahama toka 2020 kutoka Kisarawe kwenda Wilaya ya Ubungo. Hivyo rekebisha hiyo Kisarawe kwenda Ubungo. Asante.
 
Ukipewa rufaa utafika tu maana kuna mwendokasi hadi hospital, kama unalalamika barabara ndege utaweza kumudu? Huko unapotoka chanika kuna ndege?
 
Back
Top Bottom