Keynez
JF-Expert Member
- Feb 12, 2007
- 2,397
- 3,884
Baadhi yetu kwa muda mrefu tumekuwa tunaongelea athari za kufanya mjadala wa athari za corona nchini kuwa ni mwiko.
Moja ya athari zake ni familia za kitanzania pamoja na taasisi mbalimbali kushindwa kujipanga (kutokana na kwamba hawana taarifa) kutokana na mabadiliko ya lazima yanayoendelea duniani kote.
Mjadala mpana ulihitajika badala ya kutegemea vichwa vichache na mambo kufanywa kwa usiri mkubwa. Naona kama tunaficha tu vitu ambavyo wakati ukifika vinaweza kuja kutuumbua.
Kila mwaka, watanzania wengi (mwenye takwimu anaweza kutusaidia) wanakwenda sehemu mbalimbali duniani kutafuta elimu.
Kutokana na janga la corona, binafsi ninaamini (na hili nimeliwaza muda mrefu kidogo), idadi hiyo wanaokwenda nje imelazimu kupungua saana, hasa kwa sababu ya woga na utashi wa wanafunzi wenyewe na wazazi wao.
Hii ina maana kuwa kutakuwa na shinikizo kubwa la mahitaji, hasa ya elimu ya juu kwa vyuo vyetu vya ndani kwa mwaka huu wa masomo 2020-2021 na inawezekana hata kwa mwakani.
Nimesikia vyuo kama UDSM, vimefanya usajili mkubwa sana awamu hii. Sina uhakika hali ikoje katika vyuo vingine.