Changamkieni Fursa za AJIRA Kiwanda cha sukari Turiani-Mtibwa May 2020

Neek

Member
Oct 1, 2019
68
79
Kiwanda cha sukari Mtibwa Turiani kinatangaza fursa za ajira ya ukataji miwa kwa watanzania wenye umri kuanzia miaka 20-35, sifa za mwombaji awe ni mtanzania, aweze kufika kiwandani kusajiriwa akiwa na vitu vifuatavyo paspot size nne, kitambulisho cha mpiga kura au cha taifa, aje na kadi ya ATM ya CRDB Bank kama anayo, kwa asiye nayo atasaidiwa kufungua account bank. Jinsi ya kufika Turiani Morogoro , panda basi hadi Msamvu stend Morogoro kisha tafuta gari za kwenda Turiani kutoka Msamvu.

Malipo ni Tsh 6,000/= KWA SIKU, Gharama zingine kama chakula, sehemu ya kulala na matibabu ni juu ya Kiwanda cha SUKARI NJOO TUUNGE MKONO JITIHADA ZA MH. RAIS KUIFANYA NCHI YETU YA VIWANDA.​
===​
1591606159400.png
 
Weka Tangazo katika kiwango cha Lami ndugu, maana direction haijaeleweka na Contacts pia hujaweka.
 
Hahahah vipi mapambano na wale chatu na nguruwe pori inakuwa juu ya kampuni au ndani ya mshahara?
 
Shida ya kampuni zinzoendeshwa na wabongo ndio hio hawathamini muda wa mtu na efforts, mtu yupo radhi akunyonye nusu ya kufa ila ujira nao akupunje kiasi kwamba utachakaza mwili bila mafanikio yeyote. Akupigishe slasher kuanzia saa 1 asubuhi mpaka saa12 jioni kisha akulipe elfu 6!

Angekuwa mzungu ungeshangaa hapo kila kibarua analipwa 40,000 kwa siku na makadirio ya muda hakutumii kwa zaidi ya masaa 8. Wanathamini sana muda wa wenzao na nguvu. Ila unaweza bado kuta kuna takataka nyeusi kwenye bodi itaingilia kati kwa siri na kucheza dili watu walipwe 20,000 kinyume na budget ili wapige hela kwa migongo ya wenzao.
 
Back
Top Bottom