Changamkia fursa hapa:Takwimu za kushangaza za ongezeko la watu Tanzania.

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
42,875
49,554
Nawasalimu kwa salamu ya kihandisi, expansion joint wadau!
Kama kichwa cha habari kinavyosomeka,Nchi yetu ya Tanzania kwa sasa ni kati ya nchi zenye idadi kubwa ya watu na yenye ongezeko la kasi la watu barani Africa.Kwa mujibu wa idara ya worldometer ya UN,hadi kufikia 20/12/2017 Tzn ilikadiriwa kuwa na watu 58,136,713,,sawa na ongezeko la 3.1%(1,700,000) kwa mwaka na kufanya Tzn kuwa nchi ya 5 yenye idadi kubwa ya watu ikiipita South Africa,huku ikitanguliwa na Nigeria,Ethiopia,Egypt na DRC Congo.
Kati ya hao 32% wanaishi mijini,hivyo basi inakadiriwa kuwa ifikapo 2025 ,Tzn itakuwa na watu zaidi ya mil.72.Hili ni soko kubwa sana kwa sasa na baadae hasa mazao ya kilimo na nyumba za makaazi.Tukijumuisha na EAC soko hili lina jumla ya watu zaidi ya mil.185.5 hapo sijaihusisha Ethiopia,Egypt,Sudan na Somalia.
So bandugu tukae mkao wa kuchangamkia fursa za biashara na uwekezaji.
Taarifa hizi sio rasmi,hazijathibitishwa na idara ya takwimu ya taifa.
Nawasilisha.
 
Back
Top Bottom