BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,790
- 288,099
Jamaa wameshacheza na documents na sasa wanazungumza hadharani. Walikuwa wapi miezi yote hii kutwambia hili hadi leo? Fisadi Mkapa alishindwa kulizungumza hili mwenyewe pale tu lilipoanikwa hadharami miezi yote hii? Ni kipi kilichomfanya ashindwe kutwambia hili miezi yote hii? Ndio matatizo ya kutozifuatilia tuhuma nzito labda walifanya hivyo makusudi ili wampe jamaa muda wa kufanya vitu vyake ili kupoteza ushahidi!!! Duh!!
Kiwira yamsafisha Mkapa
Mwandishi Wetu
Daily News; Sunday,June 01, 2008 @19:01
Uongozi wa Kampuni ya Kiwira Coal and Power Ltd (KCP) inayomiliki mgodi wa Kiwira, umekanusha madai kuwa Rais mstaafu Benjamin Mkapa na mkewe Anna ni miongoni mwa wamiliki wa mgodi huo.
Badala yake, mgodi huo umesema Kampuni ya ANBEN inayomilikiwa na Mkapa na mkewe, ambayo awali ilikuwa sehemu ya Kampuni ya Tanpower, ilijitoa baada ya baadhi ya wanahisa wenzake kuwa na mpango wa kununua mgodi huo.
Mtendaji Mkuu wa KCP, Francis Tabaro, alisema ingawa katika hati za umiliki (Articles of Association) inaonyesha kuwa Mkapa ni sehemu ya Tanpower, lakini baadaye alijitoa.
"Ni kweli ANBEN ilikuwa sehemu ya Tanpower lakini baada ya wazo la kununua Kiwira kuingizwa na wadau wenzake, yeye aligoma akaona aitoe kampuni yake katika Tanpower," alisema Tabaro.
Tabaro pia alikanusha madai kuwa Anna Mkapa aliwahi kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Kiwira na akaeleza kuwa madai hayo hayana ukweli wowote, kwani kampuni hiyo haihusiani na kiongozi huyo.
Tabaro aliwataja wakurugenzi wa KCP kuwa ni Joseph Mbuna ambaye ni Mwenyekiti, Mafuru M. Mafuru, Wilfred Malkia na Evans Mapundi wakati serikali yenye hisa 15 katika mgodi huo inawakilishwa na Omari Chambo ambaye kwa sasa ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Miundombinu na Katibu Tawala wa Mkoa wa Mbeya, Asumpta Ndimbo.
Tabaro alisema upotoshaji unaofanywa na vyombo vya habari kuwa Rais mstaafu Mkapa ni sehemu ya wamiliki wa mgodi huo, hazina ukweli, bali zinalenga kuharibu jina la kampuni ambayo imechukua hatua ya kuendesha mgodi huo.
"Mkapa, mkewe au familia yake si sehemu ya wamiliki wa mgodi huu," alisisitiza huku akionyesha kukerwa na namna alivyodai kuna upotoshaji wa makusudi unaofanywa na vyombo vya habari.
Alisema lengo la kuripoti habari hizo ni kutaka serikali iwe na mtazamo hasi juu ya mgodi huo, hali ambayo inaweza kuzorotesha uzalishaji wa makaa ya mawe. Tabaro pia alisema kitendo cha baadhi ya maofisa wa serikali kutoa maelezo kuwa mgodi huo unachunguzwa kuhusiana na madai kuwa ulichukuliwa isivyo halali na Kampuni ya KCP, kunaweza kukaifanya kampuni hiyo kushindwa kupata fedha za kuendesha mradi huo.
Alisema kampuni yao ina mpango wa kupata fedha kutoka taasisi za benki hivyo mtazamo hasi kutoka kwa maofisa wa serikali utaathiri namna ya upatikanaji wa fedha hizo na wakati mwingine taasisi hizo zinaweza kutoa mkopo kwa masharti magumu kutokana na wasiwasi wa kisiasa.
"Cha kushangaza ni kwamba serikali iko kimya kuhusiana na madai hayo, hali ambayo haionyeshi kutatua tatizo hilo," alisema Tabaro. Akieleza tuhuma za kununua mgodi huo kwa Sh milioni 700 wakati mgodi umejengwa kwa Sh bilioni nne, Tabaro alisema wakati kampuni inanunua mgodi huo ulikuwa chakavu na mashine zake zilikuwa hazifai kuendeleza uzalishaji.
Alisema ndiyo maana KCP imeamua kutumia Sh bilioni 48 kwa ajili ya kuweka mitambo ili angalau mgodi huo uweze kuwa na uwezo wa kuzalisha tani 300,000 kwa mwaka. Wakati KCP inatoa utetezi huo, hivi karibuni Mbunge wa Vunjo, Aloyce Kimaro (CCM), alidai bungeni kuwa mgodi huo ambao ulijengwa na serikali kwa Sh bilioni nne umeuzwa kwa Mkapa na aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Daniel Yona.
Hata hivyo, Tabaro alisema Waziri huyo wa zamani Yona pia si mmoja wa wamiliki wa mgodi huo kama ambavyo inaripotiwa katika vyombo vya habari. Wiki iliyopita, Rais Mstaafu Mkapa akiwa nyumbani kwake Kijiji cha Lupaso wilayani Masasi Mkoa wa Mtwara, alisema tuhuma zote za ufisadi zinazoelekezwa kwake ni za uongo na zinaenezwa na watu ambao walitegemea kupata upendeleo wakati wa utawala wake, lakini hawakupata.
Mkapa ambaye enzi za utawala wake alijulikana kwa falsafa yake ya Uwazi na Ukweli, pia alisema yeye si tajiri, bali anaishi kwa pensheni ya serikali kama mstaafu kama walivyo viongozi wengine.