Changa la macho: Wallace Karia na Michael Wambura “sielewi-elewi”

Jeff Gemo

Member
Jul 11, 2015
34
26
k9rrNRuH.jpg

Mara nyingi imekuwa ikihubiriwa kwamba Rais mpya wa TFF Ndg. Wallace Karia ni mtu safi na asiye na makandokando, hata mimi binafsi kuna wakati niliamini hivyo na kuona sasa tumepata kiongozi shupavu na mpira wetu utabadilika.

Habari mbaya kabisa kwa wanamichezo ni kwamba, Wallace Karia anaweza kuwa ni mpigaji wa chini chini na ndio maana yuko “very comfortable” na makamu wake Ndg. Michael Wambura, na si ajabu kwamba mipango yote ya “kutafuna” pesa za TFF sasa wanaipanga pamoja.

Ninasema haya kwasababu Karia anajua undani wa ripoti ya Kampuni ya ukaguzi wa mahesabu TAC (Tanzania Audit Corporation) iliyotolewa Januari 19 mwaka jana baada ya ukaguzi wa kina juu ya matumizi ya mabilioni ya shilingi katika shirikisho hilo. Ripoti ile ilieleza mambo mengi sana na kuwataja watu wengi sana akiwemo aliyekuwa katibu mkuu wa FAT Ndg. Michael Wambura (ambaye sasa ni makamu wa Rais TFF).

Ripoti hiyo ya ukaguzi pamoja na mambo mengine ilitaja kuwa katika kipindi cha kuanzia August 15, 2014 hadi September 30 2015, TFF ilifanya malipo ya jumla ya shilingi milioni 274.072 kwa Ndg. Michael Wambura na kampuni za Punchlines (T) Ltd na Artriums Dar Hotel, katika mchanganuo wa fedha hizo, Wambura alilipwa kiasi cha shilingi milioni 67.5 malipo haya yalifanyika bila kuwa na nyaraka stahiki na Wallace Karia anajua vizuri.

Malipo hayo yote yalifanyika bila kamati tendaji ya TFF kuwa na taarifa, na wala hayakuwa katika bajeti ya TFF, hapakuwa na risiti wala uthibitisho wa waliolipwa.. yaani kiufupi ilikuwa ni magumashi, na ilipelekea baadhi ya shughuli muhimu za taasisi kukwama kabisa.

TAC katika ripoti yao wakaenda mbali zaidi kwa kusema kwamba Ndg. Wambura alilipwa pesa hizo kimakosa kwani alikuwa anaidai TFF pesa zisizozidi milioni 50, malipo yale yalifanyika kutokana na mkopo wa USD 3000 ilioupata FAT kutoka Jack System Limited. Na Wambura hakurudisha fedha zile, Wallace Karia anajua vizuri sana kuliko mimi.

Sasa hiyo tisa, kumi ni kwamba katika wadaiwa sugu 18 wa shirikisho la Mpira wa miguu TFF, yumo pia Ndg. Michael Richard Wambura anayedaiwa jumla ya shilingi milioni 50.828 ambayo sina hakika kama amelipa hata “Jero” ila alishindiliwa mipesa zaidi na hakuna aliyehoji.

Kipindi chote hiki Rais wa TFF wa sasa Ndg. Wallace alikuwa ni makamu wa Rais wa TFF chini ya “Injiania” Jamal E. Malinzi, kwahiyo haya sio mageni kwake ila kayakalia kimya pengine ni ule utaratibu wa 10%.

Ikiwa kweli TFF wameamua kuwa na nia ya dhati ya kuisafisha taasisi hii, kwanza tunaomba Wambura arejeshe fedha anazodaiwa na alizopokea kinyume cha taratibu, tutangaziwe na ikiwezekana watuombe msamaha kwa kutukosea namna hiyo.

Hatuwezi kuwa na imani na Rais mpya ambae anaufahamu mfumo mbovu uliopita akiwa makamu, na anashindwa kushughulikia ipasavyo ripoti iliyotelewa na TAC ambao kimsingi walipewa kazi hiyo na mkutano mkuu wa wanachama wa TFF.

Ifike wakati tuweni “serious” kidogo na masuala haya, huu mzizi wa ufisadi ni lazima ukatwe kwa gharama yeyote hata kama itakuwa ni kubwa lakini ni bora tuilipe mara moja na ipite tuanze upya. Sina shaka na uhalali wa viongozi hawa ila shida yangu ni uadilifu wao, tunaweza kuwa tupo mahala pabovu kabisa kuliko tulipotoka kama “sarakasi” hizi zitaendelea kuburudisha wenye mamlaka.

Jeff Gemo Mnyama Machine
The One Man Army
Affirmative Gemo The Great
Coming Back Strong than Ever!!

[HASHTAG]#SeriesFreeLife[/HASHTAG]
Season Three | Episode Zero
 
Mkuu Karia hachagui makamu wa rais bali rais na makamu wa rais huchaguliwa na wajumbe ,

Sasa kama wambura ana mauchafu sio kosa la Karia kwasababu Karia hana mamlaka ya kumchagua au kumuengua makamu

Mpaka hapo point yako imefeli

Pili Karia alivyokuwa enzi na malinzi walikuwa hawapatani na hata kuongea walikuwa hawaongei kwa tajriban miezi kibao licha walikuwa ofisi moja

Jiulize kwanini malinzi na katibu mkuu wa tff wapo segerea na Karia aliyekuwa makamu yupo saafi na kawa rais ?

Na uozo wote ni Karia aliowastua takukuru

So bado sijaona hoja ya msingi ya kuonyesha ubovu wa karia
 
Kama nimemwelewa mtoa mada, sasa ni wakati wa Karia kuhakikisha kwamba Wambura analipa deni lililotajwa na mtoa mada. Kushindwa kufanya hivyo, kwa maoni ya mtoa mada, kutathibitisha kwamba na Karia alihusika na kadhia anayoisema mtoa mada. Unasemaje kwa hilo?
 
View attachment 619440

Mara nyingi imekuwa ikihubiriwa kwamba Rais mpya wa TFF Ndg. Wallace Karia ni mtu safi na asiye na makandokando, hata mimi binafsi kuna wakati niliamini hivyo na kuona sasa tumepata kiongozi shupavu na mpira wetu utabadilika.

Habari mbaya kabisa kwa wanamichezo ni kwamba, Wallace Karia anaweza kuwa ni mpigaji wa chini chini na ndio maana yuko “very comfortable” na makamu wake Ndg. Michael Wambura, na si ajabu kwamba mipango yote ya “kutafuna” pesa za TFF sasa wanaipanga pamoja.

Ninasema haya kwasababu Karia anajua undani wa ripoti ya Kampuni ya ukaguzi wa mahesabu TAC (Tanzania Audit Corporation) iliyotolewa Januari 19 mwaka jana baada ya ukaguzi wa kina juu ya matumizi ya mabilioni ya shilingi katika shirikisho hilo. Ripoti ile ilieleza mambo mengi sana na kuwataja watu wengi sana akiwemo aliyekuwa katibu mkuu wa FAT Ndg. Michael Wambura (ambaye sasa ni makamu wa Rais TFF).

Ripoti hiyo ya ukaguzi pamoja na mambo mengine ilitaja kuwa katika kipindi cha kuanzia August 15, 2014 hadi September 30 2015, TFF ilifanya malipo ya jumla ya shilingi milioni 274.072 kwa Ndg. Michael Wambura na kampuni za Punchlines (T) Ltd na Artriums Dar Hotel, katika mchanganuo wa fedha hizo, Wambura alilipwa kiasi cha shilingi milioni 67.5 malipo haya yalifanyika bila kuwa na nyaraka stahiki na Wallace Karia anajua vizuri.

Malipo hayo yote yalifanyika bila kamati tendaji ya TFF kuwa na taarifa, na wala hayakuwa katika bajeti ya TFF, hapakuwa na risiti wala uthibitisho wa waliolipwa.. yaani kiufupi ilikuwa ni magumashi, na ilipelekea baadhi ya shughuli muhimu za taasisi kukwama kabisa.

TAC katika ripoti yao wakaenda mbali zaidi kwa kusema kwamba Ndg. Wambura alilipwa pesa hizo kimakosa kwani alikuwa anaidai TFF pesa zisizozidi milioni 50, malipo yale yalifanyika kutokana na mkopo wa USD 3000 ilioupata FAT kutoka Jack System Limited. Na Wambura hakurudisha fedha zile, Wallace Karia anajua vizuri sana kuliko mimi.

Sasa hiyo tisa, kumi ni kwamba katika wadaiwa sugu 18 wa shirikisho la Mpira wa miguu TFF, yumo pia Ndg. Michael Richard Wambura anayedaiwa jumla ya shilingi milioni 50.828 ambayo sina hakika kama amelipa hata “Jero” ila alishindiliwa mipesa zaidi na hakuna aliyehoji.

Kipindi chote hiki Rais wa TFF wa sasa Ndg. Wallace alikuwa ni makamu wa Rais wa TFF chini ya “Injiania” Jamal E. Malinzi, kwahiyo haya sio mageni kwake ila kayakalia kimya pengine ni ule utaratibu wa 10%.

Ikiwa kweli TFF wameamua kuwa na nia ya dhati ya kuisafisha taasisi hii, kwanza tunaomba Wambura arejeshe fedha anazodaiwa na alizopokea kinyume cha taratibu, tutangaziwe na ikiwezekana watuombe msamaha kwa kutukosea namna hiyo.

Hatuwezi kuwa na imani na Rais mpya ambae anaufahamu mfumo mbovu uliopita akiwa makamu, na anashindwa kushughulikia ipasavyo ripoti iliyotelewa na TAC ambao kimsingi walipewa kazi hiyo na mkutano mkuu wa wanachama wa TFF.

Ifike wakati tuweni “serious” kidogo na masuala haya, huu mzizi wa ufisadi ni lazima ukatwe kwa gharama yeyote hata kama itakuwa ni kubwa lakini ni bora tuilipe mara moja na ipite tuanze upya. Sina shaka na uhalali wa viongozi hawa ila shida yangu ni uadilifu wao, tunaweza kuwa tupo mahala pabovu kabisa kuliko tulipotoka kama “sarakasi” hizi zitaendelea kuburudisha wenye mamlaka.

Jeff Gemo Mnyama Machine
The One Man Army
Affirmative Gemo The Great
Coming Back Strong than Ever!!

[HASHTAG]#SeriesFreeLife[/HASHTAG]
Season Three | Episode Zero
Mami yake weee Mzee umerudi khaaaa
 
Back
Top Bottom