Chanel yasitisha kuuza bidhaa zake kwa watu wanaozinunua na kupeleka Urusi ikiwa ni baada ya kufunga maduka yake nchini humo

Lady Whistledown

JF-Expert Member
Aug 2, 2021
1,017
1,606
Kampuni kubwa ya kifahari ya Chanel ya Ufaransa imeacha kuuza bidhaa zake kwa watu wanaonunua na kuzipeleka Urusi, baada ya kufunga maduka yake nchini humo.

Moscow na baadhi ya wateja wameishutumu kampuni hiyo kwa kupinga Urusi, na kutishia kususia chapa hiyo.

Chanel inasema inazingatia tu vikwazo vya Umoja wa Ulaya (EU), ambavyo vinapiga marufuku kuiuzia Urusi bidhaa za anasa za bei ya zaidi ya €300 ($327; £250).

Makampuni mengi ya Magharibi yalisimamisha shughuli nchini Urusi baada ya vita vya Ukraine kuanza.

Chanel aliambia BBC kwamba vikwazo vilivyowekwa na EU, pamoja na Uswizi, pia vinapiga marufuku uuzaji wa vitu vya anasa kwa watu binafsi wanaonuia kuvitumia nchini Urusi.

Kampuni hiyo ilisema "inatii sheria zote zinazotumika kwa shughuli zetu na wafanyikazi ulimwenguni kote, pamoja na sheria za vikwazo vya biashara".

"Hii ndiyo sababu tumeanzisha mchakato wa kuwataka wateja ambao hatujui makazi yao kuu kuthibitisha kuwa bidhaa wanazonunua hazitatumika nchini Urusi," Chanel ilisema katika taarifa yake.

"Kwa sasa tunashughulikia kuboresha mbinu hii na tunaomba radhi kwa usumbufu utakao jitokeza," kampuni hiyo iliongeza.
 
Dawa ni kumchangia Putin wampe kibano and nchi ya russia ilipishwe gharama zote walizozifanya ikiwemo kodi ambazo Ukraine imepoteza kama uvamizi usingetokea... issue za vikwazo ndio zinampa kiburi Putin sababu anaishi kifahari na raia wake kawadhibiti mno
 
Sio zimbabwe hio
 
Netherlands :
Prime Minister Mark Rutte said: “We are facing an incredibly high inflation rate of 11%.

Prices are rising so fast that the government can't fix it."

HAHAHAHA
 
Waongo! Wanauza bidhaa zao urusi wanachofanya nikuondoa tu nembo/brand zao kwenye bidhaa wanazoziuza urusi
 
Dawa ni kumchangia Putin wampe kibano and nchi ya russia ilipishwe gharama zote walizozifanya ikiwemo kodi ambazo Ukraine imepoteza kama uvamizi usingetokea... issue za vikwazo ndio zinampa kiburi Putin sababu anaishi kifahari na raia wake kawadhibiti mno
Hilo litawezekana tu kama utaacha kupumuliwa kisogoni
 
Back
Top Bottom