CHAN2021: Mchezo umemalizika kwa Taifa Stars kupoteza mchezo wake wa kwanza dhidi ya Zambia

Mnavyolalamika humu ndan as if hii Taiga stars ni boooonge moja LA timu, mbona miaka yote huwa ni hivi hivi tu? Kiufupi tz hatuna wachezaji wazawa wa kushindana na timu za nje hata hii ligi yetu inabebwa na hao ma pro wa nje
 
Taifa stars imeanza vibaya huko Cameroon dhidi ya Zambia kwa kulala 2-0.
Nadhani rais atatekeleza ahadi Yake ya kutumbua waziri wa michezo ingawa hakucheza....
Hawa TFF wana jambo na huyu Mrundi.

Jana ikisikiliza kipindi cha michezo asubuhi cha E Fm, walisema timu imeishacheza mechi 10 na ni mechi mbili tu ilizoshinda tena ndani dakika 90.

Pana nini hapo?
 
Kutumbua makocha kila siku hakujazifanya simba au Yanga kuwa timu bora kama TP Maembe au AS Vita. Hivyo ni muhimu jiwe aelewe kwamba kutumbua tumbua watendaji wake ni mbwembwe tu na haiongezi ufanisi wa serikali
TP Malimao
 
Ndiyo uwezo wao ulipoishia,
Wenzenu wanawekeza kwenye mpira,nyie mmekalia siasa
Mpira wa Tanzania unachezwa kwenye vyombo vya habari.
Na siasa yenyewe bado tunategemea nec, polisi, wakurugenzi na wengineo kutuamulia.
 
Mkuu kauli za wanasiasa na masilahi binafsi ya viongozi wa mpira wa miguu hapa nchini ndio sababu kubwa ya hii team kufanya vibaya.
Kocha anataka kuwaridhisha wana siasa na baadhi ya watu kwa maslahi ya wachezaji wao kwa kutumia kivuli cha kukuza vipaji vipya.

Ukweli ni kwamba sisi Chan mwaka huu hatujapeleka team ya ushindani bali tumepeleka team ya majaribio kwenda kukuza vipaji na matokeo yake ndio haya tunayaona sasa na nakubaliana na wewe kuwa hatutapata hata pont 1 kwenye haya mashindano kamwe.

Huwezi kuacha wacheji wazoefu wote nyumbani na hata hao wachache ulio wachukua bado unawaweka bench kwa makusudi kabisa mfano mabao yote mawili makosa yalianzia katikati pale kwa baraka Majogoro Kisha cross ikapigwa pembeni kushoto kule kwa Manyama inakuja kwenye box Kapombe anajitahidi kuokoa hadi ananawa mpira, Goli la pili napo vile vile ni kule kule kushoto mtu kapiga cross jamaa anaunganisha mpira kambani.

Katikati pamekufa kabisaa ajabu Ndemla yuko bench pale hapewi nafasi, viungo wa Kati wazuri kabisa Kama Mzamiru, Sure boy, Frank Domayo na Mkude wameachwa kwa makusudi kabisa.

Kule mbele ndio kabisaa, yani unamuweka bench Faridi Musa alafu unamuanzisha Mhiru ambae hata ball control nzuri hana, Kama haitoshi tumewaacha mawinga wazuri kabisa huku Nyumbani Kama Iddi Nado na Hassani Dillunga kisa tunataka kukuza vipaji!!!

Nchimbi unamuweka mbele na Lyanga heti ndio wawe wafungaji huku huyu nchimbi hata tu kwenye team yaka hapati nafasi ya kucheza anakaa bench tangu msimu wa ligi imeanza hajafunga goli hata moja alafu eti ndio tunategemea akatupe matokeo CHAN.

Wacha tu tufungwe sababu tupo kwenye majaribio ya kikosi na si kushindana.
Nadhani first half tulifanya vizuri kidogo na hats eneo LA kiungo hatukuwa wabaya sana, mtizamo wangu ni kwamba

1. Kocha alichowaambia wachezaji wakati wa Half time kinaweza kuwa sababu kipigo. Yamkini kama aliwaambia "Hawa tunawamudu" hivyo kuwafanya wachezaji wawe na attacking mind na hivyo kutengeneza mwanya kati ya Beki na midfields & Attacker ambao ulitumia vyema na Zambia

2. Mbinu za Kocha wa Zambia za kuongea viungo ( midfields) zilitufanya tupoteane na kuwafanya Backline kuwa katika Pressure toka kwa Wazambia muda mwingi.

3. Concentration ya timu nzima labda ukiondoa Goal keeper na backline ilipotea kipindi cha pili, zile interception za first half zilipotea kabisa. Yamkini fitness ya wachezaji wetu nayo ni yakutilia shaka.

4. Nadhani tunaweza kufanya maboresho ILA maoni yangu ni kwamba tungepeleker timu ya vijana under 20 wakapate uzoefu na pia kuwawezesha kuonekana na mawakala.

Ahsante
 
Back
Top Bottom