Chan. Ten:Inastahili Pongezi kwa "Freedom of Expression, Watangaza Vipaji,Mahiri na Shupavu" -But..! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chan. Ten:Inastahili Pongezi kwa "Freedom of Expression, Watangaza Vipaji,Mahiri na Shupavu" -But..!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Pascal Mayalla, Sep 8, 2012.

 1. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #1
  Sep 8, 2012
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,548
  Likes Received: 18,216
  Trophy Points: 280
  Wanabodi,

  Wakati tukiendelea kuugulia msiba wa Mwanahabari Daudi Mwangosi, kitendo cha kupigwa na polisi hadi kudondoka chini na kamera yake mkononi bila kuiachia, akamkumbatia ofisa huyo wa polisi ili kujisalimisha na kuisalimisha roho yake, akingali na kamera yake mkononi na hakuiachia mpaka kifo kilipomkuta..., ni kitendo cha ushupavu na ushujaa wa hali ya juu kwenye tasnia ya habari!. Huyu anastahili kuitwa Shujaa wa Taifa, na damu yake haitapotea bure, itakuwa ni chemchem ya ukombozi wa wanahabari kwa ujumla dhidi ya madhila mbalimbali yayowakumba na labda pia hii ndio cheche ya moto nyikani, itakayo lipua moto wa mabadiliko nchi nzima na kufikisha sio tuu mwisho wa udhalimu wa jeshi letu la polisi kupitisha hukumu ya kifo instantly without trial dhidi ya raia wasio na hatia yoyote, bali pia unaweza kuwa ndio mwanzo wa mwisho wa serikali dhalimu ambayo polisi hao dhalimu, ni sehemu ya serikali hiyo na ndio maana inawalinda polisi dhalimu hao, kwa udhalimu wao!.
  [​IMG]

  Niikiangalia picha hii ya mwisho ya mpiganaji kamanda Mwangosi, imenifanya nikitafakari kituo cha televisheni cha Channel Ten na baadhi ya wanahabari wake mahiri, shupavu na vitendo vyao vya kishujaa, lakini...

  Kuwakumbusha tuu, Channel Ten wakati huo ikiitwa DTV,
  1. Ndio iliyokuwa TV ya kwanza kuweka msomaji wa habari zaidi ya mmoja mwaka 1994, zingine zikafuatia.
  2. Ndio ilikuwa TV ya kwanza kurusha matangazo yoyote ya televisheni ya moja kwa moja "live" 1995 na ndiyo ya kwanza kurusha habari "live" vituo vingine vikirekodi kwanza ndipo virushe!.
  3. Ndiyo ilikuwa TV ya kwanza kufanya vipindi vya mahojiano ya papo kwa papo "Vox Pop" na kipindi cha kwanza cha mahojiano ya "Vox Pop" kiliitwa "Mada Moto" Uchaguzi wa 1995!.
  4. Ndiyo ilikuwa TV ya kwanza kutangaza uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi live, na kutangaza jumla ya matokeo ya ukweli ya uchaguzi wa Zanzibar ambapo kiukweli CUF walishinda, ila ZEC ikaitangaza CCM ndio washindi!.
  5. Ndio TV ya kwanza kupigwa fine na NEC kwa kuutangaza ukweli halisi wa matokeo ya urais kituo kwa kituo na kupelekea sheria ya uchaguzi kubadishwa kuwa sasa ni marufuku kwa chombo chochote kuyatangaza jumla ya matokeo ya kura za urais toka kituo kwa kituo bali ni matokeo yaliyopikwa na NEC tuu ndio matokeo halali ya uchaguzi wa rais!.
  6. Kufuatia ugomvi fulani wa kibiashara, Mmiliki wa Channel Ten aliweka "detention" without trial kwa kusingiziwa ametaka kumuua mmiliki wa kituo kingine cha TV. Katibu Mkuu wa Mambo ya Ndani, akaamuru atolewe, pale pale katibu mkuu huyo alimwaga unga wake!.
  7. Ndicho kituo cha kwanza kuanzisha TV Talk Show iitwayo "Kiti Moto" ambayo baadae ilikuja ...
  8. Ndio TV ya kwanza kutangazo michuano ya kombe la dunia na kutangaza mbio za magari za langa langa (F1 grand prix) bure!, hata ulaya, huwezi kuona world cup au grand prix bure!
  9. Ndio TV inayoongoza kwa habari za ukweli na msisimko, vipindi vinavyoongoza kwa freedom of expression na msisimko zaidi kuliko vituo vingine vyote..lakini..
  10. Ndicho kituo kinachoongoza kwa kupika vipaji vya utangazaji wa Televisheni nchini, watangazaji wengi wa vituo vingine vingi, wamepikwa na Channel Ten, wengine kazi zao ni kuwasubiri, wakishaiva, kupakua tuu na kuyafaidi matunda yao!. Kwa haya yote, Channel Ten inastahili pongezi za dhati, lakini..

  Kabla sijamalizia ile lakini yangu, sio vibaya nikiwataja baadhi ya watangazaji mahiri na shupavu wa Chanel Ten na vitendo vyao vya Umahiri, Ushupavu au Ushujaa.

  1. Betty Mkwasa ambaye kwa sasa ni mkuu wa wilaya ya Bahi, alipikwa na Channel Ten, alipohamia ITV, akashinda Tuzo ya CNN Journalist of a Year, baadae akaukwaa u-DC!.
  2. Ahmed Kipozi, alipikwa na Channel Ten, huyu ndiye mtangazaji wa TV wa kiume aliyeongoza kwa kuwa smart na ana sauti yenye lafudhi tamu ya ajabu!. Baadae alihamia ITV na mwishowe sauti yake kutumiwa na kurugenzi ya mawasiliano Ikulu kwenye vipindi vya JK. Kwa sasa ni Mhe. DC wa Bagamoyo.
  3. Bujaga Izengo Kadago, alipikwa na Channel Ten, akahamia Morogoro kwenda kuanzisha SUA TV.
  4. Karim Besta, (RIP) alipikwa na Channel Ten na kuhamia Morogoro kwenda kuanzisha Aboud Television.
  5. Ephraim Kibonde, alipikwa na Channel Ten, na kuhamia Clouds sasa ni mtangazaji mahiri wa Radio na TV
  6. Salim Kikeke, alipikwa na Channel Ten akahamia ITV sasa ni mtangazaji kiongozi BBC Swahili.
  7. Sunday Shomari, alipikwa Channel Ten akahamia ITV sasa ni Mtangazaji kiongozi VOA
  8. Florah Nducha, alipikwa Channel Ten, akahamia Radio One, sasa ni Mkuu wa Idhaa ya Kiswahili ya UN Radio yuko NY.
  9. Sakina Datoo, alipikwa Channel Ten, akaenda Sunday Citizen, then Guardian on Sunday, sasa yuko Daily Telegraph ya UK.
  10. Yule mtangazaji wa kile kipindi cha Kiti Moto alipikwa Channel Ten, akahamia TBC, kwa sasa ni mtangazaji wa kujitegemea akimiliki kampuni yake ya matangazo kwa jina la PPR.

  Nimeziainisha baadhi ya sifa za kituo cha Televisheni Channel Ten na baadhi tuu ya watangazaji waliopitia kwenye mikono hiyo, sijawataja wale wote waliopo vikiwemo vichwa kama Jenerali Ulimwengu, Makwaia wa Kuhenga, Hamza Kasongo etc, sifa hizi zote na nyinginezo nyingi, zinakifanya kituo cha Televisheni cha Channel Ten, kustahili pongezi za dhati kwa mafanikio yote hayo!.

  Ila kama kawaida, kile kwenye mafanikio, hapakosi changamoto, na hizo ndizo msingi mkuu wa mada yangu.
  Ukiangalia safu ya vipaji vilivyo timka ni dhahiri Channel Ten kuna matatizo fulani.. na baada ya kusikia kumbe hata Marehemu Daudi Mwangosi, hakuwa mwajiriwa wa Channel Ten, he was only a correspondent!, huu ni uthibitisho wa tatizo, somewhere, some how!.

  Nauomba uongozi wa Channel Ten, ufanye utaratibu mpya kabisa wa kumuenzi Daudi Mwangosi kwa kutoa "special employment" kwa "marehemu" in terms of paperwork ili kuandaa taratibu zote za mafao tangu alipojiunga nao in terms of payment ili familia yake ipate chochote kutoka Channel Ten, hata ikibidi, wamuanzishie "Daudi Mwangosi Memorial Fund" na itachangiwa na sisi wadau ili kuilinda familia yake isiadhirike na badala yake, ipate ustawi wa jasho la baba yao!.

  Kiendo cha kuwa Daudi Mwangosi, hakuwa mwajiriwa rasmi wa Channel Ten, hakuiondolei Channel Ten, "full tortious liability" in an event of death!. Watanzania wengi hawajua kuwa kila mwenye chombo cha usafiri, ana liability na abiria wake in case of accident or death ndio maana bima ni muhimu!. Vivyo hivyo media zote, zina liability na waandishi wao in case of death, awe ni muajiriwa au sio muajiriwa as long as alikuwa anafanya kazi ya Channel Ten, then Channel Ten lazima ibebe resiponsiblities as if alikuwa full time employee!.

  Namalizia kwa kuipa tena Channel Ten pole nyingi za msiba, hongera nyingi za kuwa vinara wa "freedom of Expression" na hongera nyingi kwa upishi wa watangazaji vipaji, mahiri na shupavu lakini ...waipokee changamoto hii...lazima mbadilike, "you have to motivate and retain the best that you have na kuanza kwa kumuenzi shujaa wetu "Daudi Mwangosi" kwa all his rights, he should have had long ago when he was alive!.

  Wasalaam.

  Pasco.
   
 2. Lokissa

  Lokissa JF-Expert Member

  #2
  Sep 8, 2012
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 7,079
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  NO. ten si wewe mwenyewe kaka
  nakukumbuka sana miaka ya 1990's
  kweli wanastahili hongera kubwa
  washauri nao pia watumie U-streem ili nasi wa madongo kuinama tuweze kuwapata online
  kama star tv walivojitahidi,habari hii wafikishie pia ITV.
  nimependa sana ujasiri wa Channel ten wanajitahidi kutopendelea upande wowote
   
 3. bornagain

  bornagain JF-Expert Member

  #3
  Sep 8, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 3,389
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  Sasa wako namba ngapi sasa, issue is now how you begin but how you finished your marathon
   
 4. BIG X

  BIG X JF-Expert Member

  #4
  Sep 8, 2012
  Joined: Nov 4, 2011
  Messages: 777
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Hivi vyombo vya habari hasa hizo TV mi nafikri bado havijakomaa. Ni vile tu mwandishi mwenzao ndio yamemkuta hayo mauti na wao ndio wameanza kupiga kelele. Siku zote walikuwa wapi!!, kwani hayo yameanza leo!!, Napata shida kusema kama ingekuwa ni mtanzania mwingine wa kawaida yangepita juu juu tu, ingekuwa ni habari ya siku moja tu.
   
 5. sun wu

  sun wu JF-Expert Member

  #5
  Sep 8, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 2,025
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 0
  Yesterday's Glory..., Today's History....

  Kwenye hii Showbiz sidhani kama unaweza kuishi of what happened yesterday ukilala kidogo tu, wenzako wanakupita na ninaweza kusema huenda hawa jamaa wamelala usingizi wa pono, what matters is now..., not then...
   
 6. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #6
  Sep 8, 2012
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,548
  Likes Received: 18,216
  Trophy Points: 280
  Mkuu Lokissa, yule ni yeye, mimi ni member hapa jf, sheria yetu si hairuhusu kumfananisha member humu na yoyote!.

  Ujumbe utawafikia na soon mtawaona on U-Stream.

  Pamoja na sifa zote hizi kutoegemea upande wowote, ndio maana nikasisitiza wanastahili pongezi maana laiti ungemjua mmiliki na kumlinganisha na hii truthworthness, objectivity, Impartiality na fairness and balance, unaweza usiamini!.
   
 7. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #7
  Sep 8, 2012
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,548
  Likes Received: 18,216
  Trophy Points: 280
  Mkuu Big X, nakubaliana na wewe, hii police brutality haikuanza leo, tena japo mwanahabari mwenzetu amekufa kifo kibaya, but not painful but instant, kuna mamia wanakufa very slow death kwa mateso makuu ya torture behind closed doors na hawa kwa vile hatuwaoni, kele hazipigwi sana, ili kelele hizi zetu za sasa zinafuatia mwana media kuwa hit hard, where it hurts most!. Ni kilio hiki kitafungua pandora box ya police brutality na keweka precedence no more tear gas kwenye pecefull demonstration kama ile ya Waislamu ya ya juzi!, wale wangekuwa Chadema mbona mitaa ile mngeshuhudia dimbwi la damu!.
   
 8. MBWA HARUKI

  MBWA HARUKI Senior Member

  #8
  Sep 8, 2012
  Joined: Jul 3, 2012
  Messages: 143
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwanini watangazaji wengi wamepewa U-DC? Au ni moja ya sera za Magamba?
   
 9. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #9
  Sep 8, 2012
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 688
  Trophy Points: 280
  Pasco, tatizo la hivi vituo havikui. That is the problem, people grow in their profession and carrier, sasa mtu akishaona uwezo wake umekuwa mkubwa kuliko uwezo wa kituo kuutumia uwezo huo, anaona isiwe tabu, ngoja nitafute size yangu mbele.

  Pamoja na maswala ya maslahi na utaratibu wa ajira, bado tatizo lipo kwenye kukua kwa kituo.
  Imagine pamoja na ch ten kuwa kongwe, bado na yenyewe kama hizi nyingine haziwezi ku cover matukio live. Kunatokea mafuriko, hawawezi ku cover uokoaji, kunatokea meli kuzama, hakuna chombo cha habari kinachoweza kuonyesha kwa wakati ili kuona angalao tatizo ni kubwa kiasi gani.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 10. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #10
  Sep 8, 2012
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 50,860
  Likes Received: 23,483
  Trophy Points: 280
  Channel Ten mnaipata vizuri hapo Dodoma?
   
 11. maishapopote

  maishapopote JF Gold Member

  #11
  Sep 8, 2012
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 1,998
  Likes Received: 955
  Trophy Points: 280
  mkuu hii ni kweli na nakiri kuwa kuna tatizo kubwa katika management ya channel ten.....kubadilika ni ngumu sana
  unless something happen....Old habit die hard...
   
 12. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #12
  Sep 8, 2012
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,548
  Likes Received: 18,216
  Trophy Points: 280
  Mkuu Bigirita, vituo vyetu vingi vina matatizo, huwezi amini Channel Ten na ITV, pamoja na ukongwe wao wote, vyote viwili havina OB-Van hata moja!. Hii inamaanisha wote hawana uwezo wa kurusha live tukio lolote impromptu, kwa sababu wanatuia microwave link. TBC na Star TV wao wana OB Van na Clouds japo imeingia juzi tuu, tayari wana OB Van, sababu pekee inaowafanya Channel Ten na ITV mpaka leo hazina OB na kulipa maslahi duni sana kwa waandishi/watangazaji wao ni kuwa, wamiliki wa vituo hivi, wanavifanya vituo vyao ndio "cash cow" wao wa kumkamua maziwa!.

  Haiwezekani upike vipaji vyote halafu vikukimbie!.

  Hi unaamini kosa lililomfanya Misanya Bingi kufukuzwa kazi ni sababu alichaguliwa kujiunga udsm!. The same kwa Jerry Muro!. Charles Hillary akiwa bosi Radio One alipopata Ujerumani, alipoomba ruhusu mwajiri alimgomea, akaandika 24hrs notice na kutimka bila kusubiri majibu!, huwezi amini zengwe lilivurumishwa mpaka Ujerumani thanks God wenzetu wazungu, hawa entatain majungu majungu.

  Kwa mlioisikia ile Media Services Bill, aliwaamuru media oweners lazima waajiri professionals, kwa vile pro lazima uwalipe vizuri, hao medio owners wakiongozwa na MOAT ndio waliokuwa wapinzani wakuu wa sheria ile kwa kisingizio kuwa media ya Tanzania bado ni changa sana, haihitaji degree holders!, ili kuendelea kutumia cheap labor na kuendelea kukamua maziwa!.

  Tufike mahali media zetu sio tuu zilazimishwe kuwasomesha na kuwaendeleza staff wao, bali pia kuwalipa vizuri na kuwawekea bima!. Hiki kifo cha Daudi Mwangosi kitafumua mengi ambayo kiukweli, kitaleta ukombozi kwa wanahari wengi!.

  Kwa sheria za kazi, correspondence mwisho ni miezi 9, ukimuona hafai unaachana nae, ana faa unamuajiri!, media zetu zinaendeshwa na correspondence wengine zaidi ya miaka 10!. Tena kuwaita correspondent ndio tumewahishimu, kwa kifupi hao ni day worker kwa Kiswahili Kibarua!. Kapata ajali kazini, mwajiri anakana resiponsibilities!.
   
 13. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #13
  Sep 8, 2012
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,548
  Likes Received: 18,216
  Trophy Points: 280
  Channel Ten inapatikana supper kabisa Dodoma!.
   
Loading...