Chami: Ipatie Viwanda Nchi Yetu

Amanikwenu

Senior Member
Dec 1, 2009
187
0
Naomba nimuombe Dr. Chami afanye kila aliwezalo na timu yake katika Wizara ya Viwanda, Biashara na Masoko kuhakikisha kuwa nchi hii inakuwa na viwanda vya kutosha hasa vile vya kusindika mazao mbalimbali ya Wakulima wetu. Hili linawezekana. Ni suala la uamuzi. Itakuwa vizuri sana kama akianza na Kiwanda cha kusindika matunda mbalimbali katika wilaya ya Muheza au pale Segera. Njia nzuri ya kueneza viwanda hasa vya kati nchini ni kwa Serikali kuu kushirikiana na Halmashauri zetu kupata maeneo na kisha Serikali kuu kujenga viwanda husika na kisha kuwa na utaratibu wa kuuza HISA zake kwa wananchi wa maeneo husika ndani ya miaka mitano baada ya kiwanda husika kuanza uzalishaji. Kwa uwekezaji wa kati ya shilingi bilioni 2 mpaka 5 kwa kiwanda kimoja cha kati tutakuwa na uhakika wa kuwa na viwanda vingi ndani ya miaka 10 ijao. Lengo liwe ni kwa Serikali kuu kuwekeza angalau shilingi bilioni 250 kila mwaka katika ujenzi wa viwanda vya kati nchi nzima baada ya kufanya utafiti wa kutosha. Ili mpango huu uweze kufanikiwa ni muhimu sana kuvipa majukumu maalum vyuo vyetu vikuu (hasa SUA) na taasisi zetu mbali mbali za utafiti.
Mwaka 2006 wakati nikiwa Wilayani Njombe nilishangazwa sana na kijana ambaye amewekeza katika biashara ya kukamua mbegu za Alizeti na kuuza mafuta yake. Kilichonishangaza ni kuwa kijana huyo alikuwa anatumia mashine ndogo yenye thamani ya shilingi milioni 4 tu wakati huo lakini pamoja na watu kulima Alizeti huko Njombe bado alikuwa hapati Alizeti ya kutosha. Kutokana na hali hiyo alikuwa anafikiria uwezekano wa kwenda mkoani Singida kwa ajili ya kununua Alizeti. Kutokana na ukweli huu tunaweza kuona ni kwa kiasi Viwanda vya kusindika mazao mbalimbali ndiyo mkombozi kwa Wakulima wetu. Nje ya Viwanda tutakuwa tukisubiri miujiza katika kuindeleza nchi yetu. Mbaya zaidi hiyo miujiza haitakaa itokee hata siku moja.
 
Nyerere alijenga viwanda kila sehemu .... mafisi ya ssm yakala na kuviuwa vyotee.
Vilivyobaki vikapewa washirika wa wakuu wa ccm
 
Wala usihngaike mkuu as long as wako madarakani sahau manake hawahawa ndo waloua viwanda!
 
Hawa sera yao ilikuwa kuua viwanda kwa kisingizio cha ubinafsishaji.Leo hawawezi kugeka jiwe wataendelea na slogan yao ya kwamba serikali haifanyi biashara kwa upande mmoja na soko huru kwa upande wa pili.Chami hana jipya lao moja
 
Inasikitisha sana jinsi viwanda vyetu vilivyokufa. Ila dawa si kukaa kimya. Ni lazima tuendelee kuwaambia nini wanastahili kufanya. Gharama ya kujenga barabara yenye urefu wa kilomita moja ya lami kutokana na takwimu za Serikali ni shilingi bilioni 1.5. Kwa kiwango hiki cha fedha unaweza kujenga kiwanda kizuri cha ukubwa wa kati. Kwa mfano kiwanda cha kusindika Tangawizi Wilayani Same pamoja na mitambo yake kinategemewa kugharimu si zaidi ya shilingi bilioni 1.5. Kwa taarifa zaidi ni kuwa ukiwa na shilingi milioni 25 za Kitanzania una uhakika kwa kupata mashine toka China au India yenye uwezo wa kukamua zaidi ya tani mia tano za mbegu za Alizeti kwa siku.
 
Fikiria wewe utafanyaje uanzishe kiwanda.. this is the age of private enterprise... viwanda vya serikali sasa kwisha habari yake
 
He has been there for the past 5 yrs, any new plan??!! i dnt think so
 
Fikiria wewe utafanyaje uanzishe kiwanda.. this is the age of private enterprise... viwanda vya serikali sasa kwisha habari yake

Good suggestion.

Naamini mimi na ye yote yule hatuwezi kushindwa kujenga kiwanda cha kusindika mazao kama alizeti, au kusindika asali au kuwa na karakana za kisasa kwa ajili ya fenicha zitokanazo na mbao. Kisha kutokea hapo ktk kidogo tulichofanya twaweza kuchukua mikopo ili tupanue zaidi au tujenge mitambo mikubwa.
 
hao wahisani wao wanaowaambia serikali haifanyi biashara wao wanafanya biashara kupitia wananchi wao. serikali yetu inapaswa kuwawezesha wananchi wetu kufanya biashara, kiwa kuwapa mitaji na knowhow
 
hao wahisani wao wanaowaambia serikali haifanyi biashara wao wanafanya biashara kupitia wananchi wao. serikali yetu inapaswa kuwawezesha wananchi wetu kufanya biashara, kiwa kuwapa mitaji na knowhow

Asante kwa mawazo yako.
 
Good suggestion.

Naamini mimi na ye yote yule hatuwezi kushindwa kujenga kiwanda cha kusindika mazao kama alizeti, au kusindika asali au kuwa na karakana za kisasa kwa ajili ya fenicha zitokanazo na mbao. Kisha kutokea hapo ktk kidogo tulichofanya twaweza kuchukua mikopo ili tupanue zaidi au tujenge mitambo mikubwa.

Mkuu huko ndiko ninakoelekea. Tuombe MUNGU ndani ya miaka mitatu mambo yataanza kuonekana.
 
Mkuu huko ndiko ninakoelekea. Tuombe MUNGU ndani ya miaka mitatu mambo yataanza kuonekana.

Kama una kanafasi kidogo,wekeza ktk umeme huko vijijini mkuu, kuna maeneo yana vyanzo vya umeme na kwa siku za karibuni sio rahisi kupata umeme wa serikali na ukasababisha eneo likawa hai kwa viwanda vidogo vya mazao ya wakulima.

nawasilisha.
 
Back
Top Bottom