Amanikwenu
Senior Member
- Dec 1, 2009
- 187
- 0
Naomba nimuombe Dr. Chami afanye kila aliwezalo na timu yake katika Wizara ya Viwanda, Biashara na Masoko kuhakikisha kuwa nchi hii inakuwa na viwanda vya kutosha hasa vile vya kusindika mazao mbalimbali ya Wakulima wetu. Hili linawezekana. Ni suala la uamuzi. Itakuwa vizuri sana kama akianza na Kiwanda cha kusindika matunda mbalimbali katika wilaya ya Muheza au pale Segera. Njia nzuri ya kueneza viwanda hasa vya kati nchini ni kwa Serikali kuu kushirikiana na Halmashauri zetu kupata maeneo na kisha Serikali kuu kujenga viwanda husika na kisha kuwa na utaratibu wa kuuza HISA zake kwa wananchi wa maeneo husika ndani ya miaka mitano baada ya kiwanda husika kuanza uzalishaji. Kwa uwekezaji wa kati ya shilingi bilioni 2 mpaka 5 kwa kiwanda kimoja cha kati tutakuwa na uhakika wa kuwa na viwanda vingi ndani ya miaka 10 ijao. Lengo liwe ni kwa Serikali kuu kuwekeza angalau shilingi bilioni 250 kila mwaka katika ujenzi wa viwanda vya kati nchi nzima baada ya kufanya utafiti wa kutosha. Ili mpango huu uweze kufanikiwa ni muhimu sana kuvipa majukumu maalum vyuo vyetu vikuu (hasa SUA) na taasisi zetu mbali mbali za utafiti.
Mwaka 2006 wakati nikiwa Wilayani Njombe nilishangazwa sana na kijana ambaye amewekeza katika biashara ya kukamua mbegu za Alizeti na kuuza mafuta yake. Kilichonishangaza ni kuwa kijana huyo alikuwa anatumia mashine ndogo yenye thamani ya shilingi milioni 4 tu wakati huo lakini pamoja na watu kulima Alizeti huko Njombe bado alikuwa hapati Alizeti ya kutosha. Kutokana na hali hiyo alikuwa anafikiria uwezekano wa kwenda mkoani Singida kwa ajili ya kununua Alizeti. Kutokana na ukweli huu tunaweza kuona ni kwa kiasi Viwanda vya kusindika mazao mbalimbali ndiyo mkombozi kwa Wakulima wetu. Nje ya Viwanda tutakuwa tukisubiri miujiza katika kuindeleza nchi yetu. Mbaya zaidi hiyo miujiza haitakaa itokee hata siku moja.