Chambilecho Fidel Castro, "Mhukumuni Bashiru, historia itamwachia huru."

Kwa nini kama Bashiru anayaamini aliyoyapigania asijiuzuru au kuanzisha chama chake, madhubuti cha siasa?

Anachokisimamia hasa Bashiru ni nini? Mali za CCM tu?

Hiiiiii bagosha!
You have spoken too soon. Ukifahamu mchezo wa chess utaelewa you have to calculate your moves, na unapaswa utumie sana akili kuliko hisia. Na sasa hivi hayo ndio yanafanyika na wengi katika chama pendwa. Wanasema the truth is spoken in silence.
 
Sema nguvu ndio zilizotumika sio Bashiru. Na pia ni mali gani hizo?
Kuna aliyelalamika kaporwa mali yake kuwa ya CCM kimakosa na kwa nguvu!? Kumbuka Dr Bashiru ndiye alisimamia zoezi la kurejesha mali za CCM kwa kufanya uhakiki wa mali hizo kabla hajawa Katibu Mkuu wa Chama.

Na alipokuwa Katibu mkuu wa chama kwa kushirikina na "secretariet ya chama" wakaweka mfumo mzuri wa kukusanya mapato kutoka kwenye mali hizo. Sasa hivi CCM haihitaji kuomba kuchangiwa kuendesha shughuli zake za chama. Labda waanze hapo baadaye.
 
Kwanza hizo zinazoitwa mali za CCM asilimia 90% ni mali za Umma zilizozuchumwa na Watanzania wote kabla ya mfumo wa vyama vingi.
 
Leo nimeamka nikitafakari kuhusu mwalimu wangu Dk. Bashiru Ally. Tafakuri imenipeleka mbali hadi mwaka 2011, nikiwa mwaka wa tatu wa shahada yangu ya kwanza pale UDSM. Nyakati hizo nilikuwa mwenyekiti wa chama cha wanafunzi kilichojulikana kama Sauti ya Vijana Tanzania (SAVITA), huku Mwalimu Bashiru akiwa ndiye mlezi wetu. Mwaka huo, nilishiriki kuhariri jarida la Kigoda cha Taaluma cha Mwl Nyerere lililokuwa na lengo la kuadhimisha miaka mitatu ya "Kigoda", chini ya Prof Issa Shivji.

Mimi na mhariri mwenzangu tulikusanya makala kutoka kwa Wana-Kigoda zinazohusu ya tafakuri zao juu ya shughuli za kitaaluma na kimapambano zilizoongozwa na Kigoda. Mchangiaji mmoja hakutuma makala bali shairi. Shairi liliitwa, "Heko Nyingi Nawapeni, Kwa Kutimiza Ahadi." Mchangiaji huyo ni Dk Bashiru Ally, enzi hizo tukimwita "Mwalimu Bashiru." Na alilighani shairi hilo katika Tamasha la Kitaaluma la Mwalimu Nyerere mwezi Aprili 2011.

Mwezi Mei 2011 SAVITA iliandaa Kongamano la Kuadhimisha miaka 44 ya Azimio la Arusha. Mtoa mada alikuwa ni Prof Shivji, na mwongozaji ni Mwl Bashiru. Baada ya kongamano hilo nilistaafu uenyekiti wa SAVITA. Katika hotuba yangu ya kukabidhi uongozi, niliandika maneno haya, huku nikinukuu baadhi ya beti kutoka kwenye shairi la Dk Bashiru nililolitaja mwanzoni:
________________________
"Kwa walioishika vema, SAVITA iligeuka kuwa sehemu ya maisha yao ya kila siku. Matendo yao, mazungumzo yao, mavazi yao, matarajio yao, mitazamo yao na hata maamuzi juu ya nani awe rafiki ama adui vilijengeka katika misingi ya SAVITA niliyokwishaitaja hapo awali. Lakini, ashakum si matusi. Tuna jamii ya ajabu. Katika zama hizi za utandawazi, kuishika misingi hiyo ni ‘uendawazimu’. Tuna jamii ambayo itakushangaa usipoiba, itakukujeli usiposema uongo na itakutukana ukijidai una moyo wa kujitolea. Mwalimu Bashiru Ally aliyaona hili, ndio maana akaghani:

"Vita mliyoasisi, ni vita ya ukombozi,
Kukomboa Almasi, na samaki wa Zambezi,
Vilevile kuziasi, sera za ‘utandawizi’,
Heko nyingi nawapeni, kwa kutimiza ahadi.

"Vita ikishakolea, mtaiwa magaidi,
Hongo msipopokea, mtaitwa wakaidi,
Ushindi ukiwadia, mtaitwa mashahidi,
Heko nyingi nawapeni, kwa kutimiza ahadi."
___________________________

Miaka 10 imepita tangu niitoe hotuba ile. Sikujua kuwa niliyokuwa nikiyasema ndiyo yatamkuta gwiji huyu wa mapambano. Na shairi la Dk Bashiru pia limetimiza miaka 10. Nafikiri wakati akiliandika na kulighani hakuwa amejua yatakayotokea leo.

Kosa pekee alilofanya ni kuokoa mali za chama chake, ambapo hapo awali zilisemekana kuwa na thamani ya bilioni 60, ila baada ya uhakiki wa Kamati aliyoingoza ikagundulika kuwa zina thamani ya trilioni 1 (kwa mujibu wa vyombo vya habari). Mali za zaidi ya bilioni 940 zilikuwa zimeporwa na walafi, huku chama chake kikiwa kimewekwa mfukoni mwa mafisadi. Hao ndio wanaoongoza kumchafua leo hii.

Mara baada ya kuteuliwa kuwa katibu mkuu wa CCM, ziara yake ya kwanza aliifanya katika ofisi za Mtandao wa Wakulima Wadogo Tanzania - MVIWATA. Haikuwa mara ya kwanza kufika hapo bali alikuwa ni rafiki wa MVIWATA kwa muda mrefu kabla ya kuteuliwa. Hiyo ilifungua mlango mpya wa mshikamano katika kupambana dhidi ya uporaji wa ardhi, mbegu za kifo za GMO, rasimu ya sera mpya ya kiporaji ya ardhi, nk. Vijiji vya Msowero (Kilosa), Lukonde na Mtego wa Simba (Morogoro Vijijini), Mchukwi (Kibiti), Amboni (Tanga), na kwingineko vinamkumbuka kwa jinsi alivyoungana nao kupambana na mtandao wa waporaji wa ardhi, waliokuwa wakichoma nyumba za wanavijiji, kuwapiga na kuwafungulia wanavijiji mashtaka ya kughushi na kuchoma mazao yao mashambani. Haya huwezi kuyasikia kwenye vyombo vya habari. Kwa wavujajasho hao waliporwa ardhi, Mwalimu Bashiru ni shujaa. Huko wanamwombea dua na kumtakia heri. Ni nani atakayesikia sauti zao?

Mwaka jana, nikizungumza na Fr. Privatus Karugendo, aliniambia kuwa alishangazwa sana alipofika nyumbani kwa Bashiru akiwa katibu mkuu wa CCM. "Nyumba iko tupu. Anaishi maisha very simple," Fr Karugendo alinambia, huku akifurahi kuwa cheo hakikum-badilisha Bashiru. Hata alipolazimika kuvaa suti katika dhifa za kitaifa, alivaa 'suti za Kaunda' na sio koti na tai. Lakini vyake ni viatu vya wazi (sandles), suruali na shati.

Bashiru sio mtu wa vyeo na wala hakugombea cheo chochote. Aliteuliwa. Huyu ni mjamaa na wanamajumui wa Afrika. Samaki kwake majini, mjamaa kwake mapambanoni. Mwalimu wake, Nyerere, alipotoka Ikulu alirudi Butiama kushika jembe na kucheza bao na wanavijiji.

Natumai Mwl Bashiru atakapomaliza kutumikia nafasi yake ya uteuzi ya sasa, atarudi chuoni kufundisha, kutafiti na kushiriki katika mapambano ya wavujajasho kudai haki zao. Natumai tutapanda wote basi kwenda Morogoro kwenye mikutano ya MVIWATA. Natumai tutapanda tena bodaboda kwenda vijijini kujifunza kwa wavujajasho. Natumai atatutungia na kutughania mashairi ya kimapinduzi. Natumai tutakusanya tena maandiko ya wanamapinduzi, kuyatafsiri na kuyachapisha.

Fidel Castro alipotiwa korokoroni kwa kupambana dhidi ya ujahili nchini Cuba, alisema, "Nihukumuni. Historia itaniachia huru." Naam, historia ya mapambano dhidi ya ufisadi na uporaji wa rasilimali za wavujajasho itamwachia Mwl Bashiru huru. Na historia hiyo haitaandikwa na walafi na mafedhuli aliopambana nao. Itaandikwa na wakulima wadogo, wamachinga na bodaboda.

ASANTE SAMIA
Kuhusu mali za Chama nitakusahihisha. Hata CCM zile mali ilizozi acquire kabla ya 1992 siyo mali zake.

Kama Bashiru Ally angekuwa MKWELI na muwazi kama unavyotaka kum portray angetenganisha mali za Serikali na za CCM.

Kwa mfano viwanja vya mpira kama Maji Maji Songea, Sokoine Mbeya na CCM Kirumba, ni mali ya Watanzania wote.

Mimi mwandishi wa post hii mnamo mwaka 1977 nikiwa Form 3 nilishiriki kumwaga zege kwenye uwanja wa Sokoine Mbeya.

Bashiru ni mnafiki, hiyo ripoti ya mali za Chama aliiandika kumfurahisha aliyemtuma.
 
Chief wa Msoga gang na wapambe wake walipora mali za chama na kujimilikisha kinyemela kama zao. Na ndiyo hao sasa hivi wanamchafua Bashiru kwa nguvu zote.
Mbona naye Bashiru kakubali kujengewa gorofa na Rostam Aziz?? Bado unamuita mjamaa
 
Pamoja na machafu yoote anayotupiwa dk bashiru,ukweli ni kinyume chale, bashiru ni mzalendo,mwadilifu na mchapa kazi,huyu mtu ni moja Kati ya wajamaa waliobaki,
Mbona zile fedha za kuwanunulia akina Silinde, Gekul, Mollel walikuwa wanagawana Bashiru na Polepole na walengwa!!
 
You have spoken too soon. Ukifahamu mchezo wa chess utaelewa you have to calculate your moves, na unapaswa utumie sana akili kuliko hisia. Na sasa hivi hayo ndio yanafanyika na wengi katika chama pendwa. Wanasema the truth is spoken in silence.

Siasa hizi unazoziongelea wewe si siasa za kina Nyerere, Mandela, Castro, Che Guevara, Samora Machel na wenzao wengi walio watukuka kweri kweri.

Wewe unaongelea siasa za kinafiki, za akina Moi, Oginga, Kibaki, Ruto, waparamagamba, mwakyembe, bashiri, pole pole na wenzao. Siasa za kimaslahi zenye kupima upepo. Siasa hizi ni zile alizoziita Nyerere kuwa ni za kimalaya malaya tu.

Siasa hizi za kimalaya malaya haziwezi kuwa na tija katika jamii yoyote inayolenga haki na usawa kwa wote.
 
Mleta mada sijaelewa ni huruma unamwonea Bashiru au ni malalamiko kwa ccm kwa walichomfanyia Bashiru.

Ni hivi ccm ina wenyewe. Na wao huwa wanasema kabisa. Kasa la bashiru alifikiri angeweza kuibadili ccm irudi iwe ile ya mwalimu. Alipoingia humo tayari akawa kashajinajisi. Maana ccm ina uchafu wote.
Mambo ccm na serekali yake waliyokuwa/wanayowafanyia watu wa vyama vya upinzani yeye anajitoaje humo. Alikuwa akisema ccm itapata ushindi mkubwa. Alikuwa akijua wizi na uharibifu waliopanga dhidi ya upinzani.

Acha kumwonea huruma mtu ambaye kaamua kukaa na wezi, mafisadi, wauwaji, wabambikiaji watu kesi, waharibu chaguzi na mambo mengine kama hayo.
 
Siasa hizi unazoziongelea wewe si siasa za kina Nyerere, Mandela, Castro, Che Guevara, Samora Machel na wenzao wengi walio watukuka kweri kweri.

Wewe unaongelea siasa za kinafiki, za akina Moi, Oginga, Kibaki, Ruto, waparamagamba, mwakyembe, bashiri, pole pole na wenzao. Siasa za kimaslahi zenye kupima upepo. Siasa hizi ni zile alizoziita Nyerere kuwa ni za kimalaya malaya tu.

Siasa hizi za kimalaya malaya haziwezi kuwa na tija katika jamii yoyote inayolenga haki na usawa kwa wote.
Hata hao uliyosema walitukuka used the same game...na wataendelea til the end of time.
 
Watz wengi hasa huko CCM sasa hivi wanajivunia sana siasa hizo za kimalaya. Siasa za kuhalalisha udhalimu, ujambazi mradi tu 'zinashindisha' uchaguzi.
Siasa hizo ndio zinazoishia kuleta kutoaminiana hatimae vita iso na mwisho ya vyama na makundi mbalimbali tunayoona katika nchi mbalimbali hapa dunianiani.
Bashiru alipoingia CCM alifanya bidii sana kuimarisha UJINGA huo ambao, wakati akiwa 'Mwalimu' chuo kikuu alituaminisha wengi tu, kuwa yeye ni mwanamapinduzi wa kweli kutoka moyoni.
Walionunuliwa kutoka CHADEMA ndio wahanga waliyoharibikiwa zaidi na ndio maana wanathaminiwa zaidi. Wamefuzu kwenye huo umalaya na unafiki. Wako tayari kutunga na kusema lolote popote ili wapendwe huko uchawini.
Mungu mwenye nguvu yupo, hataachia ujinga huo kukomaa
 
Leo nimeamka nikitafakari kuhusu mwalimu wangu Dk. Bashiru Ally. Tafakuri imenipeleka mbali hadi mwaka 2011, nikiwa mwaka wa tatu wa shahada yangu ya kwanza pale UDSM. Nyakati hizo nilikuwa mwenyekiti wa chama cha wanafunzi kilichojulikana kama Sauti ya Vijana Tanzania (SAVITA), huku Mwalimu Bashiru akiwa ndiye mlezi wetu. Mwaka huo, nilishiriki kuhariri jarida la Kigoda cha Taaluma cha Mwl Nyerere lililokuwa na lengo la kuadhimisha miaka mitatu ya "Kigoda", chini ya Prof Issa Shivji.

Mimi na mhariri mwenzangu tulikusanya makala kutoka kwa Wana-Kigoda zinazohusu ya tafakuri zao juu ya shughuli za kitaaluma na kimapambano zilizoongozwa na Kigoda. Mchangiaji mmoja hakutuma makala bali shairi. Shairi liliitwa, "Heko Nyingi Nawapeni, Kwa Kutimiza Ahadi." Mchangiaji huyo ni Dk Bashiru Ally, enzi hizo tukimwita "Mwalimu Bashiru." Na alilighani shairi hilo katika Tamasha la Kitaaluma la Mwalimu Nyerere mwezi Aprili 2011.

Mwezi Mei 2011 SAVITA iliandaa Kongamano la Kuadhimisha miaka 44 ya Azimio la Arusha. Mtoa mada alikuwa ni Prof Shivji, na mwongozaji ni Mwl Bashiru. Baada ya kongamano hilo nilistaafu uenyekiti wa SAVITA. Katika hotuba yangu ya kukabidhi uongozi, niliandika maneno haya, huku nikinukuu baadhi ya beti kutoka kwenye shairi la Dk Bashiru nililolitaja mwanzoni:
________________________
"Kwa walioishika vema, SAVITA iligeuka kuwa sehemu ya maisha yao ya kila siku. Matendo yao, mazungumzo yao, mavazi yao, matarajio yao, mitazamo yao na hata maamuzi juu ya nani awe rafiki ama adui vilijengeka katika misingi ya SAVITA niliyokwishaitaja hapo awali. Lakini, ashakum si matusi. Tuna jamii ya ajabu. Katika zama hizi za utandawazi, kuishika misingi hiyo ni ‘uendawazimu’. Tuna jamii ambayo itakushangaa usipoiba, itakukujeli usiposema uongo na itakutukana ukijidai una moyo wa kujitolea. Mwalimu Bashiru Ally aliyaona hili, ndio maana akaghani:

"Vita mliyoasisi, ni vita ya ukombozi,
Kukomboa Almasi, na samaki wa Zambezi,
Vilevile kuziasi, sera za ‘utandawizi’,
Heko nyingi nawapeni, kwa kutimiza ahadi.

"Vita ikishakolea, mtaiwa magaidi,
Hongo msipopokea, mtaitwa wakaidi,
Ushindi ukiwadia, mtaitwa mashahidi,
Heko nyingi nawapeni, kwa kutimiza ahadi."
___________________________

Miaka 10 imepita tangu niitoe hotuba ile. Sikujua kuwa niliyokuwa nikiyasema ndiyo yatamkuta gwiji huyu wa mapambano. Na shairi la Dk Bashiru pia limetimiza miaka 10. Nafikiri wakati akiliandika na kulighani hakuwa amejua yatakayotokea leo.

Kosa pekee alilofanya ni kuokoa mali za chama chake, ambapo hapo awali zilisemekana kuwa na thamani ya bilioni 60, ila baada ya uhakiki wa Kamati aliyoingoza ikagundulika kuwa zina thamani ya trilioni 1 (kwa mujibu wa vyombo vya habari). Mali za zaidi ya bilioni 940 zilikuwa zimeporwa na walafi, huku chama chake kikiwa kimewekwa mfukoni mwa mafisadi. Hao ndio wanaoongoza kumchafua leo hii.

Mara baada ya kuteuliwa kuwa katibu mkuu wa CCM, ziara yake ya kwanza aliifanya katika ofisi za Mtandao wa Wakulima Wadogo Tanzania - MVIWATA. Haikuwa mara ya kwanza kufika hapo bali alikuwa ni rafiki wa MVIWATA kwa muda mrefu kabla ya kuteuliwa. Hiyo ilifungua mlango mpya wa mshikamano katika kupambana dhidi ya uporaji wa ardhi, mbegu za kifo za GMO, rasimu ya sera mpya ya kiporaji ya ardhi, nk. Vijiji vya Msowero (Kilosa), Lukonde na Mtego wa Simba (Morogoro Vijijini), Mchukwi (Kibiti), Amboni (Tanga), na kwingineko vinamkumbuka kwa jinsi alivyoungana nao kupambana na mtandao wa waporaji wa ardhi, waliokuwa wakichoma nyumba za wanavijiji, kuwapiga na kuwafungulia wanavijiji mashtaka ya kughushi na kuchoma mazao yao mashambani. Haya huwezi kuyasikia kwenye vyombo vya habari. Kwa wavujajasho hao waliporwa ardhi, Mwalimu Bashiru ni shujaa. Huko wanamwombea dua na kumtakia heri. Ni nani atakayesikia sauti zao?

Mwaka jana, nikizungumza na Fr. Privatus Karugendo, aliniambia kuwa alishangazwa sana alipofika nyumbani kwa Bashiru akiwa katibu mkuu wa CCM. "Nyumba iko tupu. Anaishi maisha very simple," Fr Karugendo alinambia, huku akifurahi kuwa cheo hakikum-badilisha Bashiru. Hata alipolazimika kuvaa suti katika dhifa za kitaifa, alivaa 'suti za Kaunda' na sio koti na tai. Lakini vyake ni viatu vya wazi (sandles), suruali na shati.

Bashiru sio mtu wa vyeo na wala hakugombea cheo chochote. Aliteuliwa. Huyu ni mjamaa na wanamajumui wa Afrika. Samaki kwake majini, mjamaa kwake mapambanoni. Mwalimu wake, Nyerere, alipotoka Ikulu alirudi Butiama kushika jembe na kucheza bao na wanavijiji.

Natumai Mwl Bashiru atakapomaliza kutumikia nafasi yake ya uteuzi ya sasa, atarudi chuoni kufundisha, kutafiti na kushiriki katika mapambano ya wavujajasho kudai haki zao. Natumai tutapanda wote basi kwenda Morogoro kwenye mikutano ya MVIWATA. Natumai tutapanda tena bodaboda kwenda vijijini kujifunza kwa wavujajasho. Natumai atatutungia na kutughania mashairi ya kimapinduzi. Natumai tutakusanya tena maandiko ya wanamapinduzi, kuyatafsiri na kuyachapisha.

Fidel Castro alipotiwa korokoroni kwa kupambana dhidi ya ujahili nchini Cuba, alisema, "Nihukumuni. Historia itaniachia huru." Naam, historia ya mapambano dhidi ya ufisadi na uporaji wa rasilimali za wavujajasho itamwachia Mwl Bashiru huru. Na historia hiyo haitaandikwa na walafi na mafedhuli aliopambana nao. Itaandikwa na wakulima wadogo, wamachinga na bodaboda.

ASANTE SAMIA
Kosa ni tungo tata 'He does keep his words, public figures have to keep their words'pia alikuwa anajtoa ufahamu ama uyumbu 'herding behavior' thoughtful people suspend their individual reasoning because of fear
 
Hata hao uliyosema walitukuka used the same game...na wataendelea til the end of time.

Siyo Nyerere, Mandela, Castro, Che Guevara wala wa namna hiyo. Fanya tafiti kujiridhisha.

Hao siyo Jiwe, Kabudi, Mwakyembe wala hao unao wadhani.

Hukuwahi kusikia ndo ndo ndo si chururu? Wacha mjomba kina mandela? Hizo zilikuwa namba zingine.
 
Leo nimeamka nikitafakari kuhusu mwalimu wangu Dk. Bashiru Ally. Tafakuri imenipeleka mbali hadi mwaka 2011, nikiwa mwaka wa tatu wa shahada yangu ya kwanza pale UDSM. Nyakati hizo nilikuwa mwenyekiti wa chama cha wanafunzi kilichojulikana kama Sauti ya Vijana Tanzania (SAVITA), huku Mwalimu Bashiru akiwa ndiye mlezi wetu. Mwaka huo, nilishiriki kuhariri jarida la Kigoda cha Taaluma cha Mwl Nyerere lililokuwa na lengo la kuadhimisha miaka mitatu ya "Kigoda", chini ya Prof Issa Shivji.

Mimi na mhariri mwenzangu tulikusanya makala kutoka kwa Wana-Kigoda zinazohusu ya tafakuri zao juu ya shughuli za kitaaluma na kimapambano zilizoongozwa na Kigoda. Mchangiaji mmoja hakutuma makala bali shairi. Shairi liliitwa, "Heko Nyingi Nawapeni, Kwa Kutimiza Ahadi." Mchangiaji huyo ni Dk Bashiru Ally, enzi hizo tukimwita "Mwalimu Bashiru." Na alilighani shairi hilo katika Tamasha la Kitaaluma la Mwalimu Nyerere mwezi Aprili 2011.

Mwezi Mei 2011 SAVITA iliandaa Kongamano la Kuadhimisha miaka 44 ya Azimio la Arusha. Mtoa mada alikuwa ni Prof Shivji, na mwongozaji ni Mwl Bashiru. Baada ya kongamano hilo nilistaafu uenyekiti wa SAVITA. Katika hotuba yangu ya kukabidhi uongozi, niliandika maneno haya, huku nikinukuu baadhi ya beti kutoka kwenye shairi la Dk Bashiru nililolitaja mwanzoni:
________________________
"Kwa walioishika vema, SAVITA iligeuka kuwa sehemu ya maisha yao ya kila siku. Matendo yao, mazungumzo yao, mavazi yao, matarajio yao, mitazamo yao na hata maamuzi juu ya nani awe rafiki ama adui vilijengeka katika misingi ya SAVITA niliyokwishaitaja hapo awali. Lakini, ashakum si matusi. Tuna jamii ya ajabu. Katika zama hizi za utandawazi, kuishika misingi hiyo ni ‘uendawazimu’. Tuna jamii ambayo itakushangaa usipoiba, itakukujeli usiposema uongo na itakutukana ukijidai una moyo wa kujitolea. Mwalimu Bashiru Ally aliyaona hili, ndio maana akaghani:

"Vita mliyoasisi, ni vita ya ukombozi,
Kukomboa Almasi, na samaki wa Zambezi,
Vilevile kuziasi, sera za ‘utandawizi’,
Heko nyingi nawapeni, kwa kutimiza ahadi.

"Vita ikishakolea, mtaiwa magaidi,
Hongo msipopokea, mtaitwa wakaidi,
Ushindi ukiwadia, mtaitwa mashahidi,
Heko nyingi nawapeni, kwa kutimiza ahadi."
___________________________

Miaka 10 imepita tangu niitoe hotuba ile. Sikujua kuwa niliyokuwa nikiyasema ndiyo yatamkuta gwiji huyu wa mapambano. Na shairi la Dk Bashiru pia limetimiza miaka 10. Nafikiri wakati akiliandika na kulighani hakuwa amejua yatakayotokea leo.

Kosa pekee alilofanya ni kuokoa mali za chama chake, ambapo hapo awali zilisemekana kuwa na thamani ya bilioni 60, ila baada ya uhakiki wa Kamati aliyoingoza ikagundulika kuwa zina thamani ya trilioni 1 (kwa mujibu wa vyombo vya habari). Mali za zaidi ya bilioni 940 zilikuwa zimeporwa na walafi, huku chama chake kikiwa kimewekwa mfukoni mwa mafisadi. Hao ndio wanaoongoza kumchafua leo hii.

Mara baada ya kuteuliwa kuwa katibu mkuu wa CCM, ziara yake ya kwanza aliifanya katika ofisi za Mtandao wa Wakulima Wadogo Tanzania - MVIWATA. Haikuwa mara ya kwanza kufika hapo bali alikuwa ni rafiki wa MVIWATA kwa muda mrefu kabla ya kuteuliwa. Hiyo ilifungua mlango mpya wa mshikamano katika kupambana dhidi ya uporaji wa ardhi, mbegu za kifo za GMO, rasimu ya sera mpya ya kiporaji ya ardhi, nk. Vijiji vya Msowero (Kilosa), Lukonde na Mtego wa Simba (Morogoro Vijijini), Mchukwi (Kibiti), Amboni (Tanga), na kwingineko vinamkumbuka kwa jinsi alivyoungana nao kupambana na mtandao wa waporaji wa ardhi, waliokuwa wakichoma nyumba za wanavijiji, kuwapiga na kuwafungulia wanavijiji mashtaka ya kughushi na kuchoma mazao yao mashambani. Haya huwezi kuyasikia kwenye vyombo vya habari. Kwa wavujajasho hao waliporwa ardhi, Mwalimu Bashiru ni shujaa. Huko wanamwombea dua na kumtakia heri. Ni nani atakayesikia sauti zao?

Mwaka jana, nikizungumza na Fr. Privatus Karugendo, aliniambia kuwa alishangazwa sana alipofika nyumbani kwa Bashiru akiwa katibu mkuu wa CCM. "Nyumba iko tupu. Anaishi maisha very simple," Fr Karugendo alinambia, huku akifurahi kuwa cheo hakikum-badilisha Bashiru. Hata alipolazimika kuvaa suti katika dhifa za kitaifa, alivaa 'suti za Kaunda' na sio koti na tai. Lakini vyake ni viatu vya wazi (sandles), suruali na shati.

Bashiru sio mtu wa vyeo na wala hakugombea cheo chochote. Aliteuliwa. Huyu ni mjamaa na wanamajumui wa Afrika. Samaki kwake majini, mjamaa kwake mapambanoni. Mwalimu wake, Nyerere, alipotoka Ikulu alirudi Butiama kushika jembe na kucheza bao na wanavijiji.

Natumai Mwl Bashiru atakapomaliza kutumikia nafasi yake ya uteuzi ya sasa, atarudi chuoni kufundisha, kutafiti na kushiriki katika mapambano ya wavujajasho kudai haki zao. Natumai tutapanda wote basi kwenda Morogoro kwenye mikutano ya MVIWATA. Natumai tutapanda tena bodaboda kwenda vijijini kujifunza kwa wavujajasho. Natumai atatutungia na kutughania mashairi ya kimapinduzi. Natumai tutakusanya tena maandiko ya wanamapinduzi, kuyatafsiri na kuyachapisha.

Fidel Castro alipotiwa korokoroni kwa kupambana dhidi ya ujahili nchini Cuba, alisema, "Nihukumuni. Historia itaniachia huru." Naam, historia ya mapambano dhidi ya ufisadi na uporaji wa rasilimali za wavujajasho itamwachia Mwl Bashiru huru. Na historia hiyo haitaandikwa na walafi na mafedhuli aliopambana nao. Itaandikwa na wakulima wadogo, wamachinga na bodaboda.

ASANTE SAMIA
Unajaribu kumsafisha mratibu wa business ya ununuzi wa wabunge na madiwani,? Eti kuunga mkono juhudi za jiwe!! Jamaa ametapanya sana pesa za walipa kodi
 
Mbunge wa kuteuliwa, mzalendo husimamia hoja yake. Mzalendo uwa kama kuna uchafu atausema wazi wazi bila kukaa kimya kisa kapewa ubunge wa kuteuliwa.

Hana uzalendo wowote huyo. Hakuna mjamaa Afrika walishakufa na kuzikwa. Kamsifuni wana CCM, mzalendo ni yule atakayepigania maslahi ya taifa siyo kuweka chama mbele.

We Bashiru unamfahamu ukiwa UDSM, mimi Bashiru namfahamu toka miaka ya 90 akiwa mwalimu wa Sekondari ya Kashozi hapo Bukoba.
Aah, kitu cha kwanza binafsi nilisoma shule ya msingi Kashozi - mimi Bashiru simfahamu physically ie sijawahi kukutana nae hata siku moja, na kusema kweli hakuna haja kinachi vuma kwa Dk.Bashiru ni sifa zake za kizalendo na zilizo tukuka kusema kweli, anajulikana kwa kutopenda makuu,kujikweza na kusimamia haki - hiyo ndio inbuilt hulka yake sifa hizo zinajulikana mpaka kijijini alipo zaliwa.

Mkuu unapo sema nafamiana na Dk. Bashiru tangu nikiwa UDSM sijui unamaanisha nini? Kwa taarifa yako nimesoma Vyuo Vikuu vya nchi za nje - sijawahi kusoma Chuo Kikuu chochote hapa Tanzania consequently madai yako hayana ukweli wowote.
 
Kila mtu hubadilika, na hawa watu wanaojifanya wazalendo wakiwa wananjaa wakipata ulaji wanageuka kabisa.
Siasa sijui ina nini. Inawabadilisha watu hadi wanakuka matapishi yao. Polepole yale yote aliyokuwa akisema kwenye mijadara ya katiba leo anaweza kuyakana, prof kabudi hadi aliowafundisha hawaamini wanachokiona, upepo huo huo umempitia Bashiru. Pale alikuwa anasema hayo alikuwa hajaona milango ikiwa wazi kwake, pale alipoona anapoweza kufika hapo ndipo uzalendo uwekwa pembeni
 
Back
Top Bottom