Tetesi: Chama tawala na Upinzani kukumbwa na mtikisiko, mapya kuibuka

MAHANJU

JF-Expert Member
Aug 26, 2014
5,244
7,970
Ni mwanasiasa ambaye anaonekana kuwa na uungwaji mkono nje na ndani ya Chama tawala, ni kwamba huyu ni kiongozi mkubwa ndani ya serikali ya awamu hii na iliyopita. Analo kundi kubwa la vijana na wasomi wengi nyuma yake, anapata uungwaji mkono na moja ya familia ya kiongozi Mkubwa mustaafu wa taifa letu na anaweza kuungana nae kuunganisha nguvu kua kitu kimoja na kuanza harakati zao mpya za kisiasa.

Ataondoka ndani ya Chama tawala na kundi lake na kuanzisha chama kipya cha siasa, sababu ya kuondoka ndani ya Chama tawala kulalamikia uminywaji wa demokrasia na kunyimwa Uhuru wa maoni ndani ya Chama.Haridhishwi kabisa uendeshwaji wa chama na kutokukubaluana na utaratibu wa uendeshwaji huo. Anaamini kua kwa uendeshwaji huu wa sasa huenda skakosa fursa ya kutimiza ndoto zake.

Anaondoka na vijana wengi ndani ya chama tawala alipo hivi sasa na kuna uwezekano wa kuungwa mkono na vijana wengine wengi kutoka upinzani ambao wanahisi kua huenda ndiye mwenye mtizamo mpya wa siasa za Tanzania, anaamini kua vijana ndio watakaompa nguvu kukikuza chama chake na kukisambaza katika maeneo mbalimbali nchini. Pia kuna uwezekano Mkubwa wa viongozi wengi ambao wamo ndani ya serikali ya sasa baadae wakamuunga mkono na kuunganisha nguvu ya pamoja.

Kabla ya 2020 anaweza kuungana na nyama vingine vikuu vya upinzani ili kutengenze nguvu ya pamoja kuingia magogoni kwa sanduku la kura.Mpaka sasa inasemekana kuwa anayo mahusiano mazuri na baadhi ya viongozi wakuu wa vyama vya upinzani ingawa yeye bado yuko Chama tawala.
 
Angehakikisha mfumo na muundo wa tume ya uchaguzi, katiba mpya nk vinapatikana kwanza akiwa huko ndani ya chama tawala (mkoloni mweusi) ndo aanzishe chama. Kinyume na hapo hatacheleweshwa kupotea kama saa8 na kabwela.
 
Vipi, na dc aliyejiuzulu anahusiana naye au!?
Tatizo ni kimhusisha na 'kiongozi mstaafu' itaibua hoja za makaburi yasiyofukuliwa na maswali yasiyojibika kama wezi wa makontena bandarini, 'hewa hewa' au uhalisia wa gharama za ujenzi wa bomba la gesi kama ni uS $1.2b.
 
Mimi nikishasikia "watamfuata baadaye" huwa naondoka. Nitarudi baadaye. Hayati Sitta aliahidi wengi kuwa waondoke yeye atawafuata baadaye. Sasa wao ndio watamfuata baadaye.
 
Kama sio fisadi sawa hata Mimi nitaunganisha nguvu..........

Ila kama ni mwizi hapana credible yangu ya kwanza ni Ufisadi...............
 
Vipi, na dc aliyejiuzulu anahusiana naye au!?
Tatizo ni kimhusisha na 'kiongozi mstaafu' itaibua hoja za makaburi yasiyofukuliwa na maswali yasiyojibika kama wezi wa makontena bandarini, 'hewa hewa' au uhalisia wa gharama za ujenzi wa bomba la gesi kama ni uS $1.2b.
Katika hilo la makaburi yasiyofukuliwa wengi wanadhani ni kuhusu walioko nje ya system kumbe sio. Ni wazi kuwa ukifukua hayo makaburi waweza kukuta roho ya mfukuaji iko huko ingawa mwili tunao huku duniani. Mfukuaji hata kama angekuwa kichaa hilo analijua na hawezi kulifanya kamwe
 
Kwa namna alivyoendesha zoezi la kujitangaza na kuomba uungwaji mkono mwaka 2015, sio MTU wa kubeza, ni moja ya vijana walioonyesha uwezo wa juu na "kisasa" zaidi. Yale mabasi, technology nk. Si MTU wa kubeza. Ingawa hapa naona umetumia hisia zako na kumtengezea story kijana marope
 
Back
Top Bottom