Chama tawala: Chama kinachoongoza serikali, Chama cha upinzani: Chama shindani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chama tawala: Chama kinachoongoza serikali, Chama cha upinzani: Chama shindani

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Magobe T, Jun 30, 2010.

 1. M

  Magobe T JF-Expert Member

  #1
  Jun 30, 2010
  Joined: Mar 19, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 357
  Trophy Points: 180
  Ndugu wanaJF, kama mwezi hivi niliangalia TV wakati wa mjadala fulani. Kwenye huo mjadala, wachangiaji walichangia, pamoja na mambo mengine, kuwa inabidi matumizi yetu ya maneno yawe chanya. Niliguswa na jinsi baadhi yao walivyoshauri kuhusu matumizi chanya ya maneno kama CHAMA TAWALA na CHAMA CHA UPINZANI. Nimeona nililete hoja hii kwenye JF ili kuwashirikisha na hatimaye tuweze, kwa pamoja, kuamua tufanye nini.

  Nashauri badala ya kusema CHAMA TAWALA kuanzia sasa tuseme CHAMA KINACHOONGOZA SERIKALI au (CHAMA KINACHOONGOZA) na badala ya kusema CHAMA CHA UPINZANI tuseme CHAMA SHINDANI. Kwa Kiingereza, badala ya RULING PARTY tuseme THE PARTY FORMING THE EXISTING GOVERNMENT na badala ya OPPOSITION PARTY tuseme COMPETITIVE PARTY.

  Maana yangu ni kutaka kuleta ushawishi kuhusu matumizi haya kuanzia vyombo vya habari, bungeni, mikutanoni na hata shuleni na vyuoni. Kufanya hivi ni kuondokana na dhana hasi na kuanza kujenga dhana chanya kuhusu vyama vyetu vya siasa na siasa kwa ujumla. Pia tutaweza kuleta maana nzuri ya uongozi wa kisiasa na kuondoka na fikira potofu zinazotufanya tujione maadui na sio washindani wa kisiasa pale tunapotofautiana kuhusu vipaumbele vyetu au maslahi ya wananchi. Je, wanaJF wenzangu mna maoni gani?

  Kama mtakubaliana na mimi basi tuanze kutumia hizi dhana mpya kuanzia sasa. Au kama kuna maneo mengine yenye maana zaidi, basi tuyaweke ili tuyatumie. Nawasilisha!

   
 2. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #2
  Jun 30, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  What's in a name?
   
 3. M

  Magobe T JF-Expert Member

  #3
  Jun 30, 2010
  Joined: Mar 19, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 357
  Trophy Points: 180
  As far as I am concerned, words create an attitude, mindset and behavioursl pattern.
   
 4. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #4
  Jun 30, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  OK -- suppose CCM adopts a different name, say Chama cha Kutetea Haki (CCKH), will it automatically unpeel itself from the ufisadi mess it's now immersed in?
   
 5. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #5
  Jun 30, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Hoja ya Magobe naona haijaeleweka kwa wengi. Msomeni vizuri kabla hamjajibu maana majibu mengi ninayoyaona nina hakika hayalengi kwenye hoja anayotaka watu wachangie maoni yao!
   
Loading...