Chama pinzani (Democrats) chakiri Joe Biden hawezi ku-debate na Donald Trump kwenye kampeni za urais 2020

sky soldier

JF-Expert Member
Mar 30, 2020
5,408
19,032

Wapinzani (Democrats) Hatimae wameuona Mwanga baada ya safari ndefu kwenye handaki, sasa ni dhahiri hata kwao kwamba Kumsdinda Trump kwa kumtumia mgombea wao Joe Biden ni kama kumchuna ngozi kupe, Haiwezekani,

Ni wazi katika hio video Nancy Pelosi amekiri kwamba Mgombea uraisi kwa tiketi ya chama chake (democrats) hataweza kupambana na trump katika mdahalo

Licha ya wamarekani kujua hili wazi ya kwamba Joe Biden atageuzwa kuwa Punching Bag ya Trump kwenye mdahalo lakini wamarekani hawajakubali huu ujumbe wa democrats maana uraisi ni hatma itayoamua muenendo wa wamarekani kiujumla, hivyo wamarekani wana kiu ya kuona mdahalo

Je kama Joe Biden Mgombea Uraisi hawezi au anaogopa kufanya debate na trump, atawaweza wachina ??? au ataishia tena kupokea zile trilioni 3 za rushwa??

Ila pengine ni kweli kabisa Biden kapewa ushauri mzuri sana maana sioni namna atayo debate na trump hasa ukizingatia ugonjwa wake wa kusahau kwa sana zikiambatanishwa na matusi na hasira kali, Perharps its the best course of action.

1598634834206.png
 
Hapa mm ndio nasemaga nahis hii nchi ni chama kimoja tu sema Elites huwa wanachezaga na akili za wananchi wao tu, kwa sababu kweli dems na watu woote walionao kwamba walishindwa leta mtu competate haswa wa kumpa high challange DT wakaona wamsimamishe Biden kweli? Hapo ni kwamba wameona DT amalize muda wake ndio maana
 
Kwamba msema ovyo Trump atamshinda Biden? Si kweli hata kidogo, kambi ya Trump wanahaha sana sana.
 
Kwamba msema ovyo Trump atamshinda Biden? Si kweli hata kidogo, kambi ya Trump wanahaha sana sana.
Hahahha Biden huyu huyu ambae anaoanda jukwaan anasahau hata alichokua anataka sema? Acha kuchekesha watu hapa Biden kushinda Nov haipo mark my words
 
Biden hayuko peke yake, hata hapa kwetu kuna wagombea leo hii ukiwaambia mambo ya mdahalo wanaweza wakakutumia wasiojulikana wakumalize kabisa.

Mdahalo sio mchezo ukizingatia pia kwamba wapinzani wako nao wanapewa fursa kukulima maswali na ndio wanakuchapa swali linalohusu kitendo labda cha kihalifu ulilofanya ukiwa madarakani ndipo unatokwa jasho hadi kwenye makucha na huna la kuwafanya. Mdahalo ni noma sana, Democrats wanajua hilo na hata ccm wanalifahamu hilo, tena vizuri sana.
 
Hapa mm ndio nasemaga nahis hii nchi ni chama kimoja tu sema Elites huwa wanachezaga na akili za wananchi wao tu, kwa sababu kweli dems na watu woote walionao kwamba walishindwa leta mtu competate haswa wa kumpa high challange DT wakaona wamsimamishe Biden kweli? Hapo ni kwamba wameona DT amalize muda wake ndio maana
Mkuu,watu hawajui kwamba urais wa marekani ni wa kimkakati sana,usishangae hata Joe Biden mwenyewe anajua kwamba DT anatakiwa kurudi madarakani kumalizia misheni alizoanzisha.Hasa vita ya kiuchumi dhidi ya China.
 
Ndio maana ake yaan anajua kabisa kwamba hapa namsindikiza mshkaji tuu.....wananchi ndio wanapumbazwa tena wachache tuu wale wasio na maseke
 
Biden hayuko peke yake, hata hapa kwetu kuna wagombea leo hii ukiwaambia mambo ya mdahalo wanaweza wakakutumia wasiojulikana wakumalize kabisa.

Mdahalo sio mchezo ukizingatia pia kwamba wapinzani wako nao wanapewa fursa kukulima maswali na ndio wanakuchapa swali linalohusu kitendo labda cha kihalifu ulilofanya ukiwa madarakani ndipo unatokwa jasho hadi kwenye makucha na huna la kuwafanya. Mdahalo ni noma sana, Democrats wanajua hilo na hata ccm wanalifahamu hilo, tena vizuri sana.
Tulitegemea kiongozi aliye madarakani ndio aogope mdahalo sababu tuna assume ana mapungufu mengi kwemye utawala wake.Trump ndio alitegemewa aogope mdahalo sababu ana mapungufu mengi sana,sasa kinyume chake wapinzani wake ndio wanaingia mitini,that's not natural aisee.
Trump japo ana matatizo mengi kiuongozi lakini nahisi watu wamampenda sababu ya kujiamini kwake,naturaly hata wanawake wanapenda mwanaume anayejiamini sio lelemama anayelialia kila saa,hata 2016 Trump alipigiwa kura nyingi sana na wanawake licha ya scandal zake na wanawake..
 
Kwamba msema ovyo Trump atamshinda Biden? Si kweli hata kidogo, kambi ya Trump wanahaha sana sana.
Ukitizama kwa makini,punde baada ya RNC kukamilika polls zimeanza ku tally au kukaribiana sana kwenye states ambazoalikuwa anaongoza Biden,unajua kwa nini?.RNC walienda na mkakati wa kueleza mafanikio ya Republican chini ya Trump kama rais,wao DNC walienda kumzodoa Trump bila kusema wataifanyia nini hasa USA.Kingine hili suala la vurugu na maandamano limewaharibia sana Liberals,waliweka unafiki mbele badala ya Facts,Naturally hakuna binadamu atapenda uchumi wake uharibiwe kisa maandamano,watu wengi walibadilika na kuja upande wa trump baada ya kuona hakuna protest tena bali uharibifu wa mali kwa hisia za kisiasa..
 
Ndio maana ake yaan anajua kabisa kwamba hapa namsindikiza mshkaji tuu.....wananchi ndio wanapumbazwa tena wachache tuu wale wasio na maseke
Yaani baada ya DNC kumpitisha Biden na hali yake ileile,nilijisemea kuna kitu tunachezewa hapa hatukielewi kabisa,Hasa huyu bibi Pelosi anatumika na deep state kumrudisha Trump WH either kwa kujua au kutokujua...Kuna mamluki kule DNC i can guess..
 
Rais au PMs anayetetea kiti chake ndiye anayetakiwa kukumbia debates. Tony Blair pamoja na uwezo wake mkubwa wa kujieleza alikuwa anakumbia debates wakati akiwa PM mpaka wamlazimishe. Lakini ukiona aliyeko madarakani ndio anataka debate tena in the middle of a pandemic ujuwe kapata KIMEO!!
 
Back
Top Bottom