Chama makini sasa kimepatikana ccm kaeni chonjo

maarufu

Member
Nov 28, 2010
63
1
JAMANI WANAJAMVI NILIKUWA NAPITIA KITABU CHA NYERERE CHA UONGOZI WETU NA HATIMA YA TANZANIA NIMEONA NI VEMA NINUKUU
"...Nilisema awali kwamba kansa ya uongozi ndani ya Chama Cha Mapinduzi isingekuwa ni jambo la kutisha sana kama tungekuwa tumeanza kuona kizuri cha upinzani kinachoweza kuiongoa nchi yetu badala ya CCM. Ubovu wa uongozi ndani ya CCM ndio uliofanya nikapendekeza tuanzishe mfumo wa vyama vingi. Nilitumaini kuwa tunaweza kupata chama kingine kizuri ambacho kingeweza kuiongoza nchi yetu badala CCM au ambacho kingekilazimisha Chama Cha Mapmduzi kusafisha uongozi wake kwa kuhofia kuwa bila kufanya hivyo kitashindwa katika uchaguzi ujao.

Lakini bado sijakiona chama makini cha upinzani; wala,dalili zozote za kuondoa kansa ya uongozi ndani ya CCM. Bila upinzani mzuri wa nje, na bila demokrasia halisi ndani ya Chama Cha Mapinduzi, Chama hili kitazidi kudidimia chini ya uzito wa uongozi mbovu. Kwa hali yetu ya kisiasa ilivyo nchini, hili si jambo la kutarajia bila ya hofu na wasi wasi!..."

"...Viongozi wetu hivi sasa wanaogopa kutumia nguvu za hoja ili kutoa maamuzi muhimu. Kwa sasa wanatumia hila zaidi kuliko hoja; vitisho kwao ni mbinu rahisi zaidi kuliko adha yakutumia akili na kupata hoja safi ya kumjibu mpinzani katika mjadala. Viongozi hawa wakipewa nafasi watatumia hoja ya nguvu tu; na hawatakuwa na haja ya kutumia akili. Kichini chini baadhi yao tayari wameanza kutumia hoja ya vitisho. Na kama tukiacha utamaduni wa woga ukazagaa tutakuwa tunakaribisha udikteta..."


CHADEMA MMESIKIA MANENO YA BABA WA TAIFA LA TANGANYIKA?

BABA WA TAIFA LA ZANZIBAR NI MOHAMED SHAMTE 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom