Chama legelege, serikali legelege na wanachi wake hoi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chama legelege, serikali legelege na wanachi wake hoi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mghaka, Jul 15, 2011.

 1. M

  Mghaka JF-Expert Member

  #1
  Jul 15, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 320
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Ukifurahia kusaidiwa na kutatuliwa matatizo na jirani yako , rafiki yako au mtu mwingine yeyote ujiandae kupokea majukumu ya kulinda masilahi yake. Hakuna bure duniani, na hakuna msaada ambao hutolewa bila kutegemea kupata matokeo ya kuneemeka kwa mtoaji msaada. Tuanze kwa kuangalia mifano hii ya misaada midogo kabisa ya ambayo pengine mtoaji hutoa kwa sababu anaziaada mfukonni, wako watu husaidia masikini barabarani sii kwa sababu wanapenda au wanaziada ya fedha bali wanatekeleza maagizo ya Mungu kujiandalia makaazi mema muda muafika ukifika yaani pale ambapo roho zao zitakuwa zimetwaliwa. Kwa hivyo huu si msaada bali watoaji hujaribu kujiandalia maisha yao baada ya kifo kwa kuonekana na wao kudhani wanatenda haki mbele za Mungu kwa njia ya kusaidia Maskini kama vitabu vitakatifu vinavyosema na kutuagiza kuwa ukila na maskini umekula na Mungu.


  Vilevile ukisaidia ndugu yako unataka utambuliwe na familia au ukoo kuwa unajali wenzako na kwamba siku hazifanani leo wewe kesho wao na kwa hiyo unafanya hivyo kwa kujiwekea bima ya kijamii katika mazingira ya mbele usiyoyajua, maelezo haya yanagusa michango ya haruai, misiba na kukopeshana kuwa sote tunafanya hivyo kwa sababu yakitufika wakati wetu na kwa jambo tusilolijua jamii inayotuzunguka isituache pweke itukimbilie


  Misaada hii imefanya watu, familia na serikali nyingi duniani kujisahau, hata pale wanapoweza, husubiri sauti ya wajomba ya kuwasaidia. Serikali hazikusanyi kodi kwa sababu zinajua kuwa kwa kuwapigia magoti wajomba zetu hawatatuache tufe na shida zetu, tukipata chetu tunakifuja kwa sababu tunajua kwa kujifunika bendera zao tutakuwa tumefanya kazi ya kuwatangaza na kueneza utamaduni wao na kwa hiyo hawatatuacha tufe na njaa.


  Tunashindwa kukusanya kodi zetu, hatuwezi kujitegemea, hatuwezi kuthubutu kulipia gharama za kupanua vyanzo vipya vya umeme mpaka tuende kuwapigia magoti. Niliwahi kujisikia utanzania na kwa kiburi nikatembea kifua mbel;e siku moja pale Mkapa aliposema kwa jeuri sana wakati akiwahakikishia watanzania ujenzi wa daraja la Mkapa kwamba kwa msaada au kwa uwezo wetu daraja hilo lazima lijengwe. Hii ndio kauli ya kiongozi hata kama alikuwa na mapungufu lakini kuna wakati alituongoza kama kiongozi.


  Leo hii tumeshindwa kutekeleza mambo makubwa yanayotugusa kiuchumi kijamii na hata kiutamaduni. Umeme hatuna, viwanda vinafanya kazi kwa muda mfupi, jana tumeanza kusikia watanzania wanaanza kusitaafishwa ili kubana matumizi, mapato ya serikali yanapungua huduma zitaanza kudoda hakuna anayesema ni lazima niwaokoe watanzania kwa hili hata kama inamaanisha nitafanya makosa katika uamuzi, hapa ndipo Lowasa anasema lazima tufanye maamuzi magumu na tusijikinge na kuishi kwenye blanketi lakuogopa kufanya maamuzi kwa kukwepa kukosea huo si uongozi, uongozi ni ushujaa na uhodari wa kusimamia maamuzi magumu na kuyatetea.

  Ni lazima viongozi wafanye maamuzi magumu na wakishindwa lazima tuwalazimishe wafanye hivyo, bajeti ibomolewe umeme upatikane kesho (kwa haraka) matumizi mengine yasiyo yalazima yasitishwe. Viongozi waanze kujitolea, wabunge wajitolea na sisi wananchi tutajitolea. Hoja hii lazima izungumzwe na Rais wetu, asiachie mtu mwingine aongoze kuhamamisha watanzania kujifunga mikanda ili umeme upatikane.


  Watanzanaia tumewaacha viongozi wakajiachia mpaka tumefikia mahali watoto wetu wa kiume wanatembea ****** nje, wakinadi chupi zao mbele ya mama zao, dada zao, shangazi zao, wakwe zao, wadogo zao na mbele ya serikali yenyewe. Je ni nani mlinzi wa ustaarabu wa Watanzania kama siyo serikali, na hili nalo ni gumu hata kulitolea mwongozo au kauli, wazazi wenzangu mumekuwa hoi hata hamuwezi kulisemea katika ngazi ya kaya.

  Nasikia kichefuchefu kuona mambo makubwa yanatushinda na mambo madogo nayo tabu kuyashughulikia ni uhuru gani wa kutembea uchi, ni uhuru gani wa kubuguzi watu wengine, ni uhuru gani usio na mipaka? ikumbukwe kuwa mavazi ni chaguo la mvaaji na hata namna ya uvaaji lakini usiwe kero kwa mtu mwingine, siku hizi huwezi ukaongozana na mama mkwe, binti yako au mtu mwingine ambaye mahusiano yenu yana mwiko wa kushuhudia aibu ya maumbile ya mwanadamu mwingine kwa sababu tu hayajasetiliwa vizuri. Tunaimba nyimbo za kuwatukuza wakubwa mpaka kunakili mambo ya fedheha. Tuilazimishe Serikali yetu isimamie hili. Ni ajabu viongozi wa kesho wanatembea uchi leo barabarani.

  Tuepuke kuwa legelege pale ambapo hatustahili kuwa legelege, chama kiepuke kuwa legelege kwa kutoa miongozi kwa serikali yake wananchi tusiwe legelege kwa kuiwajibisha serikali yetu na bunge letu lichukue maamuzi sahihi.


  Kazi kweli kweli
  Viva mapambano, viva kujitegema na viva ustarabu wa Watanzania.

  Aluta continua
   
Loading...