Chama langu Simba hatari inakuja tuchukue tahadhari

Nimekaa mara fikra za woga zimenijia. Nahofia timu yangu Lunyasi wa Msimbazi kuaga mapema kwenye michuano ya CCL. Naomba iwe ni ndoto tu

Kumbuka kwenye mchezo wao wa kwanza wa raundi ya kwanza walitoka sare ya bila kufungana AS SONGO ya Msumbiji

Ndugu zangu sare ya bilakufungana ugenini ni hatari sana. Unatembea kwenye uzi mwembaamba sana baina ya kusongambele na kutupwa nje ya mashindano.

Hapo hakuna alternative kwa Simba zaidi ya ushindi. Afadhali ile sare waliotoka watani zetu wa Jangwani na Township Rollers, sare ya bao moja kwa moja. Kama Yanga wakikaza ugenini wakatoka angalau sare ya bao mbili kwa mbili au zaidi wanafuzu kwa raundi inayofuata

Msimbazi akitoa sare ya magoli ya aina yoyote anaaga mashindano, suluhu ya bilabila ni changamoto ya mikwaju ya penati ambayo sikuzote haina mwenyewe!

Tuliidharau timu hii ya Mozambique lakini siku zote Msumbiji hua inatusumbua sana iwe kwa ngazi ya vilabu na hata timu ya Taifa. Wana style yao ya kufunga goli dakika tano za mwanzo na likang'ang'ania hadi mpira unaisha

Natoa wito kwa viongozi na hasa benchi la ufundi wasiwachukulie poa hawa jamaa

Waache kabisa tabia yao ya kufanya majaribio ya wachezaji na aina ya uchezaji, tabia ambayo kocha wetu Patric anayo sana. Waweke kikosi cha kazi isitukute aibu tukakosa pa kuweka sura zetu

Sisi mashabiki panapo majaaliwa tutakuwepo uwanja wa Taifa kutoa sapoti inayohitajika kama kawaida yetu

SIMBA NGUVU MOJA
Naona utabiri wako umetimia
 
mpira hauchezwi mdomoni haya hao Songo mmewapiga hiyo week??? Mtoa mada alikua sahihi kabisa alikosea tuu kwenye hiyo yanga akitoka 0-0 ugenini na amekiri kukosea ila bado mkajifanya vichwa ngumu
Hivi una kumbuka mara ya mwisho lini Simba kufungwa uwanja wa Taifa? Wamekuja wababe wa Egypt, Congo, Algeria, Zambia etc ila wote walisanda. Hao Songo pona yao ni kupigwa viwili ila wakizubaa ata week wanaweza pigwa.
 
Nimekaa mara fikra za woga zimenijia. Nahofia timu yangu Lunyasi wa Msimbazi kuaga mapema kwenye michuano ya CCL. Naomba iwe ni ndoto tu

Kumbuka kwenye mchezo wao wa kwanza wa raundi ya kwanza walitoka sare ya bila kufungana AS SONGO ya Msumbiji

Ndugu zangu sare ya bilakufungana ugenini ni hatari sana. Unatembea kwenye uzi mwembaamba sana baina ya kusongambele na kutupwa nje ya mashindano.

Hapo hakuna alternative kwa Simba zaidi ya ushindi. Afadhali ile sare waliotoka watani zetu wa Jangwani na Township Rollers, sare ya bao moja kwa moja. Kama Yanga wakikaza ugenini wakatoka angalau sare ya bao mbili kwa mbili au zaidi wanafuzu kwa raundi inayofuata

Msimbazi akitoa sare ya magoli ya aina yoyote anaaga mashindano, suluhu ya bilabila ni changamoto ya mikwaju ya penati ambayo sikuzote haina mwenyewe!

Tuliidharau timu hii ya Mozambique lakini siku zote Msumbiji hua inatusumbua sana iwe kwa ngazi ya vilabu na hata timu ya Taifa. Wana style yao ya kufunga goli dakika tano za mwanzo na likang'ang'ania hadi mpira unaisha

Natoa wito kwa viongozi na hasa benchi la ufundi wasiwachukulie poa hawa jamaa

Waache kabisa tabia yao ya kufanya majaribio ya wachezaji na aina ya uchezaji, tabia ambayo kocha wetu Patric anayo sana. Waweke kikosi cha kazi isitukute aibu tukakosa pa kuweka sura zetu

Sisi mashabiki panapo majaaliwa tutakuwepo uwanja wa Taifa kutoa sapoti inayohitajika kama kawaida yetu

SIMBA NGUVU MOJA
Uliona mbali
 
Back
Top Bottom