Mc Tilly Chizenga
JF-Expert Member
- Feb 7, 2012
- 4,641
- 3,675
Mzee, umeongea maneno meeengi,wewe huwezi kumpangia kocha, simple toa kikosi unachoamini ni cha ushindani,unazunguka sana Mkuu,unashindwa nini kuweka list unayoamini ndio ya kimashindano na sio ya kimajaribio kama unavyotahadharisha?Mwaga kikosi hapa, hivyo vya Mehala fungia kabatini kwako viendelee kupigwa vumbi.hata hivyo umetoa vidokezo vinavyoashiria wewe ni Shabiki LA Simba kweli na sio Kwasukwasu hongera kwa hilo.Sasa tiririka kikosi unachodhani hiko kitamrarua MTU mithili ya Mnyama Simba poriniM
Mkuu naweza kukupangia vikosi vya Simba tangia kile kilichocheza na Mehla Al Kubra ya Misri 1974, Kilichoitoa The Mighty Mufulira Wanderers 1979, kilicheza na Union Spotive Duala na kupoteza goli nne taifa mwaka 1980, kilichotaka kushuka daraja tukaifunga Yanga taifa 1986, kilichocheza tangia mechi ya mwanzo na Ferreviario de Nampula ya Msumbiji 1993 na kuendelea hadi kuingia fainali ya kombe la Abiola kabda ya kupoteza kwenye fainali mna Stella Abijan, kikosi kilichocheza Ccl makundi 2003 na vyoote hadi cha juzi kilichotambulishwa kwa Mkapa
Lakini nasisitiza kazi ya kupanga kikosi sio yangu ni ya kocha ila akitupangia hivyo tutamlaumu
Jambo la mwisho nikwambie mapenzi yako kwa Simba hayajafikia ya kwangu kwa chama hilo, pengine kabda hujazaliwa