Chama langu Simba hatari inakuja tuchukue tahadhari

Nimekaa mara fikra za woga zimenijia. Nahofia timu yangu Lunyasi wa Msimbazi kuaga mapema kwenye michuano ya CCL. Naomba iwe ni ndoto tu

Kumbuka kwenye mchezo wao wa kwanza wa raundi ya kwanza walitoka sare ya bila kufungana AS SONGO ya Msumbiji

Ndugu zangu sare ya bilakufungana ugenini ni hatari sana. Unatembea kwenye uzi mwembaamba sana baina ya kusongambele na kutupwa nje ya mashindano.

Hapo hakuna alternative kwa Simba zaidi ya ushindi. Afadhali ile sare waliotoka watani zetu wa Jangwani na Township Rollers, sare ya bao moja kwa moja. Kama Yanga wakikaza ugenini wakatoka suluhu ya kutofungana wanafuzu kwa raundi inayofuata

Msimbazi akitoa sare ya magoli ya aina yoyote anaaga mashindano, suluhu ya bilabila ni changamoto ya mikwaju ya penati ambayo sikuzote haina mwenyewe!

Tuliidharau timu hii ya Mozambique lakini siku zote Msumbiji hua inatusumbua sana iwe kwa ngazi ya vilabu na hata timu ya Taifa. Wana style yao ya kufunga goli dakika tano za mwanzo na likang'ang'ania hadi mpira unaisha

Natoa wito kwa viongozi na hasa benchi la ufundi wasiwachukulie poa hawa jamaa

Waache kabisa tabia yao ya kufanya majaribio ya wachezaji na aina ya uchezaji, tabia ambayo kocha wetu Patric anayo sana. Waweke kikosi cha kazi isitukute aibu tukakosa pa kuweka sura zetu

Sisi mashabiki panapo majaaliwa tutakuwepo uwanja wa Taifa kutoa sapoti inayohitajika kama kawaida yetu

SIMBA NGUVU MOJA
Hivi una kumbuka mara ya mwisho lini Simba kufungwa uwanja wa Taifa? Wamekuja wababe wa Egypt, Congo, Algeria, Zambia etc ila wote walisanda. Hao Songo pona yao ni kupigwa viwili ila wakizubaa ata week wanaweza pigwa.
 
Samahani kwa usumbufu mkuu, nilighafilika hapo

Mimi ni moja kati ya mashabiki wa mpira kuwahi kutokea hapa nchini,ila hapo nilipitiwa kidogo so sorry
Hakuna shida Mzee, Ila kukusaidia ile sare ya simba kwa ugenini ni afadhal zaid kuliko draw ya Yanga Nyumaban... Siku zote mechi za mtoano ukishindwa kutake advantage ya uwanja wako wa Nyumban kutolewa ni rahis sana.

Simba Msimu ulipita wa Champions League

Alimfunga Nkana taifa akafuzu hatua ya makundi
Alimfunga Vita mech ya mwisho taifa akafuzu robo fainali
Alidraw Home na Mazembe akaenda kutolewa Congo.

NB. Simba alishinda Mechi zake zote alizocheza Uwanja wa Taifa kwenye hatua ya Makundi.
 
M

Mwaka 2003 Simba ilipocheza hatua ya makundi kwa mara ya kwanza CCL alikua ametoka kukutana na mazingira kama hayo kwenye hatua za awali.

Ilitoka 0-0 kwenye Uwanja wa Taifa Shamba la bibi na Santos waliokua mabingwa wa South Africa na katika mechi ya marudiano iliyofanyika kule Bondeni wakatoka sare ya 1-1 na hivyo Simba ikafuzu kwa faida ya goli la ugenini

Mazingira hayo ndio yananifanya niwe na hofu pamoja na tabia ya timu zetu kudharau baadhi ya timu hasa za Msumbiji ambazo kiuhalisia mpira wao na wetu haupishani sana na huwenda wakawa juu zaidi yetu
 
Yanga wakikaza ugenini wakatoka suluhu ya kutofungana wanafuzu kwa raundi inayofuata

Nilikosea hapo mkuu ila nimesharekebisha. Hoja yangu ilikua Si.ba wasidhani wapo kwenye nafasi nzuri sana maana wao wanahitaji ushindi wa aina yoyote kwani sare ya magoli itamaanisha kuyaaga mashindano
 
Simba tuko vizuri zaidi tukiwa nyumbani kwa mchina/mkapa, vyuraaaaaazzz hawatatoboi ugenini
 
Hivi una kumbuka mara ya mwisho lini Simba kufungwa uwanja wa Taifa? Wamekuja wababe wa Egypt, Congo, Algeria, Zambia etc ila wote walisanda. Hao Songo pona yao ni kupigwa viwili ila wakizubaa ata week wanaweza pigwa.
Huo ndio wasiwasi mkubwa. Simba tumejenga kujiamini kupita kiasi bila kuweka tahadhari kua tunacheza na mabingwa wa nchi nyingine
 
Huo ndio wasiwasi mkubwa. Simba tumejenga kujiamini kupita kiasi bila kuweka tahadhari kua tunacheza na mabingwa wa nchi nyingine
Sio tuu kujiamini kwa Mkapa sio mahali salama,ukiangalie ile timu wakati ipo tuu kwao walikua hawajiamini, mashabiki wa Simba walikua wachache walikua na mzuka kuliko hata mashabiki wao, Cha pili wale jamaa hawana mfungaji simba ile mechi Kuna kipindi walikua Wana relax Kama wanacheza na mbao tuu kwakua wale jamaa walikua hawana madhara langoni kwa Mnyama,kikubwa kufungwa wale lazima hawawezi kuimiri presha ya pale kwa Mkapa.... Mashabiki wa Simba tusizarau hii mechi tujitokeze kwa wingi uwanjani
 
N

Natamani san na naombea iwe hivyo mkuu
 
Hivi unajua maana ya advantage?mbona unakuwa mbishi na hutaki kujifunza kwa waliokuelezea hapo juu
Ni kweli kabisa kwa maneno mengine ile sare ya hapa Taifa ni advantage kwa Yanga wakati Simba tuna mtihani mkubwa
 
Back
Top Bottom