Chama langu Simba hatari inakuja tuchukue tahadhari

Sesten Zakazaka

JF-Expert Member
Sep 10, 2017
10,561
19,054
Nimekaa mara fikra za woga zimenijia. Nahofia timu yangu Lunyasi wa Msimbazi kuaga mapema kwenye michuano ya CCL. Naomba iwe ni ndoto tu

Kumbuka kwenye mchezo wao wa kwanza wa raundi ya kwanza walitoka sare ya bila kufungana AS SONGO ya Msumbiji

Ndugu zangu sare ya bilakufungana ugenini ni hatari sana. Unatembea kwenye uzi mwembaamba sana baina ya kusongambele na kutupwa nje ya mashindano.

Hapo hakuna alternative kwa Simba zaidi ya ushindi. Afadhali ile sare waliotoka watani zetu wa Jangwani na Township Rollers, sare ya bao moja kwa moja. Kama Yanga wakikaza ugenini wakatoka angalau sare ya bao mbili kwa mbili au zaidi wanafuzu kwa raundi inayofuata

Msimbazi akitoa sare ya magoli ya aina yoyote anaaga mashindano, suluhu ya bilabila ni changamoto ya mikwaju ya penati ambayo sikuzote haina mwenyewe!

Tuliidharau timu hii ya Mozambique lakini siku zote Msumbiji hua inatusumbua sana iwe kwa ngazi ya vilabu na hata timu ya Taifa. Wana style yao ya kufunga goli dakika tano za mwanzo na likang'ang'ania hadi mpira unaisha

Natoa wito kwa viongozi na hasa benchi la ufundi wasiwachukulie poa hawa jamaa

Waache kabisa tabia yao ya kufanya majaribio ya wachezaji na aina ya uchezaji, tabia ambayo kocha wetu Patric anayo sana. Waweke kikosi cha kazi isitukute aibu tukakosa pa kuweka sura zetu

Sisi mashabiki panapo majaaliwa tutakuwepo uwanja wa Taifa kutoa sapoti inayohitajika kama kawaida yetu

SIMBA NGUVU MOJA
 
Nimekaa mara fikra za woga zimenijia. Nahofia timu yangu Lunyasi wa Msimbazi kuaga mapema kwenye michuano ya CCL. Naomba iwe ni ndoto tu

Kumbuka kwenye mchezo wao wa kwanza wa raundi ya kwanza walitoka sare ya bila kufungana AS SONGO ya Msumbiji

Ndugu zangu sare ya bilakufungana ugenini ni hatari sana. Unatembea kwenye uzi mwembaamba sana baina ya kusongambele na kutupwa nje ya mashindano.

Hapo hakuna alternative kwa Simba zaidi ya ushindi. Afadhali ile sare waliotoka watani zetu wa Jangwani na Township Rollers, sare ya bao moja kwa moja. Kama Yanga wakikaza ugenini wakatoka suluhu ya kutofungana wanafuzu kwa raundi inayofuata

Msimbazi akitoa sare ya magoli ya aina yoyote anaaga mashindano, suluhu ya bilabila ni changamoto ya mikwaju ya penati ambayo sikuzote haina mwenyewe!

Tuliidharau timu hii ya Mozambique lakini siku zote Msumbiji hua inatusumbua sana iwe kwa ngazi ya vilabu na hata timu ya Taifa. Wana style yao ya kufunga goli dakika tano za mwanzo na likang'ang'ania hadi mpira unaisha

Natoa wito kwa viongozi na hasa benchi la ufundi wasiwachukulie poa hawa jamaa

Waache kabisa tabia yao ya kufanya majaribio ya wachezaji na aina ya uchezaji, tabia ambayo kocha wetu Patric anayo sana. Waweke kikosi cha kazi isitukute aibu tukakosa pa kuweka sura zetu

Sisi mashabiki panapo majaaliwa tutakuwepo uwanja wa Taifa kutoa sapoti inayohitajika kama kawaida yetu

SIMBA NGUVU MOJA
Yani wewe ndo kenge uliyezeeka kabisa...kama hujui kitu uliza au kaa kimya
 
Hapo hakuna alternative kwa Simba zaidi ya ushindi. Afadhali ile sare waliotoka watani zetu wa Jangwani na Township Rollers, sare ya bao moja kwa moja. Kama Yanga wakikaza ugenini wakatoka suluhu ya kutofungana wanafuzu kwa raundi inayofuata
Samahan Mkuu unaujua vizur Mpira au unasimuliwa? Unasema Yanga akitoka suluhu kutofungana anafuzu huku umeandika
Msimbazi akitoa sare ya magoli ya aina yoyote anaaga mashindano, suluhu ya bilabila ni changamoto ya mikwaju ya penati ambayo sikuzote haina mwenyewe!

Which is which?
 
27 Reactions
Reply
Back
Top Bottom