Chama kipi kimefaidi zaidi kisiasa na Muungano wa UKAWA?

mwongozo junior

Senior Member
Jul 28, 2015
180
64
Wanajukwaa habari zenu

Siyo vibaya tukajadili muungano Wa ukawa baada ya uchaguzi. Najua kuna malakamiko mengi kuhusu kura Nk... lakini naomba tuchukulie /tukubali kuwa matokeo yalishatangazwa na tume na mlango umefungwa. Tufikirie mipango ya 2020.

Je chama kipi cha ukawa kimefaidi zaidi KISIASA kuliko vingine?

URAIS
Bila shaka ulikua uamuzi mgumu kwa cuf na nccr (khasa cuf) kukubali kutosimamisha mgombea urais ili kumuachia mgombea Wa ukawa (chdm). Ikumbukwe kuwa mgombea urais huongeza umaarufu Wa chama kwa kuzunguka nchi nzima. Chama kinaposhiriki uchaguzi bila mgombea urais hupunguza umaarufu na nguvu zake. Kura za urais pia huchangia kwenye ongezeko LA ruzuku kutoka serikalini.

Kwa hili LA mgombea urais naona chdm kimefaidi zaidi. Japo ni kura za ukawa lkn kiuhalisia (kwa mujibu Wa NEC) hizo kura milioni 6 plus ni za chadema. Ruzuku ya chadema itaongezeka sana hivyo kusaidia ktk uendeshaji Wa chama.

Je cuf na nccr wanastahiki kila mwezi kupewa asilimia ndogo kwenye hii ruzuku au yote itakua ya chadema? Tujadili. Wasipopewa hudhani kuwa muungano Wa ukawa utayumba? Haitaonekana kuwa chadema ilivitumia nccr, cuf na nld kama ngazi?

Je ujio Wa lowassa ulochangia hizo kura utaijenga chdm baada ya uchaguzi au utaibomoa? Chadema imefaidi kisiasa kwa kumleta lowassa kwenye urais au itaathirika negatively kwa kumleta?

UBUNGE
Nccr ilikua na wabunge 4 bunge lilopita. Kwa uchaguzi huu imepata mbunge 1. Ni neema au nakama? Ukawa imeisaidia nccr au imeingamiza?

Cuf ilikua na wabunge 2 (kutoka bara) bunge lilopita. Sasa hivi imepata wabunge 10 bara. hili ni ongezeko la zaidi ya 90%. In neema au hasara?

Chadema iilikua na wabunge 25 bunge lilopita. Sasa hivi ina 34. Ongezeko LA chini ya asilimia 20. Je ni neema au hasara kwa chadema?

Naomba tujadili. Kama nimekoseya kwenye idadi ya wabunge napokea masahihisho.
 
Hapa nccr ndio imeathirika zaidi na sababu ziko wazi walianzisha mgogoro wa ndani wakati wa kampeni badala ya kutetea chama chao sasa watajifunza cuf wamenufaika zaidi hilo hata mtatilo kalizungumzia wazi japo zilikuwepo kasoro ndogo
 
CUF imefaidi mno.Haijatumia Pesa kwa sababu haikumchangia Lowasa kwenye kampeni zake.Hakijatumia hela kimedandia lift ya bure kwenye pesa na umaarufu wa Lowasa wakajipatia bure majimbo kupitia mgongo wa lowasa bure.Majimbo kama ubungo na kinondoni Chadema Ina NGUVU ikawagawia CUF WAKAJISHINDIA kwa lift ya mgongo wa Lowassa.

CUF imevuna sana wabunge kwa mgongo wa Lowasa WA chadema wakati kwenye pesa wala hawakuchangia.Ina maana CHADEMA imetumia raslimali zake na mgombea wao Lowasa kuwapa majimbo mengi bara.Wakati UKIENDA zanzibar CUF hawajaisaidia CHADEMA walau kupata majimbo mengi.

CUF imefaidi mno kuliko vyama vyote vya UKAWA wakati walikuwa bahili wa kutupwa kuchangia kampeni za mgombea Uraisi na mwenza wake mzanzibari Duni HAJI.CHADEMA imenyonywa sana na wazanzibari wa CUF kwenye huu uchaguzi.Hata HAFLA ya kuchangia kampeni ya uraisi aliyoitisha Lowasa WACHANGIAJI WALIKUWA WATU WA BARA HAKUWEPO MPEMBA HATA MMOJA wakati tunajua wapemba wana pesa.

Kwa hali niliyoiona CHADEMA wana haki kudai MUUNGANO uvunjike wamenyonywa hadi wamekoma.Na ruzuku CUF hawatawagawia NG`O.
 
Chadema walikuwa na wabunge 23 sasa watafika mpaka 36ongezeko la zaidi ya wabunge 13 hapa kuna kura za Urais million 6 chadema haijawahi kushuka idadi ya wabunge toka imeanzishwa,kiufupi chadema graph yao haijawahi shuka ni kupanda tu huwezi sema wameshindwa hata kama uwekezaji ulikuwa vipi wamefanya vizuri CUF nao kutoka wabunge 2 mpaka kumi ongezeko la wabunge nane nao wamejitahidi kasoro NCCR NA NLD WAMESHUKA SABABU YA ULE UJINGA WA WALE VIONGOZI WA JUU WA CHAMA AMBAO BADALA YA KUPAMBANA WAKAANZA UJINGA MM NAWAPONGEZA UKAWA N.A. HII FIMBO AMBAYO CCM LAZIMA ITAWAUMA TU MAANA WATACHAPWA NAYO MPAKA WAKOME HONGERENI UKAWA JENGENI MAJIMBO YENU YAWE MFANO KWA MAJIMBO MENGINE
 
CUF imefaidi mno.Haijatumia Pesa kwa sababu haikumchangia Lowasa kwenye kampeni zake.Hakijatumia hela kimedandia lift ya bure kwenye pesa na umaarufu wa Lowasa wakajipatia bure majimbo kupitia mgongo wa lowasa bure.Majimbo kama ubungo na kinondoni Chadema Ina NGUVU ikawagawia CUF WAKAJISHINDIA kwa lift ya mgongo wa Lowassa.

CUF imevuna sana wabunge kwa mgongo wa Lowasa WA chadema wakati kwenye pesa wala hawakuchangia.Ina maana CHADEMA imetumia raslimali zake na mgombea wao Lowasa kuwapa majimbo mengi bara.Wakati UKIENDA zanzibar CUF hawajaisaidia CHADEMA walau kupata majimbo mengi.

CUF imefaidi mno kuliko vyama vyote vya UKAWA wakati walikuwa bahili wa kutupwa kuchangia kampeni za mgombea Uraisi na mwenza wake mzanzibari Duni HAJI.CHADEMA imenyonywa sana na wazanzibari wa CUF kwenye huu uchaguzi.Hata HAFLA ya kuchangia kampeni ya uraisi aliyoitisha Lowasa WACHANGIAJI WALIKUWA WATU WA BARA HAKUWEPO MPEMBA HATA MMOJA wakati tunajua wapemba wana pesa.

Kwa hali niliyoiona CHADEMA wana haki kudai MUUNGANO uvunjike wamenyonywa hadi wamekoma.Na ruzuku CUF hawatawagawia NG`O.

mentality hizi ni mbegu mbaya
cuf wamefaidi kwa kupata wabunge 10 tu bara
wakati waliowasimamisha hawakufika hata 30
chadema ilipewa nafasi zaidi ya 75
what if wangeshinda nafasi 50?
kuna wabunge wa chadema mtwara lindi huko ambako CUF pia ina nguvu
 
Back
Top Bottom