Chama kinaruhusiwa kuteua mgombea mpya baada ya aliyeteuliwa awali kuenguliwa na NEC? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chama kinaruhusiwa kuteua mgombea mpya baada ya aliyeteuliwa awali kuenguliwa na NEC?

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Keil, Sep 1, 2010.

 1. K

  Keil JF-Expert Member

  #1
  Sep 1, 2010
  Joined: Jul 2, 2007
  Messages: 2,214
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Baada ya kusoma habari hii: NEC sasa kuengua CCM kwenye Gazeti la Raia Mwema nimepata mshituko kidogo. Kwa wale ambao ni wajuzi wa Sheria labda wanaweza kutusaidia kutuelewesha.

  Kwenye habari hiyo Mzee Kinana anasema kwamba:

  Kama deadline ya kuchukua na kurejesha fomu za kugombea kutoka ofisi za NEC imeishapita, hao wagombea wapya wa CCM wataingizwaje kwenye uchaguzi?

  Ina maana vyama vya upinzani huwa havina uwezo wa kuteua wagombea wapya ili kujaza nafasi ya mgombea aliyeenguliwa?

  Sheria ya Uchaguzi inasemaje iwapo mgombea akiwekewa pingamizi na likakubaliwa, je, chama chake kinaruhusiwa kuteua mgombea mwingine?
   
 2. M

  Mwafrika JF-Expert Member

  #2
  Sep 1, 2010
  Joined: Nov 20, 2006
  Messages: 5,490
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  hapa ndipo watajichanganya hadi wachoke.

  wale wabunge kumi waliopita bila kupingwa (kwa kuondoa wapinzani wao kwa mapingamizi) wameanza kuonja joto la jiwe.
   
 3. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #3
  Sep 1, 2010
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  mhhhh
   
 4. K

  Keil JF-Expert Member

  #4
  Sep 1, 2010
  Joined: Jul 2, 2007
  Messages: 2,214
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Mkuu wangu Mwafrika,

  Nyani huwa haoni kundule (samahani kwa Mheshimiwa NN) ... angalia huyu Mzee Kinana kwenye habari nyingine anasema kwamba watu wanakimbilia kuweka mapingamizi na ilihali mabingwa wa kuweka mapingamizi ni CCM. Ila kwa kuwa JK kawekewa pingamizi, tayari anaona kwamba siasa za mapingamizi hazifai.

  .... eti kashfa za kuzusha, kama ni za kushusha si waliozushiwa waende mahakamani ili wakapewe haki yao, wanasubiri nini?

  .... eti wanahangaika kuweka pingamizi, mbona wabunge wa CCM walipokuwa wakiweka pingamizi sikumsikia akisema waende kupiga kampeni badala ya kusaka ushindi wa mezani.

  .... eti wanakimbilia kuitisha press conference, jamani Makamba ndio alikuwa wa kwanza kuitisha press conference kwamba CHADEMA wametumia lugha ya matusi, baada ya hiyo press conference ndipo Prof. Baregu alipoitisha ya kwake kujibu hoja za Makamba.

  Kinachofanywa na CCM ni sawa, lakini vyama vingine vikifanya hivyo ni makosa. Kaazi kweli kweli!

  Pingamizi la CHADEMA limewaweka pabaya, maana hawajui Tendwa atasema nini na pia hawajui maamuzi ya Tendwa kama yatakubaliwa na CHADEMA na pia hawajui next move ya CHADEMA kama itakuwa ni mahakamani au watakaa kimya.
   
 5. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #5
  Sep 1, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Kuna sheria zingine za NEC ni za kufurahisha kama si kusikitisha eti mgombea mwenye sifa zote anaenguliwa kwa kukosea tarehe ya kuzaliwa, kwa nini asiambiwe arekebishe. Au kwa nini wasipewe second chance kama watu wengine wanavyopewa kujisahihisha.

  Mfano mtu kaandika kazaliwa tarehe 18/08/2010 anaenguliwa, hivi anayepokea fomu na kuona hilo kosa kwa nini asitumie busara za kibinadamu, mimi sioni kama kosa hilo ni kubwa kiasi cha kumwengua mtu. Mgombea kama huyo adhabu yake iwe ni kusafiri kwenda mwenyewe ofisi za NEC Dar na kurekebisha na si kuenguliwa. Tutakuwa tunaacha wagombea wazuri kwa vijisababu vya kijinga.

  Makosa kama kutiwa hatiani na mahakama au kutolipa kodi au uraia hayo ndiyo yanaweza kupelekea kukosa sifa lakini si kukosea jina au kusahau kuweka sahihi. Sometimes NEC wajifunze kuwa tolerant kwa vile wana dill na binadamu wanaoweza kukosea, hata wao NEC they are not 100% perfect.
   
 6. m

  mwita ke mwita JF-Expert Member

  #6
  Sep 1, 2010
  Joined: Aug 13, 2010
  Messages: 5,491
  Likes Received: 1,220
  Trophy Points: 280
  anayejua masuala ya sheria za uchaguzi atueleze wadau kwani hata mimi nimepigwa na bumbuazi
   
 7. K

  Keil JF-Expert Member

  #7
  Sep 2, 2010
  Joined: Jul 2, 2007
  Messages: 2,214
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Mkuu Luteni,

  Makosa madogo madogo kama ya kukosea tarehe ya kuzaliwa, nakubali kwamba ni uzembe wa mgombea lakini pia ni uzembe wa msimamizi wa uchaguzi. Kiutaratibu, kabla fomu ya mgombea haijapokelewa lazima huwa inakaguliwa kama imejazwa vyema na kama kuna makosa, mhusika huambiwa hapo hapo. Makosa hayo ya kukosea tarehe ya kuzaliwa ni minor na inawezekana sababu ya pressure mtu anaweza kukosea. Kama ulivyosema, kumuengua is not fair, apewe nafasi ya kurekebisha badala ya kubaka demokrasia kwa kututangazia ushindi wa bila kupingwa.

  Kwenye mapingamizi haya kuna kitu kingine nina mashaka nacho. Mfano, mgombea X atajuaje kwamba wadhamini wa mgombea Y majina yao hayako kwenye daftari la kudumu la wapiga kura? Ina maana mgombea X anajua majina yote yaliyo kwenye hilo daftari? Hapa pananitatiza sana.

  Wagombea wengi akishamuuliza mdhamini kama shahada ya kupigia kura na akakubali, sidhani kama ana muda wa ku-verify kwamba shahada hiyo imeandikishwa kwenye daftari la kudumu la wapiga kura. Kutengua uteuzi wa mgombea aliyedhamiwa na wadhamini ambao shahada zao hazijaandikishwa kwenye daftari la kudumu, ni kuwaonea.
   
 8. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #8
  Sep 2, 2010
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Yaani Tanzania ni zaidi ya uijuavyo!
   
 9. J

  Jibaba Bonge JF-Expert Member

  #9
  Sep 2, 2010
  Joined: May 6, 2008
  Messages: 1,224
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Ni upumbavu mkubwa sana kumuondoa mgombea eti tu kwa sababu amekosea kujaza fomu. it is high time sasa NEC waliangalie upya hili. Watofautishe sifa za mgombea na ujazaji wa fomu. Kukosea kujaza fomu hakumuondelea sifa mgombea kwa sababu makosa ya kujaza fomu yanarekebishika. Lakini mgombea akikosa sifa , kwa mfano alishawahi kufungwa kwa muda unoelekezwa kwenye sheria, si raia, hajafikisha umri wa kugombea kwa mujibu wa sheria n.k. hayarekebishiki hivyo mgombea anaweza kuenguliwa. NEC liangalieni upya hili.
   
 10. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #10
  Sep 2, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Mbona NEC haikuwapa Chadema kuweka mgombea mbadala katika uchaguzi mdogo wa Mbeya Vijijini mwaka juzi baada ya yule wa awali alipoenguliwa na Tume hiyo kutokana na pingamizi la CUF?
   
 11. kilemi

  kilemi JF-Expert Member

  #11
  Sep 2, 2010
  Joined: Mar 13, 2009
  Messages: 520
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Subiri uangalie ile kashfa ya chenge kutolipa ushuru na bima ya gari! Unafikiri ataenguliwa?
   
 12. N-handsome

  N-handsome JF-Expert Member

  #12
  Sep 2, 2010
  Joined: Jan 23, 2008
  Messages: 2,317
  Likes Received: 128
  Trophy Points: 160
  Sheria tete za kumlinda Mtoto wa mama Deep Green
   
 13. kaburunye

  kaburunye JF-Expert Member

  #13
  Sep 2, 2010
  Joined: May 12, 2010
  Messages: 675
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  The boss (CCM) is always right. CCM wanaweza kupindisha sheria yeyote na kumshinikiza hakimu/jaji/NEC/tume ya uchaguzi wakubaliane nao. Wao wana tafasiri yao tofauti ya kila sheria hapa nchini. Ukiwashinda kwa tafasiri halali wanaibuka na ya kwao na kukushinda kwa nguvu. Their days are numbered. We are not fools. Aiseee
   
 14. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #14
  Sep 2, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  wakishaenguliwa wameenguliwa - Pilato
   
 15. Nyunyu

  Nyunyu JF-Expert Member

  #15
  Sep 2, 2010
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 4,370
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  Akienguliwa kwa makosa ambayo yamethibitika sheria ilivujwa ndiyo basi, hivi ndivyo ninavyofahamu. CCM wancheza na media kuvuriga hali ya hewa tu, sometime one can win battle kwa maneno tu! (creating fear to the opponent!)
   
Loading...