Uchaguzi 2020 Chama kinachotaka kuhudumia Watanzania, kinabagua na kuweka nongwa maendeleo yakipelekwa sehemu fulani ya nchi

Ngalikihinja

JF-Expert Member
Sep 1, 2009
21,545
2,000
Kampeni za vyama mbalimbali vya siasa zimeendelea kutimua vumbi maeneo mbalimbali ya nchi yetu. Leo naomba nitoe dukuduku langu kwa uchache sana. Kwa mshtuko sana nimesikitika kuona baadhi ya vyama vya upinzani kuanza ubaguzi wa waziwazi kwa kuumia na kuweka nongwa Serikali kupeleka maendeleo na kutekelezwa kwa miradi mbalimbali ya maendeleo kwenye maeneo fulani ya nchi.

Inashangaza sana lakini ni hatari unapoona mtu anayetaka nafasi kubwa kabisa ya uongozi kwenye nchi kuanza mapema kubagua watu anaotaka kuwaongoza kwa kuweka chuki za hadharani na kuumia eneo fulani la nchi kupelekewa maendeleo.

Kwani Chato iko nchi gani? Sio Tanzania. Sasa kwanini pakipelekwa maendeleo yaliyopelekwa pia sehemu nyingine za nchi mtu ateseke? Kwani Chato hakuna Watanzania mpaka wasipelekewe maendeleo wao?

Kama ni viwanja vya ndege vimejengwa kila mahali nchi nzima. Kama ni barabara kila wilaya na halmashauri kipindi hiki zimepelekewa fedha za miradi ya barabara. Kama ni taa za barabarani zimejaa kila miji nchi nzima. Sasa kwanini ikiwa Chato mtu aumie na kuweka nongwa? Kwani Chato wanaishi Wahutu au Wazuru? Si Watanzania kama Watanzania wowote popote pale nchi nzima?

Hii ni hatari sana kwa mtu tu anayeomba Urais kuanza kugawa watu na kuona kuna watu wanapaswa wapate maendeleo na wengine hawapaswi kupata. Hii ni ishara mbaya sana kwetu Watanzania. Watanzania wote popote walipo wanapaswa na wana haki ya kupata maendeleo. Si dhambi wala uvunjifu wa sheria, ni wajibu kwa kiongozi yeyote yule.

Kwa wana Chato na Watanzania wote nchi nzima hii ituamshe kama bado kuna watu wako usingizini. Hakuna kilichofanyika Chato ambacho hakijafanyika popote pale nchi nzima. Jambo gani lipo Chato na halipo kwengine Tanzania? Lipi?

Narudia tena hii ni hatari na haifai kuungwa mkono. Mwisho ni kwa Watanzania wote, tuwe makini na macho sana na baadhi ya wagombea walio tayali kutumia hila na kila aina ya njia na njama kupata uongozi, walio tayali kutugawa na kutuchonganisha ili wao wapate uongozi. Karma ya kwanza ya kiongozi ni kuunganisha na kuongoza watu kuelekea maendeleo. Sasa unapoona kiongozi anaanza kuwagawa na kuwapasua inahatarisha sana. Twende tukawanyime kura Oktoba 28.
Kwani JPM alipokuwa anahutubiwa akiwa jimboni kwa Bwege, alisemaje!? Na alipokuwa huko Musoma, JPM alisemaje juu ya kunyima maendeleo baadhi ya majimbo.!? Tusiwe na double starndard..
 
emalau

JF-Expert Member
Apr 25, 2009
2,738
2,000
Acha uongo!

*Taja wilaya nyingine nchini yenye kiwanja cha ndege kama cha Chato!
*Taja wilaya nyingine ambayo kunafanyika mpango wa kujenga hospitali kubwa ya rufaa ya kuhudumia kanda nzima!
*Taja wilaya nyingine nchini ambapo kuna mpango wa kujenga uwanja mkubwa wa kimataifa wa mpira wa miguu!

Marais waliotangulia wangeamua wajenge viwanja vijijini kwao nchi hii ingekuwaje?

Kuna miradi kama Barabara, shule, hospitali, maji nk yenye kufanana na hiyo hakuna mtu amestuka wala kuhoji!

Ila miradi inayofanyika Chato ni ya ziada, ni mzigo kwa taifa! Ukiangalia sio kila mkoa nchini una kiwanja chenye hadhi kama ya Chato!

>>Je, kuna uhusiano wowote wa Rais kutokea Chato na miradi hiyo kwenda Chato au ni coincedence tu?
Walilazimisha hata tawi la CRDB lijengwe huko wakati waweka fedha hakuna
 
Subira the princess

JF-Expert Member
Mar 3, 2018
1,699
2,000
Kampeni za vyama mbalimbali vya siasa zimeendelea kutimua vumbi maeneo mbalimbali ya nchi yetu. Leo naomba nitoe dukuduku langu kwa uchache sana. Kwa mshtuko sana nimesikitika kuona baadhi ya vyama vya upinzani kuanza ubaguzi wa waziwazi kwa kuumia na kuweka nongwa Serikali kupeleka maendeleo na kutekelezwa kwa miradi mbalimbali ya maendeleo kwenye maeneo fulani ya nchi.

Inashangaza sana lakini ni hatari unapoona mtu anayetaka nafasi kubwa kabisa ya uongozi kwenye nchi kuanza mapema kubagua watu anaotaka kuwaongoza kwa kuweka chuki za hadharani na kuumia eneo fulani la nchi kupelekewa maendeleo.

Kwani Chato iko nchi gani? Sio Tanzania. Sasa kwanini pakipelekwa maendeleo yaliyopelekwa pia sehemu nyingine za nchi mtu ateseke? Kwani Chato hakuna Watanzania mpaka wasipelekewe maendeleo wao?

Kama ni viwanja vya ndege vimejengwa kila mahali nchi nzima. Kama ni barabara kila wilaya na halmashauri kipindi hiki zimepelekewa fedha za miradi ya barabara. Kama ni taa za barabarani zimejaa kila miji nchi nzima. Sasa kwanini ikiwa Chato mtu aumie na kuweka nongwa? Kwani Chato wanaishi Wahutu au Wazuru? Si Watanzania kama Watanzania wowote popote pale nchi nzima?

Hii ni hatari sana kwa mtu tu anayeomba Urais kuanza kugawa watu na kuona kuna watu wanapaswa wapate maendeleo na wengine hawapaswi kupata. Hii ni ishara mbaya sana kwetu Watanzania. Watanzania wote popote walipo wanapaswa na wana haki ya kupata maendeleo. Si dhambi wala uvunjifu wa sheria, ni wajibu kwa kiongozi yeyote yule.

Kwa wana Chato na Watanzania wote nchi nzima hii ituamshe kama bado kuna watu wako usingizini. Hakuna kilichofanyika Chato ambacho hakijafanyika popote pale nchi nzima. Jambo gani lipo Chato na halipo kwengine Tanzania? Lipi?

Narudia tena hii ni hatari na haifai kuungwa mkono. Mwisho ni kwa Watanzania wote, tuwe makini na macho sana na baadhi ya wagombea walio tayali kutumia hila na kila aina ya njia na njama kupata uongozi, walio tayali kutugawa na kutuchonganisha ili wao wapate uongozi. Karma ya kwanza ya kiongozi ni kuunganisha na kuongoza watu kuelekea maendeleo. Sasa unapoona kiongozi anaanza kuwagawa na kuwapasua inahatarisha sana. Twende tukawanyime kura Oktoba 28.
Rubbish, na anaesema mkichagua wapinzani siwaletei maendeleo
 
residentura

JF-Expert Member
Mar 1, 2017
2,852
2,000
Uwanja wa Chato ulipitishwa na Bunge; labda tu uulize zabuni, lakini bajeti ya uwanja wa Chato iko kwenye hansard za bunge wazi kabisa. Niliwahi kuzileta hapa miezi kadhaa iliyopita mpaka watu akazidi kukasirika kwa nini bunge lilipitisha vile; wakabaki kulilalamika tu kuwa kwa nini uwanja huo haukujengwa Geita mjini badala yake ukajengwa Chato. Hili ni swali jingine lakini siyo kuwa haukupitishwa na Bunge; ni vizuri kuongea mambo ukiwa na data kamili kuliko kuongeza kwa hisia tu.
Naomba link ya huo uzi au ushahidi wa "hansard".
 
Kichuguu

Platinum Member
Oct 11, 2006
9,992
2,000
..hoja ya msingi ni miradi kulundikwa chato, huku maeneo mengine ya Geita wakiwa watazamaji.
Hap unabadilisha hoja ya msingi, ngoja nitakutafutia clip ya Lissu aliyosema kwau uwanja ule umejengwa bila idhini ya Bunge; jambo ambalo ni upotoshaji na sometimes naona kama ni insult kwa intelligence ya watanzania.
 
JokaKuu

Platinum Member
Jul 31, 2006
20,094
2,000
Hap unabadilisha hoja ya msingi, ngoja nitakutafutia clip ya Lissu aliyosema kwau uwanja ule umejengwa bila idhini ya Bunge; jambo ambalo ni upotoshaji na sometimes naona kama ni insult kwa intelligence ya watanzania.
..bunge is just a rubber stamp ya mambo ya kihuni ya watawala.

..kama utakumbuka hata ufisadi wa kuuza nyumba za serikali ambao Magufuli alihusika alipokuwa waziri ulipitishwa na bunge.
 
permanides

JF-Expert Member
May 18, 2013
4,461
2,000
Huyu mpuuzi tu anajua hawezi kupata urais anachotaka ni kutuharibia nchi kisha aende kwa mahawala zake Ulaya.

Ni YEYE aliyebeza ripoti ya makinikia akasema tutashitakiwa MIGA.

Ni YEYE aliyebeza jitihada za kupambana na uhaini Kibiti.

Ni YEYE asiyeamini katika maendeleo ya vitu na ndiyo maana chama chake hakina ofisi maalumu ya makao makuu

Ni YEYE anayedhani maendeleo ya watu hayahitaji maendeleo ya vitu.

Ni YEYE mropokaji asiyejielewa anaongoza nyumbu wenzie wasiojitambua
Acha siasa uchwara, Lisu alisema serikali haiwezi kuvunja mikataba ya madini kwani MIGA itawahusu, na kweli ni mkataba upi walivunja? Report za makinikia zilikuwa za kubumba tu, kikao cha wataalam kilichokutanisha pande zote mbili hatukuweza kuthibitisha wizi wowote kuhusu uchimbaji madini, ndio maana walisema watatoa pesa kama za urafiki mwema. Zile Noah za kila mtu nadhania zishafika na sasa wanazifanyia clearance bandarini.
 
Idimi

JF-Expert Member
Mar 18, 2007
13,124

Dah. Na Noah yangu imo humo humo melini?
 
mbandeon

JF-Expert Member
Aug 27, 2014
1,364
2,000
Huyu mpuuzi tu anajua hawezi kupata urais anachotaka ni kutuharibia nchi kisha aende kwa mahawala zake Ulaya.

Ni YEYE aliyebeza ripoti ya makinikia akasema tutashitakiwa MIGA.

Ni YEYE aliyebeza jitihada za kupambana na uhaini Kibiti.

Ni YEYE asiyeamini katika maendeleo ya vitu na ndiyo maana chama chake hakina ofisi maalumu ya makao makuu

Ni YEYE anayedhani maendeleo ya watu hayahitaji maendeleo ya vitu.

Ni YEYE mropokaji asiyejielewa anaongoza nyumbu wenzie wasiojitambua
Ni YEYE anaewaaminisha wafuasi wake kuwa CCM wabaya kumbe ni baniani ...maaana amekiri mwenyewe ndege iliyompeleka Nairobi matibabu imelipiwa na mwana CCM. RIP Mr. White.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom