Uchaguzi 2020 Chama kinachotaka kuhudumia Watanzania, kinabagua na kuweka nongwa maendeleo yakipelekwa sehemu fulani ya nchi

Bekiri

Member
Jun 30, 2013
14
75
Kampeni za vyama mbalimbali vya siasa zimeendelea kutimua vumbi maeneo mbalimbali ya nchi yetu. Leo naomba nitoe dukuduku langu kwa uchache sana. Kwa mshtuko sana nimesikitika kuona baadhi ya vyama vya upinzani kuanza ubaguzi wa waziwazi kwa kuumia na kuweka nongwa Serikali kupeleka maendeleo na kutekelezwa kwa miradi mbalimbali ya maendeleo kwenye maeneo fulani ya nchi.

Inashangaza sana lakini ni hatari unapoona mtu anayetaka nafasi kubwa kabisa ya uongozi kwenye nchi kuanza mapema kubagua watu anaotaka kuwaongoza kwa kuweka chuki za hadharani na kuumia eneo fulani la nchi kupelekewa maendeleo.

Kwani Chato iko nchi gani? Sio Tanzania. Sasa kwanini pakipelekwa maendeleo yaliyopelekwa pia sehemu nyingine za nchi mtu ateseke? Kwani Chato hakuna Watanzania mpaka wasipelekewe maendeleo wao?

Kama ni viwanja vya ndege vimejengwa kila mahali nchi nzima. Kama ni barabara kila wilaya na halmashauri kipindi hiki zimepelekewa fedha za miradi ya barabara. Kama ni taa za barabarani zimejaa kila miji nchi nzima. Sasa kwanini ikiwa Chato mtu aumie na kuweka nongwa? Kwani Chato wanaishi Wahutu au Wazuru? Si Watanzania kama Watanzania wowote popote pale nchi nzima?

Hii ni hatari sana kwa mtu tu anayeomba Urais kuanza kugawa watu na kuona kuna watu wanapaswa wapate maendeleo na wengine hawapaswi kupata. Hii ni ishara mbaya sana kwetu Watanzania. Watanzania wote popote walipo wanapaswa na wana haki ya kupata maendeleo. Si dhambi wala uvunjifu wa sheria, ni wajibu kwa kiongozi yeyote yule.

Kwa wana Chato na Watanzania wote nchi nzima hii ituamshe kama bado kuna watu wako usingizini. Hakuna kilichofanyika Chato ambacho hakijafanyika popote pale nchi nzima. Jambo gani lipo Chato na halipo kwengine Tanzania? Lipi?

Narudia tena hii ni hatari na haifai kuungwa mkono. Mwisho ni kwa Watanzania wote, tuwe makini na macho sana na baadhi ya wagombea walio tayali kutumia hila na kila aina ya njia na njama kupata uongozi, walio tayali kutugawa na kutuchonganisha ili wao wapate uongozi. Karma ya kwanza ya kiongozi ni kuunganisha na kuongoza watu kuelekea maendeleo. Sasa unapoona kiongozi anaanza kuwagawa na kuwapasua inahatarisha sana. Twende tukawanyime kura Oktoba 28.
 

Tigershark

JF-Expert Member
Oct 9, 2018
5,611
2,000
Acha uongo!

*Taja wilaya nyingine nchini yenye kiwanja cha ndege kama cha Chato!
*Taja wilaya nyingine ambayo kunafanyika mpango wa kujenga hospitali kubwa ya rufaa ya kuhudumia kanda nzima!
*Taja wilaya nyingine nchini ambapo kuna mpango wa kujenga uwanja mkubwa wa kimataifa wa mpira wa miguu!

Marais waliotangulia wangeamua wajenge viwanja vijijini kwao nchi hii ingekuwaje?

Kuna miradi kama Barabara, shule, hospitali, maji nk yenye kufanana na hiyo hakuna mtu amestuka wala kuhoji!

Ila miradi inayofanyika Chato ni ya ziada, ni mzigo kwa taifa! Ukiangalia sio kila mkoa nchini una kiwanja chenye hadhi kama ya Chato!

>>Je, kuna uhusiano wowote wa Rais kutokea Chato na miradi hiyo kwenda Chato au ni coincedence tu?
 

Kertel

JF-Expert Member
May 11, 2012
4,198
2,000
Kwani wanapinga maendeleo au matumizi mabaya ya fedha yasiozingatia sheria na kanuni za nchi,mmeulizwa ni bunge lipi lilipitisha maamuzi ya ujenzi wa uwanja wa ndege chato,zabuni ilitangazwa wapi akina nani waliomba hiyo zabuni.

Huyu aliyekuepo ndio mbaguzi kwa wananchi anaowaongoza,kwa kinywa chake ametamka kuwa hawezi kupeleka shughuli za maendeleo maeneo ambayo wamechagua watu ambao yeye hawataki(kumbuka hao ni wananchi na wanalipa kodi pia)

Angalia bomoabomoa,mwanza hawakubomolewa na sababu alitoa mwenyewe kuwa ndio waliomchagua,watu wa kibamba ubungo wakaliwa vichwa,mtu kama huyu wanini nchini kwetu.
 

Interested Observer

JF-Expert Member
Mar 27, 2006
1,866
2,000
Aliyoongea Menyekiti wenu huko kote hadi Bunda akasema wazi kabisa sijawaletea maji na barabara kwa sababu hamjachagua CCM . Hujasikia. Lisu anataka majimbo yanayo zalisha nayo yafaidike siyo kufaidisha serikali tu. Fedha zitoke Iringa na Mbeya halafu zijenge uwanja Chato wapi na wapi?
 

Bill

JF-Expert Member
Oct 5, 2007
6,045
2,000
Huyu mpuuzi tu anajua hawezi kupata urais anachotaka ni kutuharibia nchi kisha aende kwa mahawala zake Ulaya.

Ni YEYE aliyebeza ripoti ya makinikia akasema tutashitakiwa MIGA.

Ni YEYE aliyebeza jitihada za kupambana na uhaini Kibiti.

Ni YEYE asiyeamini katika maendeleo ya vitu na ndiyo maana chama chake hakina ofisi maalumu ya makao makuu

Ni YEYE anayedhani maendeleo ya watu hayahitaji maendeleo ya vitu.

Ni YEYE mropokaji asiyejielewa anaongoza nyumbu wenzie wasiojitambua
 

Blac kid

JF-Expert Member
Apr 1, 2012
5,380
2,000
Mbabu wa chatto mbaguzi hatari, kodi za jimbo la bwege anazitaka ila maendeleo hataki kupeleka kisa walichagua cuf, safari hii tunaenda na lissu, mbabu wa chatto apumzike mbaguzi wa vyama huyo
 

Kichuguu

Platinum Member
Oct 11, 2006
10,088
2,000
Kwani wanapinga maendeleo au matumizi mabaya ya fedha yasiozingatia sheria na kanuni za nchi,mmeulizwa ni bunge lipi lilipitisha maamuzi ya ujenzi wa uwanja wa ndege chato,zabuni ilitangazwa wapi akina nani waliomba hiyo zabuni.
Huyu aliyekuepo ndio mbaguzi kwa wananchi anaowaongoza,kwa kinywa chake ametamka kuwa hawezi kupeleka shughuli za maendeleo maeneo ambayo wamechagua watu ambao yeye hawataki(kumbuka hao ni wananchi na wanalipa kodi pia)
Angalia bomoabomoa,mwanza hawakubomolewa na sababu alitoa mwenyewe kuwa ndio waliomchagua,watu wa kibamba ubungo wakaliwa vichwa,mtu kama huyu wanini nchini kwetu.
Uwanja wa Chato ulipitishwa na Bunge; labda tu uulize zabuni, lakini bajeti ya uwanja wa Chato iko kwenye hansard za bunge wazi kabisa. Niliwahi kuzileta hapa miezi kadhaa iliyopita mpaka watu akazidi kukasirika kwa nini bunge lilipitisha vile; wakabaki kulilalamika tu kuwa kwa nini uwanja huo haukujengwa Geita mjini badala yake ukajengwa Chato. Hili ni swali jingine lakini siyo kuwa haukupitishwa na Bunge; ni vizuri kuongea mambo ukiwa na data kamili kuliko kuongeza kwa hisia tu.
 

Gogovivu45

JF-Expert Member
Oct 10, 2019
229
250
Huyu mpuuzi tu anajua hawezi kupata urais anachotaka ni kutuharibia nchi kisha aende kwa mahawala zake Ulaya.

Ni YEYE aliyebeza ripoti ya makinikia akasema tutashitakiwa MIGA.

Ni YEYE aliyebeza jitihada za kupambana na uhaini Kibiti.

Ni YEYE asiyeamini katika maendeleo ya vitu na ndiyo maana chama chake hakina ofisi maalumu ya makao makuu

Ni YEYE anayedhani maendeleo ya watu hayahitaji maendeleo ya vitu.

Ni YEYE mropokaji asiyejielewa anaongoza nyumbu wenzie wasiojitambua

Ni YEYE aliyebeza ripoti ya makinikia akasema tutashitakiwa MIGA. ( Wewe unafahamu hatima ya tanzania na MIGA, ana anafahamu makubaliano yake? ulishawahi kuyasoma? au ndo yale ya mlamba kuwa watanzania wale nyasi lakini ndege ya raisi inunuliwe . baada ya uwaziri akala nyundo
 

Kichuguu

Platinum Member
Oct 11, 2006
10,088
2,000
Ni YEYE aliyebeza ripoti ya makinikia akasema tutashitakiwa MIGA. ( Wewe unafahamu hatima ya tanzania na MIGA, ana anafahamu makubaliano yake? ulishawahi kuyasoma? au ndo yale ya mlamba kuwa watanzania wale nyasi lakini ndege ya raisi inunuliwe . baada ya uwaziri akala nyundo
Hamna lolote! Acacia ilikuwa ni subsidiary ya Barrick, halafu Barrick ikaamua kuingilia kati na kuidissolve Acaia, badala yake ikakubaliana na serikali kuundwa kwa Twiga. Kwa hiyo mpaka sasa hivi tunavyoongea Acacia ni nonexitent entity, na iwapo Barrick walikubaliana na serikali, na tayari wameshailipa serikali sehemu ya zile damages, sijui ni nani atapeleka mashitaka hayo unayohofia zaidi kuliko kutunza raslimali zako. Yaani kuogopa kushitakiwa kwa kulinda mali zako inakuwa ni tatizo kweli jamani? Tanzania tulipigania uhuru dhidi ya umoja wa mataifa halafu leo tuogope kupigania raslimali zetu kutoka makampuni ya watu binafsi kweli?

Anayeogopa kushitakiwa kuingia ndani ya nyumba yake akaamua kubaki nje usiku kucha hasitahili kumiliki nyumba hiyo!
 

Vessel

JF-Expert Member
Aug 29, 2018
981
1,000
Yupo ambae ni hodari zaidi,katika Hilo,anachosema yeye sicho anachomaanisha ,hapa ndipo ninapo hoji uzalendo anaojinadi kuwa nao, wakati wazalendo halisi wanaibua maovu take pamoja na kutetea haki na usawa unao patikana so tuu katika Sheria Bali hata kwenye taratibu za jamii mbalimbali.
 

law healer

JF-Expert Member
Apr 2, 2019
454
1,000
Hamna lolote! Acacia ilikuwa ni subsidiary ya Barrick, halafu Barrick ikaamua kuingilia kati na kuidissolve Acaia, badala yake ikakubaliana na serikali kuundwa kwa Twiga. Kwa hiyo mpaka sasa hivi tunavyoongea Acacia ni nonexitenet entity, na iwapo Barrick walikubaliana na serikali, na tayari wameshailipa serikali sehemu ya zile damages, sijui ni nani atapeleka mashitaka hayo unayohofia zaidi kuliko kutunza raslimali zako. Yaani kuogopa kushitakiwa kwa kulinda mali zako inakuwa ni tatizo kweli jamani? Tanzania tulipigania uhuru dhidi ya umoja wa mataifa halafu leo tuogope kupigania raslimali zetu kutoka makampuni ya watu binafsi kweli?

Anayeogopa kushitakiwa kuingia ndani ya nyumba yake akaamua kubaki nje usiku kucha hasitahili kumiliki nyumba hiyo!
We Jamaa una akili|point za msingi sana..Pia ni Mfuatiliaji wa Vitu vya Msingi.

Huyu Lissu ni Puppet tu..Anataka kutuuza kwa Makaburu.
 

KANYIMBI

JF-Expert Member
Nov 6, 2011
775
1,000
Mkuu, wapinzani wapo sahihi.
Alichokosea huyo mkubwa wa Chato ni kuendekeza umimi 'Conflict of interest'. Viongozi wenzake wote waliomtangulia hawakufanya hivyo kwenye vijiji wanavyotoka. Mbaya zaidi hakukuwa na bajeti iliyopitshwa Bungeni kwa hicho alichokifanya.

Mbaya zaidi tumehabarishwa Dada aliyeidhinisha fedha na aliyepewa tenda ya ujenzi wa uwanja wote wanauhusiano na familia ya mkubwa - hilo ni kosa jingine.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom