Chama kinachoratibu miswaada ya namna hii hakiwezi kuwa na nia njema na Tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chama kinachoratibu miswaada ya namna hii hakiwezi kuwa na nia njema na Tanzania

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ntemi Kazwile, Apr 12, 2011.

 1. Ntemi Kazwile

  Ntemi Kazwile JF-Expert Member

  #1
  Apr 12, 2011
  Joined: May 14, 2010
  Messages: 2,145
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Muswada mpya wa katiba ni kielelezo kuwa Chama Cha Mapinduzi bado hakiko tayari kuleta usawa na haki katika taifa hili.

  Wakati wengi wetu wakijawa na matumaini kuwa huenda kukawa na mabadiriko tunayoyataka kufuatia kujiudhuru kwa CC na NEC ya CCM ndani ya chama hiki kikongwe binafsi naona hii ni fursa nyingine ya kuongeza muda na kuwalaghai watanzania. Matamanio ya CCM ni kuhakikisha kuwa kinaminya uhuru hata kidogo uliopo ili kuhakikisha kuwa kundi la watawala wanaendelea kuwepo kupitia vibaraka wao.
  Kama kweli CCM ilikuwa na nia ya kuleta mabadiriko yanayotarajiwa ingekuwa mstari wa mbele kuikemea serikali yake iondokane na mpango wa kupeleka muswada wa ajabu na hii, ingewaomba wabunge wake wasiuunge mkono, lakini kwa sababu hiki ni chama cha kidhalimu kimebariki udhalimu huu na bado kinataka kutudanganya kuwa kimeanza kupambana na ufisadi kwa kuwaondoa makada wake wanaotuhumiwa kwa ufisadi kutoka kwenye vyombo vyake vya maamuzi.

  Nionavyo CCM siyo chama cha kuaminika hata kidogo, hawa wanatakiwa wawajibishwe kwa kunyimwa idhini ya kututawala wakae pembeni watu wengine nao watumikie hatutaki kuletewa mvinyo ule ule kweny chupa mpya
   
 2. I

  Igembe Nsabo Member

  #2
  Apr 12, 2011
  Joined: Jun 4, 2010
  Messages: 87
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Ngugu yangu Ntemi Kazwile, Ni kweli uyasemayo kwani CCM inatakiwa inyimwe fursa ya kuendelee kutawala Nchi hii, Soma hii sehemu ya barua ya ndugu Joseph Butiku Augosti, 2005 kwenda kwa Benjamini Mkapa ina sema hivi

  "..........Taifa zima linapiga kelele Rushwa, Rushwa, Rushwa na labda siyo rushwa tu; ni kuuza Nchi kwani fedha zinazoonekana ni nyingi sana lakini zizizojulikana zinatoka wapi!
  Wanayo pia haki ya kutaka maelezo ya Mwenyekiti wao kuhusu vianzo vya fedha hizi zinazotumiwa kuvuruga chama na Taifa. CCM itake isitake inayo kasoro katika eneo hili........"

  kwa mantiki hiyo CCM kama ingekuwa na nia ya dhati kujivua gamba, kwanza ingepambana na UFISADI kwanza au ingelishughulikia suala la Katiba pia kwa dhati na siyo utapeli huu inaoufanya kwenye macho ya jamii.
   
Loading...