jiamini360
Member
- Jan 26, 2016
- 35
- 19
Kwanini Vijana wa Tanzania tusianzishe chama cha siasa kitakachoongozwa na vijana tu na kuachana na hizi bongo movie za hawa CCM, CUF, CHADEMA, NCCR n.k
Viongozi wa chama umri miaka 18-30 mfano
Mgombea wetu Urais kijana anaandaliwa labda mtu mwenye umri wa miaka 35, anaandaliwa kwa miaka kumi kabla ya kugombea.
Kwanini nasema hivi
Kuwa mwanachama na hapa siongelei ushabiki ni kuwa na kadi ya chama na kuwa na sauti na maamuzi ndani ya chama, lakini halli ni tofauti nchini kwetu. Wenye maamuzi ni watu wachache kwenye inner circle ya vyama. Sasa kwanini vijana tusianzishe chama chetu wenyewe ambapo kila mwanachama anayelipia uanachama wake awe na sauti na uwezo wa kufanya maamuzi ndani ya chama kuanzia kuchagua viongozi, kutaka kugombea uongozi, kushauli chama n.k Hii ni kalne ya 21 yote yanawezekana kwa nguvu ya teknolojia.
Chama cha vijana kujipika kiuongozi
Sisi vijana ndio taifa la kesho na sisi ndio wakuandaa taifa la kesho kutwa. Viongozi wetu wazee walipokuwa vijana waliandaliwa kuja kuwa viongozi wa leo, kwa mfano walikuwa na chuo chao cha siasa Kigamboni. Lakini vijana wa leo wakuja kuwa viongozi wa kesho hakuna wa kuwaandaa zaidi ya kubebana kifamilia/kujuana. Kama baba yako ni mtu mzito kwenye serikali basi na wewe njia yako ni nyeupe ukitaka kujiusisha na uongozi wa Taifa lako. Ila kama ni akapuluko kama wengi wetu ngumu mno yani patashika nguo kuchanika.
Kuwa na nia thabiti na nchi
CCM: Hiki ndicho chama tawala, Japokuwa Magufuli ana mazuri yake anayayoyafanya kwa kupambana na maovu, tunasahau kwamba hayo maovu yaliyotukuka yamekuwepo chini ya utawala wao, sio jambo la kusifia ni jambo la aaibu kwa chama tawala, Magufuli ni kama Rais aliyeshinda kutoka upinzani sasa anafufua mafuvu ya chama tawala, yananuka uozo . Na CCM wengi wao wameoza, siku wakiwa wapinzani tutajua akili zao.
CHADEMA: Wapinzani wakuu Tanzania Bara. Inawezekana wana nia nzuri ila hawana misimamo. Mfano kusema hawamtambui Magufuli kama Rais lakini bado walikwenda bungeni kuapa na kuhudumia/kuhudumiwa chini ya serikali ya mtu wasiyemtambua na sidhani kama kuna kiongozi hata mmoja aliyekiri kumtambua ila wanamuita Rais.
CUF: Wenzetu hawa nao kwenye msimamo, nisahihisheni kama nimekosea. Kikatiba walisema muda wa Rais wa Tanzania Visiwani umekwisha lakini cha kushangaza mpaka leo naamini Maalim Seif bado ni Makamo Wa Kwanza Wa Rais, wanasema serikali ni batili basi Seif ajiuzuru.
Vijana na upinzani wa aina tofauti
Naamini vijana tunaweza kuja pamoja na kubuni njia mbadala za kupambana na serikali si kama wapinzani wa sasa nadhani ni dhaifu kwa sababu kila kitu wao ni kulaani tuuuuu bila kufanya maamuzi maguma siongelei kutoana ngeu, Mfano wanapinga uchaguzi wa Zanzibar badala ya kulaani basi wachukue maamuzi magumu ya wote kujiuzuru ubunge tuone kama chama tawala kitaenda bungeni chenyewe.
Vijana tukianzisha chama chetu we have got nothing to loose
Hili ni wazo tu nina mengi ya kusema ila thread ikiwa ndefu it will be boring nitaacha Wenyenchi mchakachue na kuongeza mawazo mbadala.