Chama kina wenyewe na wenyewe ndio sisi..

Mkandara

JF-Expert Member
Mar 3, 2006
15,772
8,958
Siku ya jana nilishikwa na mtafaruku mkubwa katika majibizano ya kimtandao na wana Chadema ambao kwa upeo wao wa kuelewa kile walichofundishwa ama kusoma tafsiri ni kwamba Chama chochote cha siasa kina wenyewe na wenyewe ni WANACHAMA. Kwa maana hiyo waliendelea kudai kwamba Chadema ni chama chao na wao ndio wenye mamlaka ya chama hicho na sio mtu mwingine yeyote asiyekuwa mwanachama.

Pengine watu tunapishana kuelewa na pengine mimi ndiye sijui kwamba vyama vya siasa vina wenyewe kwa sababu tu naamini wanachama HUJIUNGA na chama na hivyo kujiunga kwao ama kutojiunga hakuondoi wala kukipa uhai Chama cha siasa. Nijuavyo mimi Sii Mtei, Mrema, Maalim Seif wala Nyerere na wenzao walokuwa na miliki ya vyama vya siasa na ndio maana wakaitwa waasisi wa chama. Na wote hawa hata baada ya chama kuasisiwa, walijiunga na kupewa kadi ya uanachama wakaapishwa na sio kukabidhiwa hati miliki ya chama.

Chama hutokana na FIKRA pevu ambazo asili yake ni hekima juu ya maswali na majibu ya uongozi bora kwa wananchi wenye mahitaji na itikadi kuwa msingi wa imani ya kinadharia unaotoa mwongozo, dira na mbinu (sera) za kuwakilisha wanananchi hao katik amahitaji yao. Sasa inapofikia mtu kunambia kwamba Chama kina wenyewe kama kwamba WAZO ama FIKRA ya uasisi wa chama huwapa hati miliki wahusika wake. Imenishangaza sana hata kuona wasomi wetu wanaamini kabisa kwamba chama kina wenyewe na wenyewe ndo wananchama kwa sababu tu wamesoma Google imeandikwa kuwa ni kundi la watu wenye fikra sawa, sasa ni lini fikra ya Itikadi (Ideology) ikatokana na miti au wanyama.

Na ndio maana sasa naelewa kwa nini Mohamed Said huweka madai juu ya CCM kwa fikra za kwamba CCM ina wenyewe na wenyewe ndiio wao. Na ndio maana kuna watu ndani ya CCM, CUF, na Chadema kwa dhana zao wanafikiria kuwa mwanachama inakupa haki miliki ya chama hicho japo mwanachama HUJIUNGA na kuwa MWANA CHAMA yaani zao la chama. Na badala ya wanachama kuchukua dhamana ya waumini wa itikadi na kutenda waloyaamini kuwatumikia wananchi hutumia muda mwingi kushawishi kukinadi chama ili kuvuta wanachama zaidi. Hivyo nguvu kubwa hutumika kukijenga chama wakati chama ni falsafa zinazotoa majibu ktk maendeleo ya wananchi na sio utajirisho wa chama ama wanachama wake.

Na haitoshi inanisumbua zaidi kuona pale viongozi na wanachama wa vyama vya siasa kudhania kwamba wao ndio wenye miliki ilihali chama hicho kinaendeshwa na kodi za wananchi wote bila kujali tofauti zao ktk uanachama ama kutokuwa wanachama. Na wananchi wana jukumu kubwa la kubeba mzigo wote toka kuviendesha hadi kuwapa ridhaa ya kuongoza nchi wakitegemea watapata viongozi kumbe kinachofuata ni WATAWALA ambao kwao chama ni mali yao na chochote kinachopatikana kwa nguvu ya chama ni chao vile vile. Hivyo ndio maana viongozi wa vyama hivi wanaposhika nchi huchukulia kama ni matunda ya kazi yao.

FIKRA Hii ndio mwanzo na chombuko la kutokuwa na viongozi bali watawala na ndio maana watu wengi hujiunga na vyama vya siasa kwa sababu wanajua watahesabika ktk hisa la uwekezaji wao. Vyama vya siasa vimegeuka NGO watu wanagombea uongozi kwa sababu sio dhamana bali ni fursa (Opportunity). Na ndio maana kumbe watu wakisema uongozi mbovu wa CDM hujibiwa kwa nini hutazami yenu? wakiisema CCM wataambiwa kwani nyie mna nafuu gani? Usipokuwa na chama basi huna haki ya kuwasema wowote japo utaombwa na utatakiwa kwa udi na uvumba uwape kura yako.
 
Back
Top Bottom