Waga
JF-Expert Member
- Feb 6, 2008
- 322
- 14
Mlala hoi ambaye hawezi kumudu mlo kamili kwa siku anakuwa na matumaini pale anapoamua kukipigia kura chama hiki, na chama alichokichagua kinampa ahadi hizi
Tuta watengenezea ajira milioni moja
Tutawaletea maisha bora kwa kila mtanzania
Tutawatengenezea bara bara nzuri
Tutahakikisha hakuta kuwa na shida ya maji.
Mbaya zaidi hao hao tuliowapa kura wapo ambao wameamua kujinufaisha wao wenyewe na familia zao kwa kuamua kuitumbukiza nchi hii kwa kuchota mahela ambayo ni wazi ni za walipa kodi.
Hawa hawa tuliowapa kura wameamua kuwatetea wale wote waliojichotea mapesa ya walipa kodi kwa kutuambia..
Lowasa hausiki na sakata la Richmond
Karamagi hausiki na sakata la Richmond
Chenge pesa alizokutwa nazo hajavunja nyumba kuiba
Pesa za Epa si pesa za serikali
Report ya madini mpaka leo hatujaisikia
Haya ni machache tu kati ya mengi ambayo wanachi waliowapa kura wangependa kusikia mustakhabali wake lakini yaonekana dhahiri kuna mpango wa kuyazima na yameshaanza kupotea taaratibu.
Kinachouma zaidi ni pale wanaposahau kuwa tumewateua kuwa wapigania maslahi ya walalahoi wa Tanzania kwa kuonyesha wazi nia ya kuwanyamazisha wale wanaoonekana kuguswa na shida zilizokithiri hapa nchini kwa kuamua kutetea moja kwa moja maslahi ya Taifa hili. Tumeona wazi juzi kwa kuamua kutoonyesha hotuba ya kambi ya upinzani kuhusu bajeti ya waziri mkuu, inawabidi muelewe wazi kuwa hapo mnawakilisha wanachi na tungependa kujua nini kinachoendelea na si kuwanyima fursa hiyo.
Ni mengi sana ambayo tumeahidiwa na chama hiki lakini mpaka leo hii hakuna utekelezaji kiasi kwamba baadhi ya wabunge wake wanadiriki kusema ndani ya bunge kuwa wasipotekelezewa ahadi zao walizopewa na serikari kama hazitatekelezwa hatatoka mtu ndani ya bunge.
Cha kujiuliza hapa ni kwa nini hata wabunge wao wanafikia maamuzi ya kusema hivi ?
Ni dhahiri wamechoshwa na ahadi hewa za serikali ya chama chao ndo mana wanaamua kusema hayo wanayoyasema, na kama mbunge anachoshwa mwananchi wa kawaida ambaye hana uhakika wa kula mlo kamili kwa siku anafikiriwaje ?
TUMETENDA MEMA KUWACHAGUA LAKINI DHAHIRI MMETULIPA MABAYA