Chama hiki hakijafanya sawa kwa huyu aliyekuwa mbunge, mjitafakari sana

Countrywide

JF-Expert Member
Mar 2, 2015
18,173
27,223
Kuna mbunge mmoja ambaye kwa sasa sio mbunge tena, ambaye hali yake kiafya sio nzuri sana na ninamuombea kwa Mungu amponye apone haraka.

Suala lake lilitoka mbali sana, Wala sio la Jana wala leo. Amekua na financial crisis, hiki ni kitu Cha kawaida sana kwa binadamu hasa sisi wanaume wapambanaji.

Wakati wa uchaguzi mkuu wa 2020, wabunge wa hiki chama walichangishwa kinguvu pesa nyingi kwa ajili ya kampeni za Raisi tu kwa sababu anayegombea hakuwa na pesa.

Hivyo lilikua jukumu la wabunge kumchangia mgombea uraisi na hii ilikua ni utake usitake.

Huyu mbunge Kama tunavyojua hakua na muda mrefu kwenye siasa hivyo hakuwa ametengeneza pesa nyingi kihivyo lakini chama kilimkamua hivyohivyo.

Baada ya kushindwa ubunge, mambo yake yalianza kuwa vibaya maana alikua na madeni makubwa mengi na biashara zake zikawa haziendi vizuri kabisa.

Hivyo stress zikawa kubwa sana na hajui nini afanye, ikabidi amcheki yule jamaa muuza nguo ili waweze kuwa partner kwenye dili la jezi za timu fulani hivi kubwa, lakini bado mambo hayakua mazuri.

Muda ukapita bado hali ngumu, ndio akaenda kuomba kazi kwenye kituo Cha radio maarufu sana hapa bongo.

Kituo hicho wakakubali kumchukua ili mambo yake yakae sawa kidogo, Ila from nowhere watu walewale wa chama chake wakaanza kumsema kuwa amekubali vipi ku-surrender tena kwenye kazi ya utangazaji ikiwa yeye ashafika level ya mbunge.

Jamaa akaonaa sio kesi akahairisha hiyo kazi hapo redioni, akawa busy na music ili arudi kwenye game na akawa anatafuta promoters ili wampe show za hapa na pale, japo napo mambo yalikua magumu pia.

Sasa ni mgonjwa, chama hakija shughulikia suala la matibabu yake na imeachiwa familia tu na rafiki zake kwa kisingizio kuwa kiongozi wao ana kesi hivyo chama kwa Sasa kinashughulikia kumaliza kesi.

Yote haya yamesababishwa na chama chake, Ila Yote kwa yote naamini Mungu atampigania na atapona.

Lawama zote nazitupa kwa chama chake.

20220131_181042.jpg
 
Sisi hatujawahi kuwa wabunge wala kupata hata kipato hicho cha mbunge, lakini tukiumwa tunajitibu wenyewe na hatupati msaada wowote. Kwanini yeye ajigeuze tegemezi kwa chama kama ni kweli usemayo? Kama ni Ramli chonganishi basi umekwama. Labda useme kuwa yeye alikuwa anamtibu kila mfuasi wa CDM alipokuwa anaumwa. Ifahamike hata huko bungeni hakuwa anakwenda na wafuasi. Kama ni ugumu ni kwa wote sio kwake tu na ukweli huu anaujua.
 
CDM imeingiaje hapa?
 
Dah kama ni kweli wa Mitulinga atakuwa na hali mbaya sana aisee! Maana ikumbukwe upanuzi wa kimara-kibaha ulipita na jengo lake Kimara
 
Sisi hatujawahi kuwa wabunge wala kupata hata kipato hicho cha mbunge, lakini tukiumwa tunajitibu wenyewe na hatupati msaada wowote. Kwanini yeye ajigeuze tegemezi kwa chama kama ni kweli usemayo? Kama ni Ramli chonganishi basi umekwama. Labda useme kuwa yeye alikuwa anamtibu kila mfuasi wa CDM alipokuwa anaumwa. Ifahamike hata huko bungeni hakuwa anakwenda na wafuasi. Kama ni ugumu ni kwa wote sio kwake tu na ukweli huu anaujua.
Muulize huyo pimbi Kwani lowasa na salim wanatibiwa na ccm
 
Back
Top Bottom