Chama gani kitakwenda mahakamani kupinga uteuzi wa Dr Shein? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chama gani kitakwenda mahakamani kupinga uteuzi wa Dr Shein?

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Zak Malang, Jul 16, 2010.

 1. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #1
  Jul 16, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Chama gani kitakwenda mahakamani kupinga uteuzi wa Dr Shein?

  Kufuatana na story ya kuu Mwanahalisi wiki hiiuteuzi wa Dr Ali Mohamed Shein kuwania kiti cha urais wa Visiwani ni batili.

  Gazeti limesema kuwa suala hili liliibuliwa katika kikao cha NEC hivi majuzi na Nimrod Mkono ambaye alinukuu katiba ya Zanzibar na kusema kuwa Dr Shein hana sifa za kugombea urais Visiwani kwa sababu hana sifa za kuwania nafasi ya Uwakilishi kule.

  Na hii inatokana na ukweli kwamba Dr Shein hakujiandikisha kama mpiga kura katika daftari la kupiga kura la Visiwani, kwani alijiandikisha kule OystyerBay, jijini Dar es Salaam.

  Mkono alimtaka Dr Shein kujitoa ili kuiondoa CCM kwenye uwezekano wa kupata fedheha, iwapo atawekewa pingamizi katika ZEC au mahakamani na wapinzani.

  Aidha kuna suala la ukazi wa Visiwani. Dr Shein hajakaa Visiwani kwa miaka mitatu mfululizo.

  Lilipoibuliwa katika kikao cha NEC, suala hili liliborongwa-borongwa tu na baadhi ya wajumbe akiwemo mwenyekiti wa CCM, JK.

  Chama kikuu cha upinzani kule Zanzibar – CUF – hakiwezi kumuwekea Dr Shein pingamizi kwa vile kimeshakuwa neutralized kutokana nay ale maridhiano. Habari zinasema kuwa NCCR ndiyo wanajipanga kuweka pingamizi. NCC itakuwa kweli serious?

  Tujadili.
   
 2. Lyangalo

  Lyangalo JF-Expert Member

  #2
  Jul 16, 2010
  Joined: Sep 10, 2009
  Messages: 681
  Likes Received: 77
  Trophy Points: 45
  Wataalamu wa kaiba tusaidieni. kama ni kweli basi ccm wameula wa chuya!
   
 3. macho_mdiliko

  macho_mdiliko JF-Expert Member

  #3
  Jul 16, 2010
  Joined: Mar 10, 2008
  Messages: 6,434
  Likes Received: 2,304
  Trophy Points: 280
  Kwa scenario kama hii usitegeme tume ya uchaguzi au mahakama vina uhuru wa kufanya chochote against serikali. Serikali inaminya 'ka-kitufe' chwee... wewe uliyekimbilia mahakamani unashangaa hoja zako mahakamani zinagota.. tena watakavyofanya mambo kitaalamu litachaguliwa jopo la majaji ishirini na wanne na marafiki wa mahakama wataletwa hata kumi na tisa... na mara utasikia... oho mara hili suala ni la kisiasa blah blah.... mgombea ana sifa....
   
 4. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #4
  Jul 16, 2010
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Hii mbona si hoja?, kwani diplomat kama Ally Karume mbona alikuwa na sifa ya kugombea na ilhali yeye si mkaazi wa Zanzibar, jibu utakalonipatia kuhusu Ally Karume ndilo hilo litakalokuwa linamfit Dr Shein. Kwa kifupi ni kwamba Dr. Shein aliondoka Zanzibar akiwa ni muwakilishi baada ya kuteuliwa kuwa makamu wa rais kufuatia kifo cha Dr Omari Ali Juma July 2001. Kwa kuwa alikuwa huku bara kikazi kama na hasa kama diplomat maana ana passport ya kidiplomasia kabla hajagombea nafasi ya urais Zanzibar kama alivyo Ali Karume basi hakuna wa kumwekea pingamizi na kama litawekwa litatupiliwa mbali kwa hoja nilizozieleza hapa na nyingine nyingi tu zitakazokuwepo huko baadae.

  Hoja hii ina mpango mmoja tu nao ni kuvuruga amani na utulivu Zanzibar kwa kuwashawishi CUF kuweka pingamizi wakidhani itakuwa vinginevyo na baadae Shein atashinda na kuachana na makubaliano. Hakuna hoja hapa Dr. Shein ni Mzanzibar aliyekuwa bara kikazi za Jamhuri ya muungano kama walivyo diplomats akina Ally Karume. Case closed
   
 5. Geza Ulole

  Geza Ulole JF-Expert Member

  #5
  Jul 16, 2010
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 11,065
  Likes Received: 3,993
  Trophy Points: 280
  wewe hiyo hoja umeipata wapi ati Mkono? umemnakili au ndo mambo yenu ya Kiunguja mnayaleta hapa? hamtaki Mpemba atawale sio? mtachunana ngozi muda si mrefu!
   
 6. Faru Kabula

  Faru Kabula JF-Expert Member

  #6
  Jul 16, 2010
  Joined: Mar 26, 2009
  Messages: 10,640
  Likes Received: 2,872
  Trophy Points: 280
  Naomba niulize, hivi wagombea wote wa kiti kimojawapo (urais/ubunge/udiwani) wakiwekeana pingamizi na kuondolewa katika kinyang'anyiro, ni nani sasa atashikilia wadhifa husika (urais/ubunge/udiwani) ?
   
 7. Shalom

  Shalom JF-Expert Member

  #7
  Jul 16, 2010
  Joined: Jun 17, 2007
  Messages: 1,315
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Subiri kwanza jina lake lipitishwe na ZEC. Hujui zec wanaweza kesho kulifungua daftari na yeye akajiandikisha?
   
 8. G

  Gurtu JF-Expert Member

  #8
  Jul 16, 2010
  Joined: May 15, 2010
  Messages: 1,202
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Shalom umenena, maana chochote chaweza kutokea
   
 9. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #9
  Jul 17, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0

  Mkuu H: Hoja kubwa ya Mkono katika kikao cha NEC ilikuwa ni suala hilo a Shein kutojiandikisha kupiga kura kule Visiwani, na siyo hasa suala la ukazi. Katika hoja yako hapo juu hujazungumzia suala hili la kutojiandikisha. Katina ya Zanzibar iko wazi kabisa kuhusu hilo, na Ali Karume uliomtaja alilifahamu hili na alijiandikisha mapema kule.

  Ukubali kitu kimoja tu, kwa kuwa tume ya ZEC (na NEC) siyo huru, ni outrageously pro-CCM, basi ni ubabe tu utatumika kumpitisha Dr Shein kugombea. Mara nyingi CCM hudumu kwa mtindo huu wa ubabe na uvunjifu wa Katiba ambao sasa unaonekana kukithiri. Angekuwa ni mgombea wa chama cha upinzani hawezi kupitishwa na ZEC. Au nasema uongo jamani?
   
 10. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #10
  Jul 17, 2010
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  kwani hakujiandikisha eee?

  alikuwa hana nia ya kutumia haki yake ya kikatba au?

  hapa labda comandoo afanye vitu vyake ampinge Shein ila kwa wenginewe hasa upinzani haiwezi kupambana na tume ya uchaguzi
   
Loading...