Chama chochote kikipata wahamiaji, hasa kutoka CCM na kuwatanya kuwa viongozi wakuu katika chama, mavuno yake yanauma sana!

Pslmp

JF-Expert Member
Mar 18, 2021
1,627
2,000
Wasalaamu wana JF

Hata majumbani mwetu kuna miiko, hauwezi kupata mgeni na siku hiyohiyo unamkaribisha mpaka chumbani, Kuna matazamio na utaratibu maalum.

Kitendo cha Chandema kupata wahamaji kutoka CCM na siku hiyo hiyo kufanywa kuwa viongozi wa meza kuu Chandema na kuruhusu kufahamu mipango yooote ya Chama kwa muda mfupi, ndio kinachomtafuna M/kiti taifa wa chama hicho

Hayo mambo yanayoendelea ni matunda ya makosa ya Chandema iliyoyafanya kipindi cha nyuma.

Mh M/kiti taifa, hajaanza leo kuchunguzwa, tokea vifo hasa kifo cha aliyekuwa mbunge kutokea Mara bwana.

Na katika kuchunguzwa, hutumika mbinu nyingi sana.

Kwa hiyo, hayo yanayoendelea sasa, ni matunda ya kukaribisha wageni wapole ndani yake kumbe sio wageni pekee!

Acha dunia iendelee kuzunguka
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom