Chama changu kiniambie kampeni nashindana na nani

Mshangai

JF-Expert Member
Feb 16, 2008
468
1,085
Mimi ni mmoja wa tuliochukuwa fomu za kugombea Uenyekiti wa Mtaa baada ya kupitishwa na chama changu CCM.

Sikupata pingamizi lolote na najua nakubalika kwani hata kwenye kura ya maoni ndani ya CCM nilimwangusha aliyekuwa mwenyekiti toka CCM.

Ni bahati mbaya wagombea wenzangu wawili mmoja wa CHADEMA na mwingine wa ACT wametangaza hawagombei na hapa mtaani kwetu hilo linatambulika kwa wote hivyo mie napita bila kupingwa ingawa sio kwa heshima kama nilivyopenda mie.

Sasa kama wote wamejitoa hizi kampeni tunafanya kushindana na nani? Mbona chama chetu kinataka kututia fedheha namna hii huku mtaani tuonekane kituko?

Mie binafsi nilikuwa najitambua kuwa ningeshinda kwa umahiri wangu bila hata kutegemea nguvu ya chama changu cha mapinduzi, lakini sasa nitaweka wapi sura yangu kwani najulikana kuwa nimebebwa na hao watendaji walio pewa maagizo na Ikulu kwani ni kweli walipewa na wao wanaona fahari kujitangaza kufuata amri ya Ikulu.

Hizi kampeni hewa zinatuaibisha na tutazomewa na kukejeliwa, Dr Bashiru walau wewe unatumia busara ingilia kazi ujinga huu.

CCM hoyee!
 
Ipo siku Mwenyekiti wa Mtaa katika kuhudumia mwananchi, ukasikia kwanza sikukuchagua
 
Najuwa jamaa mjanja anataka muisaidie tnccm na chamael 10 kutangaza tumeteketeza 2019 sorry tumekeleza 2019
 
Mm sina chama maalumu kwa ujinga huu uliotokea sina haja kwenda kupiga kura kabisa!! Siwezi shiriki kitu batili
 
Naona umezindua kampeni kwa kishindo mbali kwamba huna mpinzani nakutakia kila la heri
 
tapatalk_jpeg_1573327601937.jpeg
 
Mtajijua wenyewe,mmekubali kufanywa mazuzu. Yaani mtu unapambana peke yako halafu unajipigia kampeni. Halafu mtakuja kujitangaza mmepata ushindi wa kishindo . Awamu hii nimegundua sio kila kichwa kina ubongo,kuna vichwa vina uji.
 
Pambana na kivuli hakuna namna
Najua mnatudharau sana sasa hivi kwa jinsi tunavyo endesha chama chetu, lakini msilojua ni kuwa Chama chetu kimevamiwa na wasio juwa siasa asilia ya CCM.
Kuanzia mwenyekiti wetu, KM hadi Polepole. Mbaya ni kuwa wajumbe wa NEC na KK wako kimya ingawa wanaona ujinga huu.
CCM asilia unakuta mume CCM mke CUF au CCM Mke na mume Chadema na maisha yanaenda kawaida, lakini sasa hivi ni uadui mkubwa kama genocide ya Rwanda mume Mhutu anaambiwa mchinje mkeo mtusi.
Wajibu wa kuibadili CCM irudi ya zamani ni wetu wenyewe wanaccm kwa mwakani kuisafisha.
 
Ni bahati mbaya wagombea wenzangu wawili mmoja wa CHADEMA na mwingine wa ACT wametangaza hawagombei na hapa mtaani kwetu hilo linatambulika kwa wote hivyo mie napita bila kupingwa ingawa sio kwa heshima kama nilivyopenda mie.
Kama hujatangazwa mshindi bado hujapita bila kupingwa
Maana yake hao jamaa bado wapo mchezoni
Jaribu tu kulala mpaka siku ya uchaguzi hutaamini masikio yako
 
Back
Top Bottom