Chama changu CCM tunajitengaje na aibu hii? Gamba limeondoka au limerudi kwa kasi?

Puma yetu

Senior Member
Sep 23, 2016
111
125
Hapa nazungumzia uchaguzi wa kura za maoni kuwapata wagombea ubunge, rushwa imetamalaki kila mahali.Wajumbe wa mikutano mikuu ya wilaya maeneo mengi wamepiga kura kwa kupewa rushwa sana.

CCM tunapenda sana kusema kila kitu au malalamiko yasiwe mitandaoni na badala yake yawasilishwe kwenye chama, it is too late.Naomba Majimbo yote uchunguzi ufanyike kwa kina maana rushwa imegawiwa kama njugu hasa kwa kutumia MAWAKALA wa mitandao ya simu ambapo huwezi kuona moja kwa moja jina la mtoa rushwa na utaona la wakala tu. Wote waliopitishwa kwa rushwa wakatwe bila huruma

Viongozi wetu wa chama taifa mnayo jukumu zito kuondoa mdudu huyu.Tunataka chama chetu kua kipya
 
Kuna mmoja kule Kanda ya Kaskazini pamoja na uchanga wake kwwnue siasa amepata kura 333, kila siku habari zake zilikuwa zinasambaa jinsi anavyogawa rushwa kwa wajumbe.
 
Hebu subirini. Kwamba Ndugulile ana mpunga mrefu kumzidi Makonda? Au Furaha ana mpunga mrefu kumzidi Gwajima?
 
Kwa nini mwandishi anapenda Sana mambo ya kuzusha?? Mambo ya uwongo uwongo??

Na kama ni kweli alishindwa vipi kuwatonya Takukuru?
 
Kuna mmoja kule Kanda ya Kaskazini pamoja na uchanga wake kwwnue siasa amepata kura 333, kila siku habari zake zilikuwa zinasambaa jinsi anavyogawa rushwa kwa wajumbe.
Usihofu. Dawa yake ipo Kamati Kuu. Wote waliotoa rushwa wanajulikana. Wagombea wanaokubalika na wananchi ndo majina yao yatarudi, waliopigiwa kura na wajumbe wa matawi kwa kuhonga itabakia historia kwao.
 
Shithole countries.

Nini motive yako unapotoa rushwa ili upate nafasi flani, utakuwa una nia njema kweli? sidhani.

JESUS IS LORD!
 
Kwa nini mwandishi anapenda Sana mambo ya kuzusha?? Mambo ya uwongo uwongo??

Na kama ni kweli alishindwa vipi kuwatonya Takukuru?
Wewe ni wa kuonea huruma kwa sababu huelewi lolote bora kujikalia kimya tu. Umeambiwa tukio linapangwa ndani ya dakika 2, Mgawa pesa anawaanda wajumbe anawapigia simu wajikusanye pamoja,wakishakaa pamoja eneo flani anapita hapo kama upepo na piki piki au gari isyokua yake ya siku zote na kugawa pesa dakika 1 na kusepa fasta,hao TAKUKURU mpaka waje wapokee simu na wafike eneo la tukio saa ngapi?

Hivi mlienda shule kusomea ujinga au nawe ni mtoa rushwa ndio maana unatetea ujinga?
 
Usihofu. Dawa yake ipo Kamati Kuu. Wote waliotoa rushwa wanajulikana. Wagombea wanaokubalika na wananchi ndo majina yao yatarudi, waliopigiwa kura na wajumbe wa matawi kwa kuhonga itabakia historia kwao.
Washughulikiwe wote hawa wapuuzi sana wanatuchafulia nchi
 
Hebu subirini. Kwamba Ndugulile ana mpunga mrefu kumzidi Makonda? Au Furaha ana mpunga mrefu kumzidi Gwajima?
Maeneo machache sana watu wanapita kwa haki, poa kuna kuzidiana ujanja katika kutoa rushwa we hujui. Wewe hujui, Makonda ana uzoefu gani na siasa za majimboni?
 
Usihofu. Dawa yake ipo Kamati Kuu. Wote waliotoa rushwa wanajulikana. Wagombea wanaokubalika na wananchi ndo majina yao yatarudi, waliopigiwa kura na wajumbe wa matawi kwa kuhonga itabakia historia kwao.
Kwa hiyo mtu mwenye tuhuma za rushwa adhabu yake ni kukatwa jina tu?

Kama chama kina taarifa zao na kutoa/kupokea rushwa ni jinai, kwa nini wasichukuliwe hatua kwa mujibu wa sheria?
 
Umeambiwa tukio linapangwa ndani ya dakika 2, Mgawa pesa anawaanda wajumbe anawapigia simu wajikusanye pamoja,wakishakaa pamoja eneo flani anapita hapo kama upepo na piki piki au gari isyokua yake ya siku zote na kugawa pesa dakika 1 na kusepa fasta,hao TAKUKURU mpaka waje wapokee simu na wafike eneo la tukio saa ngapi?
Kwa mtindo huu SASA ni hatarii πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚

Daaah!! πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ Hapana aisee

Takukuru wanakazi, CCM nooouuma haswaa!
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Kwa hiyo mtu mwenye tuhuma za rushwa adhabu yake ni kukatwa jina tu?

Kama chama kina taarifa zao na kutoa/kupokea rushwa ni jinai, kwa nini wasichukuliwe hatua kwa mujibu wa sheria?
Mbinu za kutoa rushwa zipo nyingi sana. Unapomchukulia mtu hatua za kisheria lazima uwe na ushahidi wa moja kwa moja na usio na shaka. Ndo maana TAKUKURU wakati mwingine hutumia fedha za moto kuwakamata watoa rushwa.

Kwahiyo, hatua ya chama kuwakata ni hatua nzuri sana kupunguza vitendo vya rushwa. Kwasabb mtu anajua hata nisipoonekana lakini ikijulikana tu kwamba nilishinda kwa kutoa chochote basi nitakatwa.
 
Kamati kuu kweli kabisa iangalie waliopita kwa kura nyingi Kuna mambo mazito ya kushangaza na kutia kinyaa yametokea huku majimboni
 
Maeneo machache sana watu wanapita kwa haki, poa kuna kuzidiana ujanja katika kutoa rushwa we hujui. Wewe hujui, Makonda ana uzoefu gani na siasa za majimboni?
Ingawa ni katibu wa uhamasishaji wa uvccm zamani naamini Makonda hana uzoefu na siasa za majimboni
 
Hivi mlienda shule kusomea ujinga au nawe ni mtoa rushwa ndio maana unatetea ujinga?
Unamaanisha Kwamba mnaotoa Rushwa Kwa mtindo mpya ndio mlienda shule kusomea welevu siyo?

πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚

Kwa hapo Bora nisomee Ujinga aisee
 
Back
Top Bottom