Chama cha Wanaume Walala hoi Tanzania (CWWT) kinasisitiza hili wakati huu wa Sikukuu

KOROE

Member
Dec 6, 2017
58
150
Kwa heshima na taadhima, sisi wanaume walala hoi, tunaoishi kwa ujanja ujana hapa town, na ukibahatika kupata mbebee mkali basi lazima umkojoze ili asikuache maana akiomba hela ataambulia maumivu ya kichwa kwa maelezo marefu kama zile essay za history form 6, mwisho holaa... Sasa huu wakati wa sikukuu ndo mara nying huwa wakati mgumu sana kwetu maana hata mbebe ukimkojoza vipi atataka japo outing.. Basi tutumie mbinu hizi mubashara kabisa ili kukwepa kuumbuka...

1.Huu ndo wakati sahihi wa kwenda kanisani tena sala zote na kusali kwa bidii sana ili wakati wa sikukuu umvute mbebee wako kanisani, kuanzia mkesha ule wa tar.24 usiku na tar.25 mchana kanisani then tar.25 usiku unasema umechoka upumzike hivyo hivyo tar.31 alaf tar.1 jan.

2.Ni muda muafaka wa kuulizia ulizia viwanja kwenye simu ili aone hela yako inatumika sana kwenye kununua vitu kama viwanja hivyo basi imjie huruma sikukuu hii asikukamue tena.

3.Toa toa mifano ya ndoa au mahusiano yaliyovunjika wakati huu wa sikukuu hasa ukionesha chanzo ni mwanamke kung'ang'ania vitu vikubwa wakati wa sikukuu kama zawadi za bei kubwa sana kuliko uwezo wa mume wake au mpenz wake.

4.Ukionaje sio mbaya ukapanga safari kwenda kijijini ukisisitiza ni utamaduni wenu kusheherekea sikukuu nyumbani na msisitize kwa kuwa atabaki peke yake hakuna sababu ya kupendeza, sasa apendeze amuone nani, au atoke out ili iweje wakati wewe haupo..

5.Jitahidi hom kama una tv au radio weka stesheni zile za dini ili kukwepa matangazo ya show ambazo anaweza kukushinikiza muende mkakae viti virefu.. stesheni za dini muda wote zitatangaza habari za bikra Maria na kuzaliwa kwa Yesu huku zikisisitiza watu wabaki majumbani kwao wakati wa sikukuu sio wa kufanya uovu.. msisitize hilo la uovu.

Pamoja tunajenga chama.

KOROE....
 

kwabwina

Senior Member
May 29, 2016
128
250
Dah ,we jamaa Haya we n Nani katika hicho chama? na makao makuu yako wapi?
 

jay311

JF-Expert Member
Oct 21, 2012
2,941
2,000
Hahaha... Chama kipyw hichi, kinaweza kuwa vhama cha pili baada ya kile cha CHAPUTA
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom