CHAMA cha Wanasheria wa Tanganyika champinga Kikwete kuhusiana na muswada wa Katiba mpya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHAMA cha Wanasheria wa Tanganyika champinga Kikwete kuhusiana na muswada wa Katiba mpya

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Nov 27, 2011.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Nov 27, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,691
  Likes Received: 82,611
  Trophy Points: 280
  Muswada wa Katiba: Kikwete sasa njia panda

  na Grace Macha, Arusha
  Tanzania Daima


  CHAMA cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS) kimemtaka Rais Jakaya Kikwete kuwasikiliza wananchi wanaopinga Muswada wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya mwaka 2011 kwa madai kuwa kulikuwa na ukiukwaji mkubwa wa sheria za nchi, taratibu na kanuni za Bunge, na kimesema wataenda mahakamani kufungua kesi ya Kikatiba kuupinga iwapo Rais atausaini.

  Rais wa chama hicho , Francis Stolla, aliyasema hayo juzi alipokuwa akitoa mada katika mjadala juu ya ushiriki wa wananchi wa jamii za wawindaji, wakulima, wafugaji, warina asali na waokota matunda asili kwenye mchakato wa uundwaji wa Katiba mpya ulioandaliwa na jukwaa la umoja wa mashirika yasiyo ya kiserikali ya wafugaji na wakusanya matunda ya asili (PING's Forum) uliofanyika mjini Arusha.

  Alisema kuwa Rais Kikwete anapaswa kuliepusha taifa na vurugu kwa kusilikiliza maoni ya wananchi wengi kwa vile haikuwa haki kuchukua maoni ya wananchi wachache kwenye mikoa ya Dar es Salaam, Dodoma na Zanzibar.

  "Rais asisaini muswada huo kuwa sheria kwa sababu ni kweli kwamba maoni yaliyokusanywa kwenye mikoa ya Dodoma, Dar es Salaam na Zanzibar ni ya wachache tu na bado tulishuhudia vurugu kubwa hadi Katiba ikichanwa ….tunataka haki ya wananchi kutoa maoni iwe kweli si kwenye makaratasi na wala wananchi wasinyimwe kwa kuhisi kuwa wakipewa fursa hiyo hawataitumia," alisema Stolla.

  Alisema kuwa wameunda kamati maalum ya wanasheria watano inayoongozwa na Prof. Angelo Mapunda wa Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam kwa ajili ya kufanya utafiti juu ya vipengele vya sheria vilivyokiukwa jambo litakalowawezesha kwenda mahakamani endapo Rais Kikwete ataamua kusaini mswada huo.

  Rais huyo wa TLS alitaja baadhi ya mapungufu hayo kuwa ni suala la kuwapo kwa miswada miwili ambapo ule wa lugha ya Kiingereza uliowasilishwa bungeni mwezi wanne mwaka huu na kusomwa bungeni mara tatu wakati ule wa Kiswahili uliwasilishwa bungeni kwa mara ya kwanza mwezi Novemba mwaka huu na ukapitishwa ukiwa umesomwa mara mbili jambo alilodai kuwa ni kinyume cha sheria.

  Alisema kuwa muswada huo uliopitishwa unaendelea kuminya haki ya wananchi katika kutoa maoni kwani kimewekwa kipengele ambacho endapo mwananchi atatoa maoni ya kupinga vipengele ndani ya muswada huo basi anaweza kushtakiwa kwa kutenda kosa la jinai ambalo adhabu yake itakuwa kifungo cha miaka mitatu jela.

  Stolla alisema kuwa hata muundo wa Bunge la Katiba una kasoro kwa kile alichosema kuwa kwa namna lilivyoainishwa ndani ya muswada huo umekaa kisiasa zaidi kwani idadi ya watu kutoka makundi mengine mbali ya kuwa hawajaainishwa bayana lakini ni ndogo hivyo kuna hatari Katiba hiyo ikaundwa kwa kuzingatia na kukidhi matakwa ya wanasiasa zaidi.

  Alisema kuwa baada ya kosa hilo kufanyika kimbilio pekee lililobaki kuhakikisha muswada huo unarudishwa bungeni kisha kwa wananchi ili wapatiwe fursa ya kusikilizwa ni kwa Rais Kikwete kutousaini.
  "Hatutanyamaza tutasema mapungufu yaliyopo kisheria, sisi kama wanasheria na wanaharakati hatutengenezi fursa zozote za kiuongozi wa kisiasa, tunasema Rais awasikilize wananchi aurudishe muswada huo bungeni, lakini akikataa tutaenda mahakamani," alisema Stolla.

  Bunge: Muswada wa Katiba unaweza kubadilishwa

  Kwa upande wake Bunge limesema kuwa Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Katiba ya mwaka 2011 unaweza kubadilishwa au kufutwa wote endapo itaonekana kuna sababu za msingi za kisheria kufanya hivyo.

  Taarifa iliyotolewa jana na Idara ya Habari, Elimu kwa Umma na Ushirikiano wa Kimataifa ya Bunge, imebainisha kuwa ikiwa muswada huo utasababisha mtazamo tofauti, unaweza kufanyiwa marekebisho kwa kuzingatia kanuni na taratibu kama inavyokuwa wakati mwingine wowote linapokuja suala la kurekebisha sheria za nchi.

  Hata hivyo, taarifa hiyo imesema kuwa Bunge halikuvunja kanuni wala sheria yoyote ya nchi wala sababu ya msingi kuzuia muswada huo usisomwe kwa mara ya pili, kwa kuwa ulikidhi mahitaji yote kikanuni.

  Taarifa imesema kuwa muswada huo ni halali na ukiwekwa saini na Rais utaendelea kusimamiwa na kutekelezwa kama sheria nyingine yoyote.

  Ilisema muswada huo ni kama mwingine wowote uliowahi kupitishwa na Bunge; na ni wa kawaida ambao unaweka utaratibu wa kuwafikia wananchi, kuwasikiliza, kupata utashi wao juu ya mapendekezo ya kuandika Katiba mpya ili kila Mtanzania aweze kushirikishwa kwa wakati husika moja kwa moja.

  Taarifa hiyo imebainisha kuwa Bunge limewashangaa baadhi ya wabunge waliosusia kikao cha kujadili muswada huo kwani wamewanyima fursa wananchi hao kuwakilisha maoni yao.

  Ilibainisha hakukuwa na sababu za msingi kwao kulalamika wakati ikizingatiwa kwamba kambi zote ziliwasilisha na kupitisha mapendekezo ya muswada huo ili wananchi waulizwe kuhusu wanachokitaka kiingizwe katika Katiba mpya.

  Iliongeza kuwa muswada huo hauhitaji ushiriki wa moja kwa moja wa wananchi isipokuwa kupitia kwa wawakilishi wao.
  Taarifa hiyo ilibainisha kuwa muswada huo ulilenga katika kuweka chombo ambacho kitafanya kazi ya kuchukua maoni ya wananchi ili kuyapeleka katika Bunge la Katiba, ambalo, litakuwa na nafasi ya uwakilishi wa kila mtu.

  Imesema Bunge limeuchambua muswada wa sheria na kuupitisha kuwa sheria na sio muswada wa kubadilisha Katiba kwa kuwa Katiba sasa haitobadilishwa, bali itaandikwa upya na serikalil iliyo madarakani kwa sasa na Bunge lake.

  Mapema wakichangia katika mjadala huo jana, wengi wa washiriki walielezea mapungufu ya sheria katika ugawaji na umilikaji wa ardhi kwenye maeneo ya wafugaji, wawindaji na waokota matunda ambapo walitaka haki zao ziainishwe kwenye Katiba tofauti na sasa ambapo mara kwa mara wamekuwa wakiondolewa kwenye maeneo yao kuwapisha wawekezaji kwa kile wanachoambiwa wanaondolewa kwa maslahi ya umma.

  Aidha walitaka Katiba mpya itambue uwepo wa Wamasai ndani ya Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro na kuendesha kilimo cha kujikimu, kujenga zahanati na shule badala ya kuwaachia uhuru wageni kujenga mahoteli na nyumba nyingine katika hifadhi hizo.

  Katika hatua nyingine Baraza la Wanawake wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Bawacha), limemshukia Spika wa Bunge Anne Makinda, kutokana na kupitisha Muswada wa Sheria ya Kuunda Katiba Mpya ambao ni kandamizi kwa wanawake nchini.

  Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Kaimu Mwenyekiti wa baraza hilo, Susan Lyimo, alisema Spika yuko kimaslahi ya chama tawala (CCM), badala ya wanawake.
  "Tunawaomba wanawake wote watuunge mkono kwani athari za muswada ni nyingi na muathirika mkubwa atakuwa mwanamke, kitendo cha Makinda sio cha kiungwana mbele ya wanawake na umma wa Watanzania," alisema.

  Alisema uamuzi wa Spika Makinda na Waziri wa Katiba na Sheria, Celina Kombani, kukataa maoni ya wanawake na hatimaye kupitisha muswada huo ni jambo la kulaaniwa.

  Susan alisema suala la Katiba ni nyeti, na si mali ya CCM bali ya Watanzania wote hivyo yasiruhusiwe makundi ya watu wachache wenye malengo ya kulinda maslahi yao kuamua mustakabali wa nchi.

  Alisema muswada huo ni janga kwa taifa kwani unaweka wazi kwa mtu atakayetoa elimu ya uraia kuhusu sheria hiyo atafungwa miaka mitatu.

  Akifafanua juu ya upotoshwaji na propaganda zilizofanywa na CCM na CUF alisema hali hiyo inaweza kuleta machafuko ambayo athari kubwa itakuwa kwa wanawake, watoto na wananchi wenye ulemavu. Na propaganda zilizofanywa na wabunge wanawake juu ya Muswada huo ni za kupuuzwa.
   
 2. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #2
  Nov 27, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Tatizo la uongozi kwa mazoea ndio kama hivi; kila kitu watu kufanyia mzaha hadi na Muswada unaogusia MOYO wa Taifa kwa maana ya Katiba.

  Bila busara za kina kurudisha UUNDWAJI WA KATIBA MPYA kwa wananchi wenyewe ni wazi kwamba kutaibuka zogo kubwa la Mgogoro wa Kikatiba na hata kuhitajika baadhi ya watendaji wa ngazi za juu serikalini kuhitajika kukaa pembeni kwa kukiuka Katiba ya sasa.
   
 3. ntamaholo

  ntamaholo JF-Expert Member

  #3
  Nov 27, 2011
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 10,148
  Likes Received: 2,109
  Trophy Points: 280
  No way out, kupigana ndilo suluhisho letu watanzania tunaohitaji kuwafanya wanasiasa, watumishi wa umma, wanaharakati kuongozwa kwa matakwa ya jamii yaani wote kuwajbika kwa jamii. Tukiuwana, watakaobaki wataengeneza kitu kitakachowafaa vizazi vijavyo
   
 4. Bornvilla

  Bornvilla JF-Expert Member

  #4
  Nov 27, 2011
  Joined: Feb 17, 2011
  Messages: 925
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 35
  Upupu mtupu! Sasa nahisi kuwa Tanzania hakuna wanasheria,na kama wapo basi ni wapotoshaji. Wanapotosha kwa maslahi ya nani? Hebu ona! Wanatumia mwanya wa watanzania kutopenda kusoma na kupenda kusikiliza zaidi kuwapotosha. Jamani huu ni muswada wa tume itakayoundwa,bunge la katiba na kazi zao! Sasa mbona mwatwambia ndio Muswada wa sheria(katiba)? Ndg zanguni nawaombeni kama huo muswada hamjausoma mwende mkausome halafu ndio mlete hoja zenu. Tuache kusikiliza sana badala yake tusome viandikwa ili tusipotoshwe. Kwenye suala la katiba kuna upotoshaji mkubwa sana na wananchi wameuamini.
   
 5. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #5
  Nov 27, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  TANGANYIKA LAW SOCIETY, CHADEMA, NCCR-MAGEUZI, UDASA, JUKWAA LA KATIBA, CUF, TLP: TUNAWAOMBENI KUPELEKA KESI JUU YA 'MUSWADA WA MAKINDA' MAHAKAMANI HARAKA

  dr Mashilila, ugomvi wetu namba moja ya ofisi ya Bunge ni kama ilivyoainishwa kwanye taarifa hiyo hapo chini penye wino mwekundu na wa kijani.

  Endapo utakua umechanganya kidogo madesa juu ya swala hili nyeti kitaifa, tunaomba kukufahamisha kwamba;

  1. Bunge kazi yake ni kutunga sheria kama ambavyo WANANCHI KWA WINGI WETU tunavyotaka (Kuunda Katiba HAPANA)

  2. Serikali kwa mana ya the Executive wao kazi yao Utendaji wa KILA SIKU kwa kuzingatia sheria zilizopo (Kuunda Katiba HAPANA)

  3. Mahakama kazi yao ni kusimamia HAKI kwa mujibu wa sheria zilizopo (Kuunda Katiba HAPANA)

  4. Wananchi kazi yetu ni KUSHIRIKI NA KUDAI KUSHIKISHWA katika mambo yote hayo hapo juu kwa kuwa kila atendaye lolote hapo juu anfanya hivyo kutokana tu na baraka za MAMLAKA zetu KAAMA AMBAVYO TULIVYOZIKASIMU KWA na wala si vinginevyo.

  Lakini tukija kwenye hili swala nyeti la UUNDWAJI WA KATIBA hiyo hapo sasa haswaaa ndio kwenyewe JUKUMU LETU MAMA, LA MSINGI KIKATIBA, NA NI JUKUMU LISILOKASIMIKA kwa mtu yeyote, chombo wala kikundi kulitekeleza bila ya uwepo wetu kama Mabosi na Madereva washika ushukani TOKA MWANZO KABISA HADI KIKOMO CHA mchakato wote huu.

  Hivyo basi, kwa kuwa ni sisi wananchi peke yetu ndio tunaoingi katika maeneo yote hayo manne bila kuzuiliwa na na Katiba, tunasema hatujashirikishwa lolote juu ya huu Muswada wa Makinda n kwamba hadi sasa hatujui kwamba kati ya Miswada miwili (Moja ya Kiingereza na Nyingine tofauti kabisa ikiwa katika lugha ya Kiswahili) hajafahamu bado kwamba ni muswada upi huo uliozaa hako k sheria ka-kupelekwa kwa Rais Kikwete.

  Wala hatujajua taratibu zilizotumika katika muswada gani kati ya hizo mbili kutushirikisha sisi wananchi na kwamba NI NAANI HUYO HASA aliyekua akisimamia, kuhakiki na kuhakikisha kwamba kweli maoni yetu kama umma wa Tanzania na wala si maoni ya baadhi tu ya wanasiasa NDIYO KWELI yameingizwa katika muswada huo kabla ya kuwa sheria.

  Pamoja na mapungufu kede kede tena yenye uwezekano mkubwa wa kusabnabisha vurugu na hatimaye umwagaji damu nchini mwetu, sisi (Wana-JF) kama sehemu ya wadau wa katiba tunapenda kuwata Tanganyika Law Society na au taasisi nyingine yoyote ile nchini WAKACHUKUE HATUA ZA HARAKA NA ZA KISHERIA kupeleka swala hili mahakamani maramoja na kwanza TUKAANZE NA COURT INJUNCTION juu ya zoezi lote hili haraamu mpaka mchakato mzima uwe umetokana na sisi na kusimamiwa na sisi wananchi na wala si vinginevyo.


   
 6. kaburungu

  kaburungu JF-Expert Member

  #6
  Nov 27, 2011
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 1,603
  Likes Received: 2,458
  Trophy Points: 280
  Hao TLS nao wataambiwa kuipeleka serikali mahakamani Kunahatarisha amani kwa sababu mahakamani kutakuwa na msongamano wa watu, hivyo alsa-babu! Wanaweza leta machafuko!

  Nchi hii mi hata sielewi nani mtetezi wa kweli wa watanzania hawa waliopo wakitishwa tu, wamefyata mkia, mfn ni hao akina Deusi kibamba!

  Kichefuchefu!!!!!!!!!
   
 7. TANMO

  TANMO JF-Expert Member

  #7
  Nov 27, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 8,919
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  Kelele zote hizi lakini Jamaa hawasikii kitu?
  Kweli Madaraka matamu..!
   
 8. Malipesa

  Malipesa JF-Expert Member

  #8
  Nov 27, 2011
  Joined: Aug 23, 2011
  Messages: 310
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Mimi nionavyo kama itatengenezwa katiba isiyokidhi mahitaji ya wengi ama katiba mbovu basi haitadumu kwa muda mrefu, itafika mahali tutahitaji tena katiba mpya hata kama nia baada miaka 10, Nomba Mungu awajaze viongozi wetu busara ikatengenezwe katiba nzuri itakayodumu kwa muda mrefu sana ikifanyiwa marekebisho madogo madogo tu.

  Hivi kwani Spika na Wabunge wake hawasikii kelele zinazopigwa na wanaharakati na watu wengine kupinga mswada huu wa
  kutengeneza katiba mpya? Eti utasikia serikali sikivu! Kivipi? King'ang'anizi cha nini? Kuna kitu gani kilichofichika ndani yake? Kuna maslahi ya nani yako ndani yake? Kwani ikirekebishwa ikawa tofauti na sasa kuna madhara gani?

  UKIONA JAMBO LINAPIGIWA KELELE SANA KUAWA MAKINI SANA, VINGINEVYO...................
   
 9. RUV ACTVIST.

  RUV ACTVIST. JF-Expert Member

  #9
  Aug 3, 2014
  Joined: Jan 14, 2012
  Messages: 471
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  Watu wanarumbana juu ya nini hasa wajibu wa BMK ,nini hasa tafsiri ya haya maneno mawili.....KUBORESHA na KUBADIRI......majaji na mahakimu tusaidieni.....toweni tamko au tafsiri ya hii sheria ya mabadiliko ya katiba,tumjue mchawi ni nani.
   
 10. Not_Yet_Uhuru

  Not_Yet_Uhuru JF-Expert Member

  #10
  Aug 3, 2014
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 1,305
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Majaji na mahakimu with wamejaa woga wamekuwa mafarisayo wakuu...wanasimama kulinda watawala waliojaa dhuluma na sio kulinda umma unaoihangaikia haki. Ni aibu ya taifa na mhimili yake isiyojitambua kuwa huru.
   
 11. SaidSabke

  SaidSabke JF-Expert Member

  #11
  Aug 3, 2014
  Joined: Sep 28, 2006
  Messages: 1,969
  Likes Received: 223
  Trophy Points: 160
  Hao ndio waliochemsha s I lolote ni ukoko tuu hajui mustakabali wa nchi kisiasa kwa serikali tatu
   
 12. Bavaria

  Bavaria JF-Expert Member

  #12
  Aug 3, 2014
  Joined: Jun 14, 2011
  Messages: 44,100
  Likes Received: 11,250
  Trophy Points: 280
  Miaka yote walikuwa wapi wnakuja leo?
   
Loading...