Chama cha wanasheria Tanzania bara (TLS) chaendesha mafunzo ya wakufunzi wa wasaidizi wa kisheria

Vedasto Prosper

Verified Member
Jul 30, 2013
92
125
TLS inaendesha mafunzo ya siku tano yaliyoanza leo tarehe 20/8/2018 na yanayotarajiwa kumalizika tarehe 24/8/2018. Mafunzo hayo yameandaliwa na Chama cha Wanasheria Tanzania Bara (TLS), kwa kushirikiana na Wizara ya Katiba na Sheria, na Shule ya Mazoezi ya Sheria (Law School of Tanzania). Lengo la semina hii ni kuwajengea uwezo wakufunzi wa mafunzo kwa Wakufunzi wa Wasaidizi wa Kisheria (Paralegals) Tanzania nzima.
2c2dd889-34d1-4718-a385-a52269728082.jpeg

Akifungua mafunzo hayo Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Ndugu Amon Mpanju amesema Sheria ya msaada wa kisheria pamoja na mambo mengine imetambua kwa mara ya kwanza wasaidizi wa kisheria kuwa ni moja ya kada katika tasnia ya kisheria. “Sheria imeweka bayana utaratibu wa namna ya kuwaratibu na kuwasimamia wasaidizi wa kisheria. Pia seria imeweka masharti anayopaswa kuwa nayo mtu anaetaka kusajiliwa kuwa msaidizi wa kisheria ambapo moja ya mashari hayo mtu huyo anapaswa kupatiwa mafunzo yatakayoratibiwa na Msajili wa watoa Huduma ya Msaada wa kisheria. Naamini mafunzo haya tunayoyatoa wiki nzima kwa lengo la kuwaandaa kuwa wakufunzi wa wasaidizi wa kisheria nchini”.

Matarajio ya Wizara, Chama cha Wanasheria Tanzania Bara (TLS), Chuo cha Mafunzo ya Kisheria kwa Vitendo ni kwamba mtatumia muda wenu wa siku tano vizuri na kuelewa maeneo muhimu ambayo wasaidizi wa kisheria wanatarajiwa kufundishwa na kuelewa ili huduma wanayoenda kuitoa kwa jamii iwe ni huduma bora.
3026c635-95ea-4069-990d-82c4e942d91e.jpeg

Sheria imenainisha kazi wanazopaswa kuzifanya na zile walizokatazwa kuzifanya hivyo kwa mafunzo haya sasa hatutegemea wasaidizi wa kisheria kuingia kwenye migiogoro na mawakili na vyombo vya utoaji haki kwani mtawasaidia kuuelewa majukumu yao kisheria na yale makatazo yote.

Katika kutenda mambo yoyote kuna wale ambao hukiuka masharti yaliyowekwa, hivyo tunazo kanuni za maadili za watoa huduma ya msaada wa kisheria. Ni matumaini yetu kwamba kanuni hizi zitafafanuliwa kwa kina kwa wasaidizi wa kisheria kuzifahamu na kizifuata.

Wakufunzi hawa wawe mabalozi wema katika kuwaelekeza wasaidizi wa kisheria katika kufuata masharti ya sheria na kufahamu mambo mengine ya muhimu katika kusaidia jamii ambayo haina uwezo kufahamu wajibu na haki zao. Wasaidizi wa kisheria wakijengewa misingi mizuri basi tutarajie hata migogoro na mashauri katika Mahakama zetu yatapungua kwa kasi kubwa.


Akiongea katika hafla hiyo Mkurugenzi Mtendaji Kaleb Gamaya amesema, “Mafunzo haya yanatolewa kwa wakufunzi 60, na watapata mafunzo hayo kwa awamu tatu na tumeanza na wakufunzi 20 katika awamu hii ya kwanza.” Tunawapongeza Legal Aid Facility (LSF) kwa kutuwezesha kuwajengea uwezo kwa wakufunzi hao kwani mahitaji ya msaada wa kisheria katika jamii hasa vijijini ni mkubwa sana. Wananchi hasa wa kipato cha chini wamekuwa wakiangaika kupata msaada wa kisheria ikiwemo kupata wakili, lakini huduma hiyo sasa itasogezwa karibu kabisa kwa kuwatumia wasaidizi wa kisheri (Paralegals) ambao wapo karibu kila kata ya Tanzania Bara.

TLS tunashirikiana na LSF katika kuwafunza wakufunzi wa wasaidizi wa Kisheria (Paralegal) ili elimu hii ishuke mpaka kwa wasaidizi hao wa kisheria kwa manufaa ya wananchi ili waweze kupata Elimu ya Kisheria, Ushauri wa Kisheria, na pia waweze kupata utatuzi wa migogoro midogo midogo kabla ya kufikia ngazi za juu za kimaamuzi.
115369b8-54fc-4da6-8ccb-40ee210f1506.jpeg
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom