Chama cha wanasheria Tanganyika(TLS) mnakwama wapi? Mnachangisha mabilioni lakini mikutano yenu haiko laivu Facebook,Twitter wala Youtube!

chiembe

JF-Expert Member
May 16, 2015
11,975
20,612
Kuna taasisi zinajiendesha kizamani sana na utawasikia viongozi wake wakihimiza uwazi katika shughuli za umma na wanadai Bunge Laivu, charity begins at home

TLS kinachangisha michango ya mabilioni na kinapata misaada ya kifedha kutoka nje ya nchi.

Leo wanafanya mikutano yao kwa mujibu wa sheria, mikutano hiyo haiko laivu, ni kama mikutano ya cult fulani, Ni hawahawa huwataka wanachama wasiohudhuria watumie proxy, hata anayetumia proxy anahaki ya kujua mnajadili nini, kuweni laivu

TLS ni chama kinachowakilisha maslahi ya umma, umma unataka kujua mnaendeshaje mambo yenu, kuna vyombo vingi vya habari na mitandao ya kijamii inayoweza kuwasaidia kuwasiliana na umma.

Kuna Youtube-Live

Facebook-Live

Facebook wwatch party

Twitter-Live

Hata pasco mayalla pia ana kampuni yake PPR ambayo ingeweza kuwasaidia katika mawasiliano na hata vipindi vya kimkakati katika prime time ambapo mngejieleza kwa umma kuhusu kilichowakutanisha

Badilikeni,sasa hivi mdau wa ubeligiji angekuwa anakunywa waini yake huku anaangalia laivu
 
Hata wageni rasmi katika mikutano hiyo huwa ni watu wasio na vyeo vikubwa nchini (viongozi wa mihimili), inakosa hadhi ya kitaifa wakati TLS ni taasisi kubwa kabisa kitaifa. Na hii nafikiri ilianza kabla hata ya kupata uongozi unaoonekana una usiasa
 
Niliwahi kuliona hilo but very nice umeleta uzi, hawa jamaa kiukweli bado wapo old age japo wanatumia zote na update laws.
 
Tutanue mjadara tuangalie na taaluma zingine...bodies ya wahasibu(NBAA), ya ugavi (PSPTB), ya mabenki (TIOB), ya wakaguzi hesabu za ndani ( IIA), wahandisi, ya iT (CISCO) na nyingine nezo nyingi ...haziko laivuu
 
ilikuwa inarushwa na watetezi tv ila kwa kusua sua sana...inapaswa waji upgrade aisee, sio kuita tu waandishi
 
Back
Top Bottom