Chama cha Wanasheria nchini kubaki na jina la "TANGANYIKA" LAW SOCIETY

MBATATA

JF-Expert Member
Jul 23, 2013
542
209
Muniwie radhi kama hili lilishatolewa maelezo huko nyuma. Baada ya Muungano unaosifika sana jumuiya nyingi za kijamii, kisiasa, kiimani na hata kitaaluma zililiridhia kubadili utambulisho wa jumiya hizo na kuchukua majina ambayo yanaendana na utaifa wa ki -Tanzania.
Hata hivyo Chama cha Wanasheria nchini kimeendelea kubakia na jina lake la "TANGANYIKA " LAW SOCIETY, ambalo wengi tunapata shida kuelewa msingi wake, na hasa vijana amabao hawana ufahamu wa kutosha kuhusu mambo ya Tanganyika zaidi ya kuwa ndio taifa liliopata uhuru kabla ya muungano. wa Tanzania. Je Hili limekaaje?
 
Good question.....
 
Mbona hata ZLC - zanzibar law society ipo! Muungano ni wa NCHI mbili au sio?
 
Muniwie radhi kama hili lilishatolewa maelezo huko nyuma. Baada ya Muungano unaosifika sana jumuiya nyingi za kijamii, kisiasa, kiimani na hata kitaaluma zililiridhia kubadili utambulisho wa jumiya hizo na kuchukua majina ambayo yanaendana na utaifa wa ki -Tanzania.
Hata hivyo Chama cha Wanasheria nchini kimeendelea kubakia na jina lake la "TANGANYIKA " LAW SOCIETY, ambalo wengi tunapata shida kuelewa msingi wake, na hasa vijana amabao hawana ufahamu wa kutosha kuhusu mambo ya Tanganyika zaidi ya kuwa ndio taifa liliopata uhuru kabla ya muungano. wa Tanzania. Je Hili limekaaje?
Tanganyika Law Society ni chama cha Wanasheria kwa upande wa Tanganyika tu,(Bara), hakifiki Zanzibar,kwa hiyo sii cha muungano, kama ulitaka kiitwe Tanzania Law Society ingebidi kiwe cha Tanzania nzima (Bara na Visiwani). Ila Tanganyika bado linatumiwa na wengi, mf: Tanganyika Farmers Association, Interntnl School of Tanganyika, etc.
Tanganyika is our True Identity, whether we were born before or after the Union!
 
Tanganyika Law Society ni chama cha Wanasheria kwa upande wa Tanganyika tu,(Bara), hakifiki Zanzibar

Halafu walivyo watu wa ajabu leo utasikia wamejadili mambo ya uchaguzi wa Zanzibar wakati swala la uchaguzi si swala la muungano.Hilo swala lilitakiwa wakalijadili Zanzibar Law SOCIETY.Lakini wanasheria wetu leo wataamua kuvunja katiba wazi wazi na kuingilia mambo ya ndani ya Zanzibar kwa kuongelea jambo lisilo wahusu.

Kama ni cha wanasheria wa Tanganyika maswala ya Nchi ya Zanzibar kuyaleta nchi ya tanganyika mambo yasiyo ya muungano ni sawa? Hawavunji katiba ya nchi kwa kuyaongelea mambo ya nchi ingine ambayo hayamo ndani ya katiba?

Wanachokifanya sio kuingilia mambo ya ndani ya nchi ya Zanzibar?

Hicho chama wakitaka kukifanya chama cha siasa waende wasajili tu.Tulitegemea kama wanasheria wakae waongelee changamoto wanazopata wananchi kwa mawakili,mahakimu na uozo ulioko sekta yao ya sheria wao wanaleta siasa.

Ombi langu wazingatie katiba ya nchi.Wao ni wasomi wa sheria wasilete choko choko kwa kudandia vitu ambavyo si vya muungano.Hao akina Karume wakasome maada zao kwenye chama chao cha wanasheri cha kwao Zanzibar.Si wao wanasema Zanzibar ni nchi na ina kila kitu kuanzia sheria zao,jaji mkuu wao,chama chao cha wanasheria nk waende kwao.

Wanasheria watanganyika na nyie msilagaike namna hiyo usomi wenu uonekane kwenye uzingatiaji
 
Haswa!
Kwa mujibu wa madhumuni ya kutaka mambo yanayogusa pande zote za muungano Tanzania yapate jukwaa lenye Utanzania, basi chama hiki kingekuwa makini zaidi na kuunganisha malengo na matarajio katika utaifa huo, na kuongoza mijadala na makongamano husika. Ila kama TLS kinataka kutoa elimu, au kuwapa fursa wa Zanzibari (ambako huenda fursa kama hii huko kwao visiwani si rahisi), hilo ni suala la kuweka wazi! Haionyeshi upeo muafaka kuendelea kujitambulisha kama "Tanganyika ......' na kisha kuendeleza mihemko ya upande wa pili.
 
Ukimaliza kuhoji TANGANYIKA LAW SOCIETY UANZE KUHOJI ZIWA TANGANYIKA NA UWANJA WA MPIRA WA MIGUU LAKE TANGANYIKA STADIUN
 
Muniwie radhi kama hili lilishatolewa maelezo huko nyuma. Baada ya Muungano unaosifika sana jumuiya nyingi za kijamii, kisiasa, kiimani na hata kitaaluma zililiridhia kubadili utambulisho wa jumiya hizo na kuchukua majina ambayo yanaendana na utaifa wa ki -Tanzania.
Hata hivyo Chama cha Wanasheria nchini kimeendelea kubakia na jina lake la "TANGANYIKA " LAW SOCIETY, ambalo wengi tunapata shida kuelewa msingi wake, na hasa vijana amabao hawana ufahamu wa kutosha kuhusu mambo ya Tanganyika zaidi ya kuwa ndio taifa liliopata uhuru kabla ya muungano. wa Tanzania. Je Hili limekaaje?
Ndugu MBATATA
Tanzania ni Muungano wa baadhi ya mambo baina ya Tanganyika na Zanzibar.
Tanzania ina serikali mbili na mamlaka tatu za kisheria.
Mamlaka hizo ni 1.Mamlaka ya mambo ya Muungano, 2. Mamlaka ya mambo ya Tanganyika ambayo yanasimamiwa na Serikali ya Muungano (Dhana ya kuvaa joho la muungano inahusika hapa) na mamlaka ya mambo ya Zanzibar yanayoendeshwa na kusimamiwa na serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

Mahakama si jambo la Muungano,ingawaje Mahakama ya Rufaa imefanywa kuwa ni Jambo la Muungano

The article of Union between Tanganyika and Zanzibar ina vipengele vingi baadhi yake ni

And the said Parliament and Executive shall have exclusive authority in such matters throughout and for the purposes of the united Republic and in addition exclusive authority in respect of all other matters in and for Tanganyika.

(v) The existing laws of Tanganyika and of Zanzibar shall remain in force in their respective territories subject-

(a) to any provision made hereafter by a competent legislature;

Kama umeaminishwa Tanganyika haipo kwa sababu ya kuitwa Tanzania bara basi umeingizwa mjini.
Tanganyika imevaa koti la Muungano tu. Kwa hiyo Chama cha wanasheria hakifanyi kosa kubalia kuwa na jina hilo. Kwa sababu Sheria zinazotumika Tanzania bara(Tanganyika) ni sheria za Tanganyika.
 
sijui kwa nini watu wanakuwa wanafiki na kujifanya hawajui historia na wala hawajawahi kutana na kitu kama tanganyika.
 
Unajua Kuna mambo mengine siyo ya muungano na mengine yapo kwenye muungano, zamani, kwenye somo la geography kulikuwa pia Kuna maswali kwa ajili ya watu wa zanzibar, sijui siku hizi, mambo ya sheria, mambo ya afya, usafiri, mambo ya muungano ni machache tu nadhani yatakuwa manne au saba hivi. Cha muhimu ni kuwa Kuna mambo mengine hayapo kwenye muungano na mengine yapo, kumbuka wazanzibari huwa wanasema tanganyika imevaa koti la muungano, tafakari Sana hii sentensi.
 
Back
Top Bottom