Chama cha Wanajeshi wa Kikiristo - ASSOCIATION OF MILITARY CHRISTIAN FELLOWSHIPS (AMCF)

Kama kuna mzigo mzito kuubeba hapa duniani basi ni HISIA. Mtu ukiongozwa na hisia siku zote unakuwa mwepesi wa kuuliza maswali tata na kuomba majibu. Lakini cha ajabu, majibu yote unayopewa huwa hayatoshi kubadili hisia zako kwani ulishadhamiria kuamini unavyoamini.

Kinachowafanya mdhanie kuwa wanajeshi hawasali ni nini? Kinachowafanya mdhanie kila anayeshika silaha na kuongea suala la dini ana mtizamo wa ki-Al Shaabab ni nini? Kwenye majeshi yooote kuna Chapels ambao ndio wahudumu wa kiroho kwenye majeshi kwa upande wa wakristo. Sasa kinachofanya wanaoona ubaya kwa hilo waone ubaya ni dhamira zao.

Wakristo wana associations nyingi sana na zote ni kwa maendeleo ya jamii. Kuanzia jeshini, relief aids, education, health na hata ipo association of christian librarians sasa sijui cha ajabu nini. Au mlifikiri wanajeshi wakristo wakifa hawajaliwi mustakabali wao wa kiroho?

Tuwe na hoja za maana. Kama nia ni kulinganisha vitu mbona pale kunapokuwa na shughuli za maendeleo hamsemi kwa nini wana-volunteer na sisi hatu-voluntii?

Hisia za kinyonge ni zigo kubwa mithili ya ujinga

Kwani hiyo association ni kwa ajili ya kusali kusali si wanaenda kanisani?? mkuu mbona sikujakupata bado

Vipi waislamu wakianzisha association kama hiyo; mtakuwa mnasema the same language??

Mfumo kristo hadi jeshini twafaaaa...
 
teh teh hao ni alshabaab sorry LORD RESISTANCE ARMY:eyebrows::eyebrows:
 
Bana Hicho chama hakipo Jeshi la wananchi Tz. Nithibitishie kama kipo. Hizo tetesi kama za magazeti ya Udaku.
 
Kwani hiyo association ni kwa ajili ya kusali kusali si wanaenda kanisani?? mkuu mbona sikujakupata bado

Vipi waislamu wakianzisha association kama hiyo; mtakuwa mnasema the same language??

Mfumo kristo hadi jeshini twafaaaa...

Nakumbuka hata mimi nilipokuwa jeshini kwa mujibu wa sheria (JKT) tulikuwa na chama au unaweza kuita ushirika wetu na tulikuwa tunasali kama kawaida. Pia kulikuwa na chama cha waislam nao walikuwa wanakutana na wanasali na kuzungumza mambo yao ya dini yao.

Its quite logical, binadamu whether ni mwanajeshi, daktari, rubani, engineer etc, anamhitaji Mungu, na ana ruksa ya kukutana na wenzake katika kumuabudu na kujifunza juu ya Mungu ili mradi hawavunji sheria za nchi. Watajifunza vipi mambo ya muumba wao kama hawakutani? Hilo halina mjadala tunachokataa ni mfano wa Alshabaab ambao wao wanakutana na kupanga kuua watu in the name of their 'small capital letter' god.
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom