Chama cha Wamiliki wa Mabasi (TABOA) chapinga Kanuni za Latra kwa madai kuwa zinawakandamiza

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
2,664
2,000
Chama cha Wamiliki wa Mabasi Tanzania (Taboa), wamepinga kanuni za sheria ya usafirishaji iliyoweka masharti mbalimbali ikiwamo kuwataka wamiliki kuwajibika pindi mizigo ya abiria inapopotea.

Wakizungumza wakati wa mkutano wa wamiliki hao kujadili kanuni za sheria hiyo zilizotolewa na Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchikavu Tanzania (Latra) na kutoa maamuzi, walisema hawakubaliani na uwajibikaji huo kwa kuwa dhamana ya mizigo ya ndani ya basi ipo kwa abiria.

Walisema kwa kanuni hizo mpya, itakuwa ni wajibu wa mmiliki wa basi kutunza mizigo iliyolipiwa na isiyolipiwa (ya mkononi) ya abiria, jambo ambalo alisema ni gumu kwao, kwa kuwa mizigo isiyolipiwa abiria na thamani yake haijasajiliwa popote, hivyo ni ngumu kujua kiwango cha mizigo aliyonayo.

“Wewe umepanda gari kuna mizigo imewekwa kwenye buti, hivyo tuna rekodi zake kuwa ipo wapi na imelipiwa, tatizo ni wewe umepanda ndani ya gari una mizigo mingine ikiwamo vitu vya thamani kama simu halafu vikaibiwa baadaye unasema umepoteza simu ya Sh. milioni 2 kumbe ni Tecno ya Sh. 300,000,” alisema mmoja wa wasafirishaji.

Jingine wanalopinga ni gari ikiharibikia njiani mmiliki atatakiwa kuleta gari lingine ndani ya saa nane, jambo ambalo ni gumu kwa kuwa kanuni hazijaangalia uharibifu huo utakuwa umetokea wapi.

Wasafirishaji hao walisema watatumia njia mbili, mojawapo ni ya kisiasa kwa kuwasiliana na viongozi wa kisiasa na wakiona hawapati msaada watakwenda mahakamani kudai mabadiliko.

Aidha, wasafirishaji hao walisema kanuni hizo ni ngumu na zenye vikwazo vingi kwa ustawi wa kiuchumi wa wamiliki hao.

Awali, Katibu Mkuu wa chama hicho, Enea Mrutu, alisema kanuni hizo mpya zilizo katika Sheria ya Usafirishaji ya Mwaka 2019 ya Mamlaka hiyo sio rafiki na zina mazingira ya kuwakandamiza wamiliki wa mabasi.

“Kanuni mpya za usafirishaji za mwaka 2020 zilizowekwa sisi hatukushirikishwa na kwa kweli ni kandamizi na zisizo tekelezeka,” alisema Mrutu.

Alisema kwamba chini ya kanuni hizo mpya, Latra ndiyo yenye jukumu la kuidhinisha mtoa huduma ya vidhibiti mwendo katika mabasi (VTS), jambo ambalo limepingwa vikali na wamiliki hao wa mabasi kwa maelezo kuwa gharama zitakazotozwa zitakuwa kubwa kupita kiasi, hivyo kutaka uhuru katika kuamua mtoa huduma hiyo.

“Tunalazimishwa mtu atakayetufungia VTS (vidhibiti mwendo) awe ameidhinishwa na Latra, na pia sasa wanataka mtu atakayefungu mifumo ya kukata tiketi kwa njia ya mtandao amwidhinishe yeye, kitu ambacho kinafanya wasafirishaji kupata ugumu kwenye kufanya kazi,” aliongeza.

IPP MEDIA
 
peno hasegawa

JF-Expert Member
Feb 24, 2016
1,795

Ushauri wa bure kwa TABOA.tafuteni biashara nyingine ya kufanya hiyo ya mabasi imewashinda na itaendelea kuwashinda.Enea mrutu ana kampuni yake inaitwa kirumo magari yake ni mabovu kupindukia Sasa unapinga gari ikiharibika ulete gari jingine ndani ya masaa nane.

Utalipata wapi wakati uliyonayo yote ni mabovu?sheria hiyo imekaa vizuri mlikuwa mnawatesa abiria sana.Enea mrutu ukiwakama katibu mkuu waTaboa imarisha kwanza mabasi yako au ununue mengine mapya Jambo ambalo huwezi ndipo uanze kuipinga hii sheria mpya.
 
Fernando sucre

JF-Expert Member
Jul 14, 2018
293
500
Ushauri wa bure kwa TABOA.tafuteni biashara nyingine ya kufanya hiyo ya mabasi imewashinda na itaendelea kuwashinda.Enea mrutu ana kampuni yake inaitwa kirumo magari yake ni mabovu kupindukia Sasa unapinga gari ikiharibika ulete gari jingine ndani ya masaa nane.utalipata wapi wakati uliyonayo yote ni mabovu?sheria hiyo imekaa vizuri mlikuwa mnawatesa abiria sana.Enea mrutu ukiwakama katibu mkuu waTaboa imarisha kwanza mabasi yako au ununue mengine mapya Jambo ambalo huwezi ndipo uanze kuipinga hii sheria mpya.
Hill neno....
 
Bambushka

JF-Expert Member
Jan 9, 2020
1,666
2,000
Mabasi siku hizi yanakuwa kisasa zaidi mengi hayana konda, ni dereva na abiria...mfano Dar Moro..

Sasa abiria waibiane, dereva anawajibika vipi, kwamba hakutunza mzigo wa ndani wa abiria?? It's absolutely ridiculous!

Ni sawa na kusema walimu wa shule za bweni wawajibike na upotevu wa vifaa vya watoto wanavyopoteza mabwenini...

Everyday is Saturday...................... :cool:
 
Mabasi ya Dar Moto, yape muda kidogo SGR inaanza kazi mapema, so hiyo biashara itawashinda tu mapema.hivyo sheria ikae Kama ilivyopitishwa.wamiliki wametesa abiria sana.
 
Bambushka

JF-Expert Member
Jan 9, 2020
1,666
2,000
Mabasi ya Dar Moto, yape muda kidogo SGR inaanza kazi mapema, so hiyo biashara itawashinda tu mapema.hivyo sheria ikae Kama ilivyopitishwa.wamiliki wametesa abiria sana.
Wamiliki ndiyo wanaoiba mizigo anayopakata abiria??nieleweshe tafadhali..

Siku zote, mizigo ya kwenye buti la gari ni dhamana ya basi, hii ikipotea au kuharibika mabasi yanawajibika...
Na mizigo anayoingia nayo ndani abiria ni ya kwake...ataangalia kaiweka wapi..konda hawezi kujua mzigo anaoshuka nao abiria ndiyo aliopanda nao coz haujalipiwa na hauna lebo...
Hii gharama itarudi kwa abiria, TABOA wataleta sheria za kigaidi...mizigo yote kwenye buti...kasoro wallet, maziwa ya mtoto na nepi..

Everyday is Saturday..................... :cool:
 
Alvajumaa

JF-Expert Member
Jul 5, 2018
3,419
2,000
Hiyo kanuni ya kuleta gari baada ya gari kuharibika ni muhimu sana, kuna siku safari moja natoka Mtwara gari iliharibika, saa 6 ya usiku tupo kibiti mpaka nafika Dar ni saa 9 usiku

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bambushka

JF-Expert Member
Jan 9, 2020
1,666
2,000
Mabasi ya Dar Moto, yape muda kidogo SGR inaanza kazi mapema, so hiyo biashara itawashinda tu mapema.hivyo sheria ikae Kama ilivyopitishwa.wamiliki wametesa abiria sana.
Hiyo SGR ndiyo ukipoteza mzigo ulioingia nao ndani watakulipa??

Je, nauli itakuwa ngapi??kila mtanzania ataimudu?? Msongamano?? Maana yaweza kuwa shubiri tu kama huu mwendokaraha wa DART.

Pili, je kutakuwa na usafiri wa treni muda wote au ndiyo 12asubuhi, saa 4asubuhi, saa 8mchana na 12jioni??

Abiria abakie akichunga mzigo wake anaoingia nao ndani ya basi....

Everyday is Saturday...................:cool:
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom