Chama cha Wamiliki wa Mabasi chatangaza mgomo wa usafirishaji abiria na mizigo

Sijui kama hii ni nakala ya andiko rasmi la kanuni husika, ila kama ndiyo, basi licha ya matatizo ya kutokutekelezeka kwa baadhi ya vipengele vya kanuni hizo, mathalani kumfutia leseni mmiliki kwa kosa la chombo chake kusababisha ajali iyenye kuleta vifo au majeruhi, lakini uandishi pia hauko makini. Kwa mfano na sababu gani kuwa na sehemu zingine chombo kinaitwa basi, na zingine kinaitwa gari?
Mkuu mimi nakubaliana nawe kwenye andiko la rasimu lina kasoro na makosa. SUMATRA waendele kupokea maoni ya wadau na kufanya Public hearing ya kutosha nchini siyo ile ya Dar-es-salaam pekee yake haitoshi.
 
Kenyatta ameshajitolea msaada wa Matatuu kuja kusaidia Usafiri Tanzania Migomo oyeee Gomeni tu... Ni Viongozi wa Africa na hata nyie mkachaguliwa mtakuwa hivyo hivyo no kutatua zaidi ya kukomoa tu...
 
Hii sheria kichaa kabisa. Inaendana kinyume na sheria ya trafic act pamoja na makosa ya barabarani.
Kosa la driver kinalotokana na uzembe halimhusu mwenye gari.
Mwenye gari analo jukumu la fidia , yaani liability kwa third party .
Makosa ya criminal au jinai la trafic accident sio lake.
Hii sheria kichaa ni sawa na kuwambia musifanye hii biashara...na mtu anayejitambua hawezi kuingia biashara hii.
Hata kisheria tu kama kampuni ni limited liability basi ..inayowajibika ni kampuni sio ma directors.
Jee kama ni hivvo Dart mwendo wa kasi wakisababisha ajali wafungwe ma share holder wote akiwamo waziri ?
Mambo mengine tunafanya kwa kukurupuka tu...
Wako sahihi kugoma kabisa
 
WaTz wengi wamepoteza maisha, kupata vilema, kunyanyaswa kstiks sekta ya usafiri. Wamiliki wapate fursa ya kukaa na mamlaka, ila sijsons ubaya wa sheria hizi, ukizingatia jinsi wamiliki walivyozembea katika kuhakikisha wateja wao wanathaminiwa.
 
Kiuhalisia kila mtumia barabara na vyombo vya usafiri anatakiwa kuwajibika. Nimeona kwenye nchi za wenzetu kila mtu ana wajibu wake katika kutumia barabara na vyombo vya moto, mfano abiria asipofunga mkanda, au kuvaa kofia ngumu hilo ni kosa lake. Na gari ikiwa mbovu barabarani hilo ni kosa la wote, mwenye gari na mwendesha gari.
 
elfu 5 yangu imesalimika nilikwiaha iandaa kwa hofu ya kukosa daladala! na huko kwingine vipi kuna mgomo? au mme salimika kama sisi wadom
 
Jiamgalieni na mgomo wenu huyu jamaa hajaribiwi..
Hv Katibu wa chama cha madereva aliishia wapi aliposimamia mgomo kipindi kile

Sent from my TECNO P5 using JamiiForums mobile app

Usiwatishe bwana! Hakuna mwanadamu asiyejaribiwa labda kama katoka huko kusikojulikana. Waache wagome kama wameona hiyo ndiyo njia mwafaka. Punde na wafanyakazi watagoma maana hakuna atakayeendelea kuvumilia kutopandishwa mshahara wala daraja kwa miaka mitano.
 
Back
Top Bottom