Chama cha Wamiliki wa Mabasi chatangaza mgomo wa usafirishaji abiria na mizigo

Mbona ipo vizuri. Sijaona ubaya wowote kwenye huu utaratibu mpya.
Mwanabodi tatizo la wamiliki hawataki kuchangia kuonyesha hizo kasoro za kwenye hiyo rasimu! kama kuna marekebisho yafanywe wao day one walianza kuonyesha kuwa watagoma zikipitishwa. Ni lazima nikiri kuwa SUMATRA hawakutoa muda wa kutosha kupokea maoni ya wadau mjadala ulikuwa wa siku moja tena mji wa Dar-es-salaam pekee yake wangeufanya hata na baadhi ya mikoa.
 
Chama cha Wamiliki wa Mabasi(TABOA) kwa kushirikiana na Wamiliki wa Malori na Chama cha Wasafirishaji Mkoa wa Dar es Salaam kimetangaza mgomo wa usafirishaji abiria na mizigo nchi nzima kuanzia siku ya jumatatu ili kushinikiza serikali kutopitisha sheria ya usafirishaji inayotarajiwa kusomwa mara ya tatu na kupitishwa siku ya Jumanne wiki ijayo.

Akitoa maazimio hayo yaliyofikiwa katika mkutao mkuu maalumu wa chama cha wamiliki wa Mabasi, Malori, Daladala na Baji, katibu mkuu wa TABOA Bwana. Eneo Mrutu amesema sheria inaloyolenga kupitishwa haikuwashirikisha wadau na haitenganishi makosa ya dereva na mmiliki, hali inayosababisha kosa lililofanywa na dereva linasababisha mmiliki kufungwa jela.

Aidha amewaomba wabunge bila kujali itikadi za vyama vyao kutopisha sheria hiyo mpaka ifanyiwe marekebisho kwa kuwa inalenga kuharibu sekta ya usafirishaji nchini.

Chanzo: ITV

mafuta yakipanda nauli ziko palepale vipuli pia hamuangalii hilo sumatra mje muweke vyombo vya usafir muone kama mtayaweza haya
 
Hii sheria ikipitishwa nita wadharau sana wabunge.
Yaani watz huwa wanalalama tu bila hata kujua kitu. Hizo kanuni za SUMATRA wala haziendi bungeni ni nzuri tu zinampa mwajiri wajibu ikitiliwa maanani yeye ndo anaomba leseni Sumatra. Majukumu ya dreva ni kuendesha gari na makosa atakayotenda kuhusiana na uendeshaji wa gari yeye ndo atakuwa responsible. Wamiliki wasikwepe majukumu yao!
 
Jukumu gani unalozungumzia hapa, umeisoma vizuri hiyo sheria.

Mmiliki ananunua suti then Dereva na konda wasipo zivaa mmiliki anahusika vp hapo.
Yani manayake mmiliki azurule na gari kilasiku ilikuhakikisha dereva anavaa suti??.

Dereva akikatisha ruti mmiliki anahusika vipi, unafungia leseni kwasababu dereva amekatisha ruti??

Mmiliki hukoaliko anajua kwamba dereva anakatisharuti huko barabarani??.
 
[HASHTAG]#Waache[/HASHTAG] wagome mabasi yao walinunua wao Na hakuwasindikiza mtu kuyanunua # msiwapangie mtapanda ungo trans
 
Nasikia ni kiki ya Mzee! Atakuja from no where kuifuta sheria hiyo, si mnajua "Mzee wa makiki kama msaniiiii" in Nikki wa pili's voice
 
Jukumu gani unalozungumzia hapa, umeisoma vizuri hiyo sheria.

Mmiliki ananunua suti then Dereva na konda wasipo zivaa mmiliki anahusika vp hapo.
Yani manayake mmiliki azurule na gari kilasiku ilikuhakikisha dereva anavaa suti??.

Dereva akikatisha ruti mmiliki anahusika vipi, unafungia leseni kwasababu dereva amekatisha ruti??

Mmiliki hukoaliko anajua kwamba dereva anakatisharuti huko barabarani??.

Nijukumu lake kununua suti wamekuwa hawataki kununua suti za madereva pia ni jukumu lake kumsimamia dereva asikatishe ruti. Akiwalipa vizuri madereva si dhani kama dereva atakuwa kichaa wa kukatisha ruti. Kuna gari nyingi madereva wanamikataba mizuri hawafanyi ujinga huo. Duniani kote mwajiri anajukumu kwa mwajiriwa wake kwa nini ishindikane kwa wenye magari hapa TZ tu???
 
Sasa hivi huwezi kupata ruti sumatra kama dereva hana mkataba.

Unaposema mkataba mzuri huo mkataba mzuri unadhibitishwa na nani?.

Ukiona gari ya abiria inafanya kazi barabarani ujue dereva anamkataba uliodhibitishwa na Sumatra ndio maana gari imepata ruti.

Sasa sijuiunaongelea mkataba upi mizuri atakao mfanya dereva asifanye makosa.
 
Nijukumu lake kununua suti wamekuwa hawataki kununua suti za madereva pia ni jukumu lake kumsimamia dereva asikatishe ruti. Akiwalipa vizuri madereva si dhani kama dereva atakuwa kichaa wa kukatisha ruti. Kuna gari nyingi madereva wanamikataba mizuri hawafanyi ujinga huo. Duniani kote mwajiri anajukumu kwa mwajiriwa wake kwa nini ishindikane kwa wenye magari hapa TZ tu???
mkuu nauli zinapangwa na haohao uhasama, mikataba ya madereva inasajiriwa na haohao uhasama, wekeni nauli ya dar mwanza iwe laki nane muone kama madereva hawatalipwa vizuri..
 
Nijukumu lake kununua suti wamekuwa hawataki kununua suti za madereva pia ni jukumu lake kumsimamia dereva asikatishe ruti. Akiwalipa vizuri madereva si dhani kama dereva atakuwa kichaa wa kukatisha ruti. Kuna gari nyingi madereva wanamikataba mizuri hawafanyi ujinga huo. Duniani kote mwajiri anajukumu kwa mwajiriwa wake kwa nini ishindikane kwa wenye magari hapa TZ tu???

kuna mambo yameshafanyika huko "duniani" kweli ni mazuri je kwetu hapa unauhakika wakati wake ndio huu au unahitajika muda ebu cheki mwendokasi mpaka inafikia yanagongana yenyewe kwa yenyewe......ukizungumzia mishahara mizuri(Bima ya afya, mafao ya uzeeni, likizo n.k) kwa madereva wa daladala na kondakta wake hivi bado nauli itakuwa ni 400 au itashuka...SUMATRA hii hii inayosema itakata ushuru kwa kila chombo ya usafiri unao pakia abiria kuanzia wawili ila sasa hivi wanalazimisha boda boda walipe ushuru wakati boda inapakia abiria mmoja....
 
Hizo sheria ni nzuri sana nimep3nda acha zipite zifanye kazi madreva wanafanya safar ndefu na hakuna muda mzur wa kupumzika mf dar to sumbawanga

Kwa njia hii pia madreva wengine watapata ajira kupitia sekta hiyo

Kikubwa sheria zinalenga usalama wa abiria
 
kuna mambo yameshafanyika huko "duniani" kweli ni mazuri je kwetu hapa unauhakika wakati wake ndio huu au unahitajika muda ebu cheki mwendokasi mpaka inafikia yanagongana yenyewe kwa yenyewe......ukizungumzia mishahara mizuri(Bima ya afya, mafao ya uzeeni, likizo n.k) kwa madereva wa daladala na kondakta wake hivi bado nauli itakuwa ni 400 au itashuka...SUMATRA hii hii inayosema itakata ushuru kwa kila chombo ya usafiri unao pakia abiria kuanzia wawili ila sasa hivi wanalazimisha boda boda walipe ushuru wakati boda inapakia abiria mmoja....
naona kwa hili nauli zitashuka, dereva wa bajaj umkatie bima ya afya umlipie nssf umlipie paye umdhamini na mkopo nmb kwa hiyohiyo 400? lazima nauli ishuke kidogo.
 
hah hah ha ha shida hapa tunakurupuka.......
 
kuna mambo yameshafanyika huko "duniani" kweli ni mazuri je kwetu hapa unauhakika wakati wake ndio huu au unahitajika muda ebu cheki mwendokasi mpaka inafikia yanagongana yenyewe kwa yenyewe......ukizungumzia mishahara mizuri(Bima ya afya, mafao ya uzeeni, likizo n.k) kwa madereva wa daladala na kondakta wake hivi bado nauli itakuwa ni 400 au itashuka...SUMATRA hii hii inayosema itakata ushuru kwa kila chombo ya usafiri unao pakia abiria kuanzia wawili ila sasa hivi wanalazimisha boda boda walipe ushuru wakati boda inapakia abiria mmoja....

Acheni sababu mifumo hii tumekopi toka huko ulaya kwa nini tusiweze?? Tuanze kama kutakuwa na changamoto ndo maisha bila changamoto hatuwezi kuendelea tusiogope changamoto!!
 
Sasa watakaoathika ni wasiokuwa na makosa mm naona wangegoma madereva wa wabunge
 
Sijui kama hii ni nakala ya andiko rasmi la kanuni husika, ila kama ndiyo, basi licha ya matatizo ya kutokutekelezeka kwa baadhi ya vipengele vya kanuni hizo, mathalani kumfutia leseni mmiliki kwa kosa la chombo chake kusababisha ajali iyenye kuleta vifo au majeruhi, lakini uandishi pia hauko makini. Kwa mfano na sababu gani kuwa na sehemu zingine chombo kinaitwa basi, na zingine kinaitwa gari?
 
Back
Top Bottom