YEHODAYA
JF-Expert Member
- Aug 9, 2015
- 36,909
- 51,904
Hakuna njia yoyote ya mabasi ya daladala yenye uhakika wa kuingiza pesa nyingi kama njia ya mabasi yanayoenda kawe liliko kanisa la Mtume na Nabii Bulldoza Mwamposya.
Daladala wanapiga ROUTE na kupakia hadi basi hadi zinashindwa kuhimili uwingi wa watu wanaofurika kwa Mwamposya.
Wamiliki wa daladala ombeni mamlaka ziongeze usajili wa mabasi ya kwenda Kawe kwa Mwamposya kuwe na route nyingi za kutoka kila kona ya jiji kwenda kwa Bulldoza Mwamposya.
Kawasaidia sana daladala kuwaongezea mzunguko wa pesa.
Vyama vya wafanyabiashara na wamiliki wa daladala ni vizuri kuwatunuku watu kama Mtume na Nabii bulldoza Mwamposya kwa kuwasaidia kuingiza mapato.
Nakumbuka pale Kenya kuna kanisa kiwanda cha Cocacola kilijitolea kujenga sababu hilo kanisa ndio lilikuwa likiongoza kwa unnywaji wa bidhaa za Cocacola kwa kuwa na umati mkubwa kama wa Buldoza Mwamposya. Lile kanisa liliamriwa na mmiliki wa kiwanja wahame wakawa hawajui waende wapi kiwanda cha Cocacola kikatafuta eneo na kujenga kanisa kwa mikataba kuwa bidhaa za Cocacola tu ndio ziwe zinatumika.
Wafanyabiashara ule umati wa Buldoza Mwamposya ni fursa. Ni bahati mbaya wafanyabiashara hawajui hawa watu kama mzee Mwasapile wa Kikombe cha Babu na wakina Buldoza Mwamposya waweza badili kabisa mzunguko wa fedha na kuwasaidia wafanyabiashara biashara zao kwenda juu mno.
Mzee Mwasapile wa kikombe cha Babu aliinua biashara na uchumi wa Arusha kwa kiwango cha juu mno ila viroho vya korosho vya Watanzania viliharibu.
Wenzetu mfano Nigeria wana TB Joshua mjengo wake ulianguka ukaua watu kibao wenye viroho vya korosho wakataka TB Joshua afungiwe serikali ikagoma kutokana na mamilioni ya midola inayoingia Nigeria na na daladala zinavyoingiza pesa wakaona itaua ajira serikali ikampa minishani kibao TB Joshua na kumwacha aendelee na shughuli zake
Wamiliki wa daladala kuweni na shukrani kwa mtume na nabii Buldoza Mwamposya.