Chama cha wamiliki wa daladala, mpeni tuzo Nabii Mwamposya kwa kuwasaidia kuingizia mapato makubwa kwenye biashara zenu

YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
27,439
2,000
Hakuna njia yoyote ya mabasi ya daladala yenye uhakika wa kuingiza pesa nyingi kama njia ya mabasi yanayoenda kawe liliko kanisa la Mtume na Nabii Bulldoza Mwamposya.

Daladala wanapiga ROUTE na kupakia hadi basi hadi zinashindwa kuhimili uwingi wa watu wanaofurika kwa Mwamposya.

Wamiliki wa daladala ombeni mamlaka ziongeze usajili wa mabasi ya kwenda Kawe kwa Mwamposya kuwe na route nyingi za kutoka kila kona ya jiji kwenda kwa Bulldoza Mwamposya.

Kawasaidia sana daladala kuwaongezea mzunguko wa pesa.

Vyama vya wafanyabiashara na wamiliki wa daladala ni vizuri kuwatunuku watu kama Mtume na Nabii bulldoza Mwamposya kwa kuwasaidia kuingiza mapato.

Nakumbuka pale Kenya kuna kanisa kiwanda cha Cocacola kilijitolea kujenga sababu hilo kanisa ndio lilikuwa likiongoza kwa unnywaji wa bidhaa za Cocacola kwa kuwa na umati mkubwa kama wa Buldoza Mwamposya. Lile kanisa liliamriwa na mmiliki wa kiwanja wahame wakawa hawajui waende wapi kiwanda cha Cocacola kikatafuta eneo na kujenga kanisa kwa mikataba kuwa bidhaa za Cocacola tu ndio ziwe zinatumika.

Wafanyabiashara ule umati wa Buldoza Mwamposya ni fursa. Ni bahati mbaya wafanyabiashara hawajui hawa watu kama mzee Mwasapile wa Kikombe cha Babu na wakina Buldoza Mwamposya waweza badili kabisa mzunguko wa fedha na kuwasaidia wafanyabiashara biashara zao kwenda juu mno.

Mzee Mwasapile wa kikombe cha Babu aliinua biashara na uchumi wa Arusha kwa kiwango cha juu mno ila viroho vya korosho vya Watanzania viliharibu.

Wenzetu mfano Nigeria wana TB Joshua mjengo wake ulianguka ukaua watu kibao wenye viroho vya korosho wakataka TB Joshua afungiwe serikali ikagoma kutokana na mamilioni ya midola inayoingia Nigeria na na daladala zinavyoingiza pesa wakaona itaua ajira serikali ikampa minishani kibao TB Joshua na kumwacha aendelee na shughuli zake

Wamiliki wa daladala kuweni na shukrani kwa mtume na nabii Buldoza Mwamposya.
 

red apple

JF-Expert Member
Dec 6, 2012
521
1,000
Siku ya kwanza nilishangaa sana kukuta umati mkubwa barabarani, kuuliza naambiwa wametoka kanisani kwa Mwamposya,Natamani Siku moja niende kwenye ibada yake, nami nishuhudie kinachowavuta watanzania wenzangu.
 

YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
27,439
2,000
Siku ya kwanza nilishangaa sana kukuta umati mkubwa barabarani, kuuliza naambiwa wametoka kanisani kwa Mwamposya,Natamani Siku moja niende kwenye ibada yake, nami nishuhudie kinachowavuta watanzania wenzangu.
usipime wakitoka foleni ya magari utakoma .ENEO la kanisa la MWAMPOSYA Traffic wanatakiwa kuwepo kuongoza magari hasa muda wa watu kutoka ibadani maana si umati tu wa watu lakini pia kuna umati wa magari binafsi wanaosali pale.KUTOKA ibadani ni patashika nguo kuchanika magari foleni inaanzia kanisani,waweza tumia saa nzima hujatoka viwanja vya kanisa kufika barabarani wakati ni eneo fupi tu la hatua mia tu
 

YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
27,439
2,000
Siku ya kwanza nilishangaa sana kukuta umati mkubwa barabarani, kuuliza naambiwa wametoka kanisani kwa Mwamposya,
HUO UMATI HUTEMBEA sababu ya upungugufu wa daladala za kawe wengi huenda kwa miguu toka kawe hadi mwenge au morocco kutafuta usafiri wa kwenda sehemu mbalimbali za jiji sababu daladala za kawe huzidiwa abiria haziwezi beba wote

SUMATRA ongezeni mabasi ya kwenda kawe au mwendokasi jumapili mfano njia nyingi mabasi yenu huwa matupu pelekeni mabasi yenu kawe mida ya watu kutoka ibada ya kwanza na ya pili muone kama faida ya wiki nzima hamtaipata siku hiyo ya jumapili tu peke yake
 

mwasu

JF-Expert Member
Jul 13, 2011
10,196
2,000
Imani ni kazi sana, kuna siku nilialikwa na wafuasi wake oooh! twende tukakanyage mafuta nikaenda nikayakanyaga ajabu sioni tofauti yoyote kabla na baada, ina imani sana na Mungu lakini sina imani na binadamu kabisa, kulishana keki na kukanyaga mafuta NADHANI ina hitaji imani haswa kwa MWAMPOSYA.
 

YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
27,439
2,000
Imani ni kazi sana, kuna siku nilialikwa na wafuasi wake oooh! twende tukakanyage mafuta nikaenda nikayakanyaga ajabu sioni tofauti yoyote kabla na baada, ina imani sana na Mungu lakini sina imani na binadamu kabisa,
BIBLIA KATIKA 2 Nyakati 20:20 inasema ; mwaminini Bwana, Mungu wenu, ndivyo mtakavyothibitika; waaminini manabii wake, ndivyo mtakavyofanikiwa.

KUMWAMINI mungu kunakupa kuthibitika imani yako mbele zake

kufanikiwa unatakiwa umwamini nabii

.WEWE kama humwamini nabii hata ungekanyaga na kuoga na kunywa mafuta ya upako hufanikiwi kabisaa usitarajie hali yako kubadilika.

WAAMINI MANABII tumefanikiwa .Wachovu wengi makanisani ni wale wasioamini manabii .Wachungaji wao wamechoka na makanisa yao yamechoka na waumini choka mbaya

Hata wewe kama utaendelea kutoamini manabii hali yako haitabadilika kaoge maji ya upako mafuta au maziwa ya upako kula hata keki lote la upako peke yako hufanikiwi kama huamini nabii
 

chokodari

JF-Expert Member
Jun 2, 2015
642
500
Imani ni kazi sana, kuna siku nilialikwa na
wafuasi wake oooh! twende tukakanyage
mafuta nikaenda nikayakanyaga ajabu sioni
tofauti yoyote kabla na baada, ina imani sana
na Mungu lakini sina imani na binadamu kabisa, kulishana keki na kukanyaga mafuta
NADHANI ina hitaji imani haswa kwa
MWAMPOSYA.
Wewe huna imani kuna watu wanafanikiwa pale wengi sana mbaka wasanii wakubwa wengine waislam wanasali pale majina kapuni so ni bora ukae kimya kuliko kukebehi haipendezi
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom